Nikiwa kama Mtz nilipata bahati kufika Nairobi na nilikuwa huko kwa muda wa Mwezi mmoja! Kitu kikubwa kilichonishangaza ni kwamba Kenya au nisema Nairobi kuna Watu wengi sana hakuna Lugha wanayoijua kwa kwa ufasaha, yaani kuna Watu hawawezi kuongea Kiswahili chote kwa ufasaha, pia hawawezi kuongea kiingereza chote kwa ufasaha na cha ajabu kabisa pia hawawezi kuongea vilugha vya kikwao kama kijaluo au sijui Kikuyu pia kwa Ufasaha, hili kwangu mimi ilikuwa ni Culture shock! Sasa hawa watu wanaongea Lugha Gani kwa ufasaha kabisa na kwa umahili?
Ulifanya huu utafiti wako kwa muda wa mwezi mmoja tuu????:biggrin:
Tena,,ni vipi ulivyo wahi kujua kwamba hata 'vilugha' vyao kama kijaluo
na Kikuyu hawafahamu sababu nilazima uwe unafahamu hivyo vilugha
ndivyo uweze kuwatoa makosa??????
Hiki si nikichekesho cha mwaka.
Kuja Kenya,,,kaa kwa miaka kama miwili,,kwa uchache,,tena uwe na watu
zaidi ya ishirini watakao kusaidia kwa hiyo kazi ya lugha na wazunguke
Kenya mzima ndivyo uweze kusema ambayo umeyaleta katika hii
thread.
Nenda mahali kama Marekani ama Uingereza ambapo utadhani kwamba kila mtuu
anaweza kukitumia kiingereza kwa ufasaha,,,bro, sis,,utapata " culture shock"
hiyo yako.:biggrin::biggrin:
Tebea bro,,,,utaona mengi na sihivyo unavyo fikiri.
Tena,,,lugha maana yake ni nini.
Ni kumwezesha mwanadamu kumfahamu mwenzake.
Sasa,,kama ungelisema eti wakenya hawafahamiani na sababu ni
lugha,,,yaani maghari barabarani yanangongana kila saa,,,,ukiitisha
soda dukani wanakuletea maziwa,,,ukienda benki kutoa pesa ule
mfanyi kazi wa benki anakudunga sindano,,,ukipeleka ngari lako garage
wabadilishe oil wana paka rangi,,,,
Hapo ningelisema Kenya tunashida ya lugha.
Lakini,,,upende usipende,,,ukweli ni kwamba Kenya ndicho kituo cha
East Africa.
Hivi juzi,,,TZ ilifukuza walimu maelfu kutoka Kenya.
Sitaki kuongeza zaidi lakini,,,Kizuri cha jiuza na kibaya cha jitembeza.
Mwisho,,,,Tembea na utajua kwamba si kwenu tuu ambapo chakula cha
pikwa vizuri.
Nimejaribu ku upindua kidogo huo msemo wa kiswahili,,, kwa sababu fulani.
Mimi mwenyewe,,na zungumza Kikuyu safi,,,Kiswahili sina shida saana,,,
Kiingera naongea vizuri kuliko wataliano wengi,,niliwahi kufunza wa faransa
hicho kiingereza ambacho ni cha madugu zao kutoka wiingereza,,,this this,,
'that is spade',,this,,,'that is soil'..this,,,, 'that is water'.
Kiarabu,,nilikisoma kwa uchache katika madrassa huko Lamu.
Wenye kiswahili safi katika hii Kenya kama coastal area ndio,,
kimaendeleo,,, wako nyuma ya wale hata kukitamka kiswahili
chenyewe ni shida.
Sasa,,maana ngani kuongea lugha safi mbali unaenda kulala
na,,,njaa.
Tafakari hayo ndugu.