Hawa ndo wale wanaotafutaga waume/ wake humu halafu wakishapata, na kumwagana wanamwagana humu humu...
Mpe cha mwisho kwanza cha kuagana ............!
:tape: :love:
hata mawasiliano ya Simu hamna umpe ujumbe wake!!!!!!!!.....
Mpe cha mwisho kwanza cha kuagana ............!
:tape: :love:
Mtoto wetu umemuacha au unaondoka naye!??
Tatizo hatajua mpaka akikukosa ndio atatuletea taarifa,mana ID zenyewe fake.
No, usiondoke muhurumie huyo mtoto!
umekusanya mtaji wa kutosha au ndo unarudi kijijini kwa wazee,kama hujachukua endelea kumvumilia kama mwezi hivi ujichotee rasilimali mwaya.....kitaa ni pagumu thana.
Hii ID si fake ni jina langu mwenyewe hata huko duniani naitwa hivi akiingia humu na kusoma hivi atajua tuu ni mimi na hiyo avatar yangu pia anaijua so akiunganisha dots ya picha na avatar atajua ni mie.
Ooooooooohh sikujua kama utabadilika x2
Baki salamaaaa kuonana nawe ni majaliwaa
Ooooh ulimwengu kweli una mambo mengi mamaaaaaaah x2
Baba mtoto.:wave:
Message zangu hajibu simu yangu hapokei busy mitandaoni, nimerusha message hii kwenye mitandao yote anakoshinda ili ujumbe umfikie na ajue kuwa nimefanya maamuzi na niko siriasi.
Naondoka nae, maana tangu azaliwe hajawahi kumnunulia hata pipi achilia mbali kumsindikiza shuleni na kumpeleka hospitali anapoumwa. Baridi, joto, jua na mvua vyote navipata mimi kwa ajili ya mtoto, siwezi kumuacha mtoto.
Akiamua kukutafuta atakupataje? muachie hata account ya skype. Lakini kumbuka hasira hasara. Mia
Tatizo mnaangalia sana tamthilia.
Mmeo unakuja kumtalikia kwenye mtandao wa kijamii tena wenye ID feki?
He he he, labda kama mlikutana humu humu.
Pole, hapo umejila mwenyewe.
Na mie mke mwenzio leo ndio nahamia rasmi mjengoni,ukinyanyuka tu wenzio twakaa so usije ukabadili mawazo ati