LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
Ilikuwa ni mwezi wa saba sikumbuki tarehe ndo niliaga JF na kuelekea kijijini nikitokea Dar, baada ya kumaliza mafunzo ya ufundi, na nikijiapiza mjini ntarudi kutembea tu. Lakini hapa ninapoandika huu ujumbe nipo nimelalia maboksi kwenye geto la kupanga baada ya kuungua na maisha ya kijijini huku nikiwa na ujuzi wangu vizuri tu. Kwanza kabisa mimi ni fundi - simu, radio, umeme wa majumbani. Natengeneza video mbali mbali na vitu vingi vingi tu vinavyotumia umeme.
Changamoto za kijijini:
Asanteni nawasilisha
Changamoto za kijijini:
- Upatikanaji haraka wa diode au spea za maredio tv nk.
- Umbali wa kuvifikia nauli 12000 kwenda na kurudi.
- Intaneti, unapokuwa unahitaji msaada wa kiufundi kupitia google
- Kazi za msimu
- Wateja wengi ni malialia n.k
Asanteni nawasilisha