kuwa na lugha inayotambulika kimataifa ni hatua kubwa sana kimaendeleo, kama ulikua hujui au umeamua kujifanya hujui ujupe matumaini ya muda mfupi, huoni hao waingereza wnavyojivuni lugha yao kutumika dunia nzima, lugha huenda na tmaduni hivyo kusambaa kwa lugha pia ni kusambaa kwa tamaduni za jamii husika
Ninacho elewa ni kuwa unapowakuta watu na jinsi yao ya maisha, lazima uwaheshimu na kutengamana nao jinsi walivyo. Huwalishi na hujawasomesha. Hivyo mwenye mada hii kuja kwetu hapa Nairobi na baada ya mwezi mmoja tu anatukejeli kwa misingi ya lugha, hiyo ni dharau, hivyo ndivyo tulivyo, tunaongea lugha nyingi na kujivunia tamaduni zetu. Akirudi Bongo na kuendelea na maisha yake huko, asubiri tukija basi atakua na fursa ya kutukejeli.hata hivyo ktk wakenya wanaondika kiswahili kizuri jf wewe unajitahidi.kwa hili acha nikusifie mkuu.bila shaka uliishi vizuri na wabongo ulipo kuwa tz.kuna wale jamaa zenu wanaishi tz wakiwa wana behave as if they're so special than their host plus na kale katabia ka u-selfishness wa kikenya.wanaondoka tz wakiwa hawaja acha hata marafiki bali maadui.
Wanaongea ki-tribalism
Sent from Nokla using Jf app
Ile siku nitaona mwanafunzi anaanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa kutumuia Kiswahili bila kuchakachua na kingereza, basi hiyo ndio siku nitakomaa nacho. Lakini hadi sasa na katika enzi hizi za kisasa bado hakijaboreshwa.
Kipindi fulani tukiwa kwenye kongomano la wahandisi wa softwares tokea hapa EAC wakiwemo Wabongo, tulikubaliana kujadili maswala ya ufundi kwa kutumia Kiswahili, lakini la kushangaza hata Wahandisi Wabongo wenyewe walijikuta hawakamilishi chochote bila Kingereza.
Unawakuta Wachina, Wajapani, Warusi nk wao wanasomea hadi fani zao bila kujua neno moja la Kingereza, maana lugha zao zimeboreshwa. Kiswahili chetu hiki bado tena sana.
Kwa hiyo unataka kusemaje sasa? Na isitoshe wewe Ni muongo hakuna Lugha Duniani iliyojikamilisha hivyo! Hata Kiingereza Chenyewe zaidi ya asilimia 60% ya maneno yake ni ya kuazima kutoka Kilatini, Kigiriki, Kifaransa, Kijerumani n.k.
Kijapani hivyo hivyo Wanatumia maneno mengi sana ya kuazima na hasa ya Kijerumani kwenye maswala ya Sayansi kama Medicine na pia kwenye Sheria kwa maana Wajapani wanatumia Sheria za Kijerumani.
Wachina na Wakorea hivyo hivyo hakuna Mwanasayansi wa Kichina ambaye atajifundisha Fizikia au Kemia kuanzia Cheke chea mpaka Chuo Kikuu kwa Kichina kitupu yaani bila kutumia maneno ya kuazima ya kimagharibi kama Atom, Quantum, Protein n.k ktk Kiingereza kuna kitu kinaitwa loan words au maneno ya kuazima na Lugha zote Duniani ziko hivyo Kichina kina maneno mengi ya Kipersia na Kipersia kina maneno mengi ya kiarabu vile vile Kihindu...Ni kama wewe huwezi kuongea Kikikuyu kwa masaa mawili mfululizo bila kuweka neno la Kiswahili aua lenye asili ya Kiswahili, fikiria kidogo na utaliona hilo...
Hivyo kusema kwamba Kiswahili hakijitoshelezi ni UJINGA Uliokithiri na hauna tofauti na Wazungu waliokuwa wanasema Waafrika hatuko tayari kujitawala na hivyo tunawahitaji na sisi tukawaamini!
Nikiwa kama Mtz nilipata bahati kufika Nairobi na nilikuwa huko kwa muda wa Mwezi mmoja! Kitu kikubwa kilichonishangaza ni kwamba Kenya au nisema Nairobi kuna Watu wengi sana hakuna Lugha wanayoijua kwa kwa ufasaha, yaani kuna Watu hawawezi kuongea Kiswahili chote kwa ufasaha, pia hawawezi kuongea kiingereza chote kwa ufasaha na cha ajabu kabisa pia hawawezi kuongea vilugha vya kikwao kama kijaluo au sijui Kikuyu pia kwa Ufasaha, hili kwangu mimi ilikuwa ni Culture shock! Sasa hawa watu wanaongea Lugha Gani kwa ufasaha kabisa na kwa umahili?
Itakuwa hivyo hadi ijitokeze lugha mya ya watu wote na ukabila uishe. Kwani kuna ubaya? Wanao ongea lugha sanifu wana advantage gani wapi?
kama muliweza kuelewana inatosha sana hayo mengine hayakuhusu.
Mbali na lugha,jaribu kuwauliza wanajivunia muziki wao wenye mahadhi gani,sisi tuna bongo flava na muziki wa mwambao,South Afrika wana Kwaito,Kongo wana bolingo,Kenya je?
Ile siku nitaona mwanafunzi anaanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa kutumuia Kiswahili bila kuchakachua na kingereza, basi hiyo ndio siku nitakomaa nacho. Lakini hadi sasa na katika enzi hizi za kisasa bado hakijaboreshwa.
Kipindi fulani tukiwa kwenye kongomano la wahandisi wa softwares tokea hapa EAC wakiwemo Wabongo, tulikubaliana kujadili maswala ya ufundi kwa kutumia Kiswahili, lakini la kushangaza hata Wahandisi Wabongo wenyewe walijikuta hawakamilishi chochote bila Kingereza.
Unawakuta Wachina, Wajapani, Warusi nk wao wanasomea hadi fani zao bila kujua neno moja la Kingereza, maana lugha zao zimeboreshwa. Kiswahili chetu hiki bado tena sana.
small thinking america, russia england zambia egypt spain.wana nini.vile uelewa nchi ambazo industry imekomaa style zote za mziki unawili kama ilivyo kenya sio sauti moja kama choir.