Nilijiona mjanja kumbe mjinga tu, hatimaye leo nimetapeliwa

Duh bado kuna watu wanapigwa Kwa style hizi kumbe safari bado ndefu sana..
 
Hii niliwahi kuiskia maeneo ya Mwanjelwa pale, Aliyepigwa alikuwa mwanamke alibaki tu kupiga kelele wajamaa washakula ndefu. Sema pole Mkuu
 
Vijana wa Mbeya ni Washamba sana,haya mambo yamekuwepo huko Usukumani zaidi ya miaka 50 wewe leo ndo unagutuka umepigwa?

Wewe mshamba wa Songwe Lucas mwashambwa hebu njoo umuone ndugu yako huku!
 
Hivi huu utapeli Wa kizamani hivi Bado upogo tu na watu wanapigwa mi nilitapeliwaga Kwa staili hii 2018
 
Chai hi Hadi SAS unatapeliwa kwa gia hyo SAS s utoke humu tumesha Seema magret thinker hawatapeliwi kijinga
 
LEO BORN TOWN NIMETAPELIWA/NIMEIBIWA,

SIJUI ILIKUWAJE, NIMEBAKI NAJICHEKA TU.

Basi bhana leo jumapili ya tarehe 17-03-2024 nikaamka zangu maghetoni nikasema wacha nikanunue boxer kabwe, nikachukua zangu tsh 30,000/= nikaweka mfukoni nikabeba begi langu nimenunua juzi buku 23 nikaliweka mgongoni, wakati nataka nitoke nikaiona simu yangu nayo haina hata wiki samsung galaxy note 10+ 5g ya Gb 512 ram Gb 12 nilinunua 450,000 dar na kadi ya benki nilitaka nikatoe kama laki moja hivi maana nilikuwa sina balance ndani.

Nikawaza nikasema ngoja simu kubwa niiache na kadi ya benki pia nayo niiache, niondoke tu na 30k pamoja na begi la mgongoni na kiswaswadu.

Nimefika kabwe nikanunua boxer za 15k, karanga za kutafuna za 1,700 na mche wa sabuni wa buku 3. Nikabakiwa na 10k na shilingi mia nane maana nilitoka na buku la nauli home.

Sasa wakati natoka mle sido naitafuta bajaji nikakutana na fala mmoja hivi akanisalimia nikamjibu akawa ananiulizia ofisi za TMC zilipo, mi nikamjibu kuwa sijui, palepe akatokea jama mwingine naye akamuuliza wapi zipo ofisi za TMC, akawa anamuuliza huku anamuonesha kipakiti kidogo kina madini ya dhahabu kwamba anataka ayapeleke ili akayauze yeye hapajui.

Jamaa wa kile kimadini nitamuita hassani, na jamaa huyu mwingine aliyeulizwa pamoja na mimi nitamuita kessy, (majina ya kufikirika ili kurahisisha usimuliaji).

Basi bhana kessy akawa anamfokea hassan kwamba inakuaje anakuwa mpumbavu anauliza na kuonyesha mali hovyo hovyo, vipi akikutana na watu wenye nia ovu wakamuibia?,

Kile kipakiti kilichokuwa na dhahabu kilikuwa kimeandikwa "Dhahabu grade A, yenye thamani ya milioni 30".

Kessy akaendelea kumfokea hassan, "wewe umetoka wapi?, umebeba mali kiasi hiki na hata hujielewi", "kwanza ofisi za TMC hazipo hapa", aliendelea kessy.

"Dogo unamuelewa huyu?, hana akili hata kidogo" kessy alikuwa akiongea huku ananiangalia mimi,.

Kisha kessy akaanza kumuuliza hassan,
kessy: "vipi kama tukikusaidia kukupeleka ukauza mzigo wako sisi utatupatia shingapi ngapi?
Hassan: "mimi nitawapa tuu hata makumi mawili mawili nitawapa",
Kessy: "we fala nini?, sisi tunataka tukusaidie afu utupe elfu ishirini ishirini?, utatupatia hata 200k kila mtu",
Hassan: "nyie nisaidieni kwanza mengine tutaangalia".
Kessy: "dogo twende tumpeleke kwa mama mchungaji tukamsaidie kuuza" kessy akaniambia mimi huku akionyesha kuanza safari, Bad enough nikakubali kujoin the troop, hapo ndipo nikaenda kupigwa.

Tukaanza safari ya kuelekea kuuza "mzigo" ili tupige hela, tukiwa njiani hassan alionesha kuwa na mashaka sana akihofia kwamba tutaenda kumpiga mzigo wake.

"Mimi hapa nimeagizwa majembe ya kulimia na machepe nataka niuze haraka niwahi chunya, kwanza hapa tupo wapi?, nionyesheni njia ya stendi mimi nirudi chunya" alikuwa anaongea hassan huku akionyesha hofu ya kuibiwa.

Mimi na kessy tukawa tunafanya kazi kubwa sana ya kumpunguza wenge hassan ili asiachane nasi tusije tukakosa hela.

"Sasa nyie tangulieni mimi mniache nyuma msije mkanikaba mniibie, mimi nawafuata" aliongea hassan na sisi tukawa tunafanya kama anavyosema ili kumtoa hofu.

Tukiwa tumetangulia mbele mimi na kessy tukawa tunaambiana kwamba hapa hili ni dili letu wawili, tunapiga hela na yeye (hassan) tunampa hela kidogo maaana anaonekana haelewi chochote, nami nikawa namuunga mkono kessy huku wote tukiwa tunageuka geuka kumuangalia hassan kama anaendelea kutufuata.

Tukafika sasa hapo karibu na sehemu ya kuuza mzigo.

Kessy akasema sasa dogo wewe tulia hapa na haasan mimi naenda kucheki mazingira ya kuuza mzigo, mimi nikasema sawa, hilo halina shida, nikabaki na hassan huku nikiendelea kumpanga kuwa atulize wenge.

Baada ya dakika chache kessy akaja akiwa ameshika karatasi ndogo mfano wa zile zinazokuwa ndani ya pakiti ya sigara zinazofanana na aluminium foil, akampa hassan huku akimuambia "mnunuzi amesema weka mzigo humu ukiuacha wazi utaharibika", hassan akachukua akaweka mzigo ndani ya karatasi.

"Sasa mnunuzi kasema atanunua kwa 29.7m maana 300k anataka alipie ushuru, kasema tuende NMB bank soweto yeye ametangulia na gari", alisema kessy.

Hassan akawa anauliza ni wapi huko?, tukaanza tena kazi ya kumuelekeza.

Hassan akasema sawa twende ila wewe sikuamini(kessy), hivyo ili msije mkanikaba, nipeni vitu vyenu nishike mimi, kessy kwa haraka akatoa wallet yake na kumpa hassan ili amuamini huku akisisitiza kuwa wallet ina 240k ndani, nami nikasema hapa nisibaki nyuma, nikatoa kisimu changu kidogo nikampa ashike pamoja na ile 10k iliyobaki, hassan akawa anakataa akisema kwamba tumempa vitu vidogo, tumuongeze hela.

Mimi nikarudisha vitu vyangu mfukoni na kessy akachukua wallet yake, tukamwambia hassan kuwa aendelee kubaki na mzigo huku tukienda benki tukifika ndio atautoa.

Hassan akabaki na mzigo huku tukianza kuifuata benki ya NMB ili tukutane na mnunua madini tumalize biashara, sheria ikawa ni ileile, kuwa mimi na kessy tunatangulia mbele na hassan anatufuata.

Baada ya hatua kazaa hassan akasimama na kuanza kurudi nyuma, kessy akasema "dogo hebu tumuwahi tumpange twende benki, hatuwezi kuikosa hii hela" nami nikasema kuwa ni wazo zuri kabisa. Tukaanza kumfuata hassan taratibu bila kumkimbiza ili asiingiwe na mashaka akaogopa na kutemana nasisi.

Tukamkuta na kuanza tena kumshawishi, tukaanza tena kumpa vitu ashike ili atuamini, mimi nikamuongezea na begi langu likiwa pamoja na vile vitu nilivyonunua ma kunipa mimi mzigo niushike.

Mimi nikapokea na kuuweka mfukoni, hassan akasema kuwa mimi ndio nibaki na mzigo na sio kessy, maana kessy anaonekana jambazi, mimi nikaona sio shida nikabaki na mzigo huku nikitangulia mbele ili tukifika pale banki mimi ndio niongee na mnunuzi, tulivyozidi kusonga mbele kessy akaja akaniambia kuwa mimi niende pale nmb nikawasubiri, yule mnunuzi yupo na gari nyeusi, nikawasubiri pale na huku akisisitiza kuwa nisije nikawatoroka.

Mimi nikafata kama walivyosema, nikaelekea benki, na nikawa nageuka nyuma kuona kama wananifuta, na kweli wakawa wananifuata, nikafika pacha ya kuelekea benki nikageuka nyuma niwaone, ni kweli wakawa wanakuja ila gap kati yangu na yao lilikuwa kubwa sana, nikasema sio shida ngoja niendelee kwenda benki.

baada ya kama hatua 20 nageuka nyuma wale jamaa siwaoni, nikasema wacha nicheki mzigo kwanza, nikaangalia hivi OMG ni mchangaa. Dah!. Nikacheka sana huku nikiwaza kadi yangu ya benki na Note 10 yangu, vipi kama ningevibeba?,.

Kiukweli nilijiona mjinga sana huku nikitabasamu na nikiwa sina hata mia ya nauli,. Ikabidi nianze safari ya kurjea home kwa mguu. Huku nikiwa nishapigwa tukio tayari. Kiukweli niliona gheto ni mbali sana huku nikiwaza ujinga nilioufanya na kukumbuka kuwa kuna jamaa humu jf huwa anasema "when the deal is too good, think twice", lakini nikajipa moyo kwa kurefer kitabu cha Dale carnegie "how to win friends and influence people" kwamba moja ya chapter zake ni "do not condemn, criticise, or complain", huku nikiendelea kurudi home kwa mguu😁😁😁.

IT'S ALL OVER.
Kama nyie ndio born town, basi hii nchi haina town.

Utapeli wa mwaka 1999 huo unapigwa leo 2024?
 
Dah, kitambo sana hii kitu

Huu utapeli nikiwa na Maza mwaka 1994 maeneo ya Kiwalani walitokeaga jamaa wawili hivi hivi wakataka kumtapeli Maza. Shida ni kua Maza aliona udwanzi kuanza kizunguka nao akiwa na Mimi, hapo nina miaka kama 13 hiv.

So kwakua Maza aliona kuanza kuzunguka na mimi itakua tabu akawaambia hawezi kuwasaidia. Lakin hapo Kwenye kuwaachia hela ili wasiwe na wasiwasi wa kukimbia na Mzigo walitaka awape Pete na Saa Seiko5
 
Utapeli wa miaka ya 90 bado unafanya kazi miaka ya 2024 hukuu, kweli mjini kutegemeana
 
Yani huu wizi wa namna hii mara ya mwisho nilikutana nao 2008 pale ubungo …na tena hao wajinga wanajifanyaga wanaongea kisukuma!

Walivyo wajinga hata ukiwashitukia wanapunguza bei hadi hata 60,000/= madini ambayo wanadai ni million kumi kifupi hao wanawatapeli washamba tuu na wenye tamaa ya mafanikio ya haraka!

Kwa akili ya kawaida kweli mtu ana hata ya kutoka chunya na madini wakati masoko uko chunya yapo ya kutosha na bei ni ile ile …? Wewe hadi leo unanasa kwenye mtego wa kizamani namna hii?

Wewe ni mjinga sana
 
Huu wizi wa kitapeli nilikutana nao Tunduma , nikiwa natoka hapa boarder naelekea kule msikitini eneo maarufu kwa jina ilo wanapochenji dola mara namuona jamaa anakimbia mbio spidi kubwa akitokea bondeni ninakotoka mimi akadondosha bonge la butungutu la pesa ambazo ni dola feki.Baada ya kudondosha akatokea jamaa mwingine kwa spidi akaokota lile burungutu na kunipa ishara ni nyamaze nisiongee.Mimi wala sikua na interest na chezo lao ukizingatia Dar hiyo michezo ilifanyika miaka hiyo.Nikabaki naendelea na safari yangu mara jamaa akawa anajitaidi kuniongelesha nikae kimya ili tukagawane hiyo pesa uchochoroni.
Nikamwambia aisee mbona huu wizi au utapeli ni wa kizamani sana tumeupitia manzese ila nakupa ofa moja kama una pesa nikupe mbinu mpya za kutapeli online jamaa akabaki anacheka na kuondoka zake.
 
😂😂😭😭 omg ni mchanga!
Yaaani nipate dhahabu nisijue kwa kuuza😂😂😂
 
na mungu alikukomesha maana na wewe ulishakua na mawazo ya kumtapel yule mwenye dhahab ukawa unadhan dhulma inaenda patupu?
 
Back
Top Bottom