DA HUSTLA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 3,805
- 4,107
Ilikuwa ni mwezi wa saba sikumbuki tarehe ndo niliaga JF na kuelekea kijijini nikitokea Dar, baada ya kumaliza mafunzo ya ufundi, na nikijiapiza mjini ntarudi kutembea tu. Lakini hapa ninapoandika huu ujumbe nipo nimelalia maboksi kwenye geto la kupanga baada ya kuungua na maisha ya kijijini huku nikiwa na ujuzi wangu vizuri tu. Kwanza kabisa mimi ni fundi - simu, radio, umeme wa majumbani. Natengeneza video mbali mbali na vitu vingi vingi tu vinavyotumia umeme.
Changamoto za kijijini:
Ndo vimenifanya leo hii nimelala kwenye mabox na vifaa vyangu vya kazi hapa Arussha mjini leo hii
- Upatikanaji haraka wa diode au spea za maredio tv nk.
- Umbali wa kuvifikia nauli 12000 kwenda na kurudi.
- Intaneti, unapokuwa unahitaji msaada wa kiufundi kupitia google
- Kazi za msimu
- Wateja wengi ni malialia n.k
Asanteni nawasilisha
We nae una ufundi huo unaenda kijijini kufanya si ungebaki hapa Dar ukakimbiza mdogo mdogo.
Anyways, kumbe Arusha ni kijijini, una taka ugomvi na machalii.
Sent using Jamii Forums mobile app