Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Nilimuuliza wewe ni Nani mpaka unitishe hivi?
Alijibu: hapo upo wapi? Mimi Nina hela Sina Sheria.[emoji848][emoji15][emoji848][emoji15][emoji31]
Hii Dunia wakati mwingine ina manyanyaso ndio maana wengi hukochukulia Sheria mkononi inapo bidi
 
Jamaa ni wa TARURA siyo TANROAD?
 
Kwanini unaficha uonevu na unyama kama huu. Inatakiwa useme una utaje kila baya walilokufanyia ili hao watu wajulikane. Wanakuingiza selo bila kuandikishwa mapokezi. Kiongozi ww una tatizo sana. Ushahidi unao huyo jamaa wa TARURA hao walitaka kukuua.
Nimeficha kwasababu za kiusalama kwasababu bado wananisakama
 
All in all jeshi la polisi haliaminiki tena kwa wananchi walio wengi, kwa mambo yao ya kuvunja sheria wanayotufanyia raia.!
Polisi ni wavunjifu wa Sheria na kunyanyasa raia.
 
Nina uhakika kwenye fuvu lako la kichwa kuna ufa kiasi unashindwa kuweka ubongo wako sawa. Sijui umsoma jamaa na kumuelewa ama unaandika upupu bila kuelewa.
Huenda hajasoma na kuelewa
 
Kwa Kuwa hayaja kukuta omba Mungu iendelee kua simulizo kwako
 
Huu ni ukweli
 
Jeshi la polisi Lina mapungufu mengi Sana, wengi hatujatedewa haki, lakini mtu anaeleza yaliyomkuta watu ambao ndio waathirika wanamdhihaki mlalamikaji badala ya kuchangia mawazo ya kulirekebisha. Sasa hivi inaonekana jeshi la polisi Kuna vikundi vya kuwapora fedha wafanyabiashara wa madini na kuwaua, kwa utani tunaofanya hili genge litaimarika sana.Pole Sana mtoa Mada.
 
Huyu siyo wa kumpa pole Mkuu maaana ni tapeli. Arudishe pesa waliyokubaliana na mwenzake Mil 20 aone kama wataendelea kumfuata fuata. Vinginevyo anakoelekea ni kupotea mazima
 
Mimi pia niliwekwa rumande siku tatu,vitisho vingi,,ila sikuteswa...kisa tu polisi alikua anataka Laptop yangu ambayo nimenunua kihalali,Bali sikua na risiti,nilinunua kwa jamaa yangu alitoka nayo China...mwisho wa siku nikawaachia Laptop,na elfu 60..nikatoka...mpaka leo anaitumia MacBook air
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…