Nilikuwa Kenya, Culture Shock!

Nilikuwa Kenya, Culture Shock!

kuwa na lugha inayotambulika kimataifa ni hatua kubwa sana kimaendeleo, kama ulikua hujui au umeamua kujifanya hujui ujupe matumaini ya muda mfupi, huoni hao waingereza wnavyojivuni lugha yao kutumika dunia nzima, lugha huenda na tmaduni hivyo kusambaa kwa lugha pia ni kusambaa kwa tamaduni za jamii husika

hao wanaoona lugha haina faida kwa taifa wanajifariji tu.
nawashauri wachunguze ni namna gani nchi ya uingereza inapata faida kwa kupitia miradi mbalimbali ya uchapaji vitabu chini ya shirika lake la oxford press.
vitu vingine watu wanabisha tu ili kujirizisha.
 
hata hivyo ktk wakenya wanaondika kiswahili kizuri jf wewe unajitahidi.kwa hili acha nikusifie mkuu.bila shaka uliishi vizuri na wabongo ulipo kuwa tz.kuna wale jamaa zenu wanaishi tz wakiwa wana behave as if they're so special than their host plus na kale katabia ka u-selfishness wa kikenya.wanaondoka tz wakiwa hawaja acha hata marafiki bali maadui.
Ninacho elewa ni kuwa unapowakuta watu na jinsi yao ya maisha, lazima uwaheshimu na kutengamana nao jinsi walivyo. Huwalishi na hujawasomesha. Hivyo mwenye mada hii kuja kwetu hapa Nairobi na baada ya mwezi mmoja tu anatukejeli kwa misingi ya lugha, hiyo ni dharau, hivyo ndivyo tulivyo, tunaongea lugha nyingi na kujivunia tamaduni zetu. Akirudi Bongo na kuendelea na maisha yake huko, asubiri tukija basi atakua na fursa ya kutukejeli.
 
Ile siku nitaona mwanafunzi anaanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa kutumuia Kiswahili bila kuchakachua na kingereza, basi hiyo ndio siku nitakomaa nacho. Lakini hadi sasa na katika enzi hizi za kisasa bado hakijaboreshwa.
Kipindi fulani tukiwa kwenye kongomano la wahandisi wa softwares tokea hapa EAC wakiwemo Wabongo, tulikubaliana kujadili maswala ya ufundi kwa kutumia Kiswahili, lakini la kushangaza hata Wahandisi Wabongo wenyewe walijikuta hawakamilishi chochote bila Kingereza.
Unawakuta Wachina, Wajapani, Warusi nk wao wanasomea hadi fani zao bila kujua neno moja la Kingereza, maana lugha zao zimeboreshwa. Kiswahili chetu hiki bado tena sana.
 
Kwa hiyo unataka kusemaje sasa? Na isitoshe wewe Ni muongo hakuna Lugha Duniani iliyojikamilisha hivyo! Hata Kiingereza Chenyewe zaidi ya asilimia 60% ya maneno yake ni ya kuazima kutoka Kilatini, Kigiriki, Kifaransa, Kijerumani n.k.

Kijapani hivyo hivyo Wanatumia maneno mengi sana ya kuazima na hasa ya Kijerumani kwenye maswala ya Sayansi kama Medicine na pia kwenye Sheria kwa maana Wajapani wanatumia Sheria za Kijerumani.
Wachina na Wakorea hivyo hivyo hakuna Mwanasayansi wa Kichina ambaye atajifundisha Fizikia au Kemia kuanzia Cheke chea mpaka Chuo Kikuu kwa Kichina kitupu yaani bila kutumia maneno ya kuazima ya kimagharibi kama Atom, Quantum, Protein n.k ktk Kiingereza kuna kitu kinaitwa loan words au maneno ya kuazima na Lugha zote Duniani ziko hivyo Kichina kina maneno mengi ya Kipersia na Kipersia kina maneno mengi ya kiarabu vile vile Kihindu...Ni kama wewe huwezi kuongea Kikikuyu kwa masaa mawili mfululizo bila kuweka neno la Kiswahili aua lenye asili ya Kiswahili, fikiria kidogo na utaliona hilo...

Hivyo kusema kwamba Kiswahili hakijitoshelezi ni UJINGA Uliokithiri na hauna tofauti na Wazungu waliokuwa wanasema Waafrika hatuko tayari kujitawala na hivyo tunawahitaji na sisi tukawaamini!
 
Kaka kuna lugha ya vijana hapo Nairoo huwezi kujua ni lugha gani,hiyo sheng yao wanijua wao pia wanaongea kifupi na kinyume cha neno kwa kuchanganya kiswahili,kiingereza na lugha za asili zao,kwa mfano Sato,ni kifupi cha Saturday,na wanongea haraka kiasi kwamba kujua wanaongea nini inakuwa shughuli,pia kama ilivyo huku TZ watu wa matatu wana lugha yao sawa na huku kwa watu wa daladala/wapigadebe
 
Kwa hiyo unataka kusemaje sasa? Na isitoshe wewe Ni muongo hakuna Lugha Duniani iliyojikamilisha hivyo! Hata Kiingereza Chenyewe zaidi ya asilimia 60% ya maneno yake ni ya kuazima kutoka Kilatini, Kigiriki, Kifaransa, Kijerumani n.k.

Kijapani hivyo hivyo Wanatumia maneno mengi sana ya kuazima na hasa ya Kijerumani kwenye maswala ya Sayansi kama Medicine na pia kwenye Sheria kwa maana Wajapani wanatumia Sheria za Kijerumani.
Wachina na Wakorea hivyo hivyo hakuna Mwanasayansi wa Kichina ambaye atajifundisha Fizikia au Kemia kuanzia Cheke chea mpaka Chuo Kikuu kwa Kichina kitupu yaani bila kutumia maneno ya kuazima ya kimagharibi kama Atom, Quantum, Protein n.k ktk Kiingereza kuna kitu kinaitwa loan words au maneno ya kuazima na Lugha zote Duniani ziko hivyo Kichina kina maneno mengi ya Kipersia na Kipersia kina maneno mengi ya kiarabu vile vile Kihindu...Ni kama wewe huwezi kuongea Kikikuyu kwa masaa mawili mfululizo bila kuweka neno la Kiswahili aua lenye asili ya Kiswahili, fikiria kidogo na utaliona hilo...

Hivyo kusema kwamba Kiswahili hakijitoshelezi ni UJINGA Uliokithiri na hauna tofauti na Wazungu waliokuwa wanasema Waafrika hatuko tayari kujitawala na hivyo tunawahitaji na sisi tukawaamini!

Ninachosema ni kuwa kuna tume zimebuniwa za kuboresha kiswahili lakini bado kazi. kama lazima tuazime maneno basi tunafaa ku-swahilinise the borrowed words kama walivyofanya Wazungu na kote kwingine. kwa mfano jinsi naona umetumia neno "Sayansi". ila kwa sasa hivi bado shughuli tena kubwa sana.
 
Nikiwa kama Mtz nilipata bahati kufika Nairobi na nilikuwa huko kwa muda wa Mwezi mmoja! Kitu kikubwa kilichonishangaza ni kwamba Kenya au nisema Nairobi kuna Watu wengi sana hakuna Lugha wanayoijua kwa kwa ufasaha, yaani kuna Watu hawawezi kuongea Kiswahili chote kwa ufasaha, pia hawawezi kuongea kiingereza chote kwa ufasaha na cha ajabu kabisa pia hawawezi kuongea vilugha vya kikwao kama kijaluo au sijui Kikuyu pia kwa Ufasaha, hili kwangu mimi ilikuwa ni Culture shock! Sasa hawa watu wanaongea Lugha Gani kwa ufasaha kabisa na kwa umahili?

Itakuwa hivyo hadi ijitokeze lugha mya ya watu wote na ukabila uishe. Kwani kuna ubaya? Wanao ongea lugha sanifu wana advantage gani wapi?
 
Ukinisoma vizuri utaona kwamba hakuna mahali nimeandika kwamba kuna Ubaya wowote bali, nilishangaa tu. Kwangu mimi sijawahi kuona au kukutana na hali kama hiyo yaani Mtu ambaye hana Lugha yoyote anayoweza kuiongea kwa ukamilifu bila ya kuchanganya na Lugha nyingine...Ni hivyo tu na ndio maana nikasema ilikuwa ni Culture shock kwangu!
 
kama muliweza kuelewana inatosha sana hayo mengine hayakuhusu.

Labda kama hauelewi nilichomaanisha, ni kwamba sijawahi kukutana na hali kama hiyo lkn sija Mhukumu Mtu na wala sijasema kwamba ni kitu kibaya, bali nilishangazwa tu, ni rahisi kihivyo!
 
Mbali na lugha,jaribu kuwauliza wanajivunia muziki wao wenye mahadhi gani,sisi tuna bongo flava na muziki wa mwambao,South Afrika wana Kwaito,Kongo wana bolingo,Kenya je?
 
small thinking america, russia england zambia egypt spain.wana nini.vile uelewa nchi ambazo industry imekomaa style zote za mziki unawili kama ilivyo kenya sio sauti moja kama choir.
 
Ile siku nitaona mwanafunzi anaanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa kutumuia Kiswahili bila kuchakachua na kingereza, basi hiyo ndio siku nitakomaa nacho. Lakini hadi sasa na katika enzi hizi za kisasa bado hakijaboreshwa.
Kipindi fulani tukiwa kwenye kongomano la wahandisi wa softwares tokea hapa EAC wakiwemo Wabongo, tulikubaliana kujadili maswala ya ufundi kwa kutumia Kiswahili, lakini la kushangaza hata Wahandisi Wabongo wenyewe walijikuta hawakamilishi chochote bila Kingereza.
Unawakuta Wachina, Wajapani, Warusi nk wao wanasomea hadi fani zao bila kujua neno moja la Kingereza, maana lugha zao zimeboreshwa. Kiswahili chetu hiki bado tena sana.

Lawmaina78, kwanza hongera sana kwa kiswahili hiki fasaha,maashallah..ni hivi kiswahili kinakuwa sana kila siku na utohoaji wa maneno mbalimbali unaongezeka sana kama tu lugha zingine hata kiingereza,Pia teknolojia inapokuwa pia kiswahili kinazalisha misamiati mbalimbali mfano ilivyokuwa kwa jokofu,kikokotozi,kinakilishi n.k na leo hata mtandao wa kijamii wa Facebook upo pia ktk lugha yetu adhimu NA ni lazima kama wazawa tujivunie lugha yetu,na karibu nchi zote zinajivunia lugha yao hata kama si ya kimataifa,tatizo kuna hawa wakenya wenzio baadhi huwa wakija Tz wanakuwa na dharau sana kwa wabongo na hiyo sheng yao wakati hata ustaarabu hawana mahasidi hawa,wanaona kama tuko in a primitive mode...
 
small thinking america, russia england zambia egypt spain.wana nini.vile uelewa nchi ambazo industry imekomaa style zote za mziki unawili kama ilivyo kenya sio sauti moja kama choir.

Tofautisha ustawi wa viwanda na miundombinu dhidi ya miziki wa asili,inapendeza sana na ni ufahari kijisifia chako hata kama unashiriki na vya wengine!!! Na hata spain,Egypt,n.k wana miziki yao ya asili,wamerica weusi wa kule wanajivunia hiphop...
 
Back
Top Bottom