Elections 2010 Nilikuwa mkereketwa wa CHADEMA lakini nimejitoa

Mnafki mkubwa! siasa za ccm ni unafki mtupu, eti Ngoda naye alikuwa CHADEMA, vp ulinyimwa viti maalum? Pole!
 
Kwako Zawadi
Nataka nikununulie zawadi ya lipstick, ili lips zako zipendeze.

Huwezi jua, soko lako likaongezeka mara dufu.
 
Uwe mkweli. Ulitumwa na mafisadi kutoka chama chao wanachokipenda ili uingine Chadema na kuvuruga. Inaonekana mbinu hiyo ilishindikana ndiyo maana ukaondoka.

Pipooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooz .............

Mwaka huu, mtasema mengi.
 
Mimi nakuunga mkono kujitoa chadema kwani inaonekana hata tanzania umejitoa kwani hujui umaarufu wa dr. Slaa.
Samahani mara ya mwisho kuwa tanzania ilikuwa lini?
 
Huyu anayejiita Zawadi gift what ever kwenda zako usitutishe hapa kwani ulipojiunga na chama ulituambia iweje leo uje kututangazia????? Nendeni bana kwani nani anawataka hapa.. Uongo wako umeonekana hahaha eti nimeamua kukihama chama cha CHADEMA yaani mnakuwa waongo mpaka siku mnarudi kwake yeye aliyewaleta. Tuondolee pumba zako hapa
 
cham hiyari yako kaka au dada! kajiunge na akina lowasa na rostamu la aziz kule kuna mgawo wa vitenge na kofia. huku tunagawa nafsi zetu kwa ajili ya Taifa letu

ROHO ZETU TUMEZIWEKA REHANI KWA AJILI YA TAIFA LETU KUPITIA KWAKO EWE DR SLAA, USIOGOPE TUPO NAWE
 

Pole sana mkuu, Unfortunately, you have not communicated. There is no message
 
Nilikuwa mkereketwa wa CHADEMA



Wakereketwa wako Chama Cha Mafisadi, Kwanza mnakereketwa nini?

Katika CHADEMA hatuna wakereketwa bali wafuasi.
 
Post yako iko vague sana, unaona vipi utueleze kiundani zaidi?

1. Ataigawa nchi vibaya sana.
Ataigawa vipi nchi? Maelezo zaidi tafadhali.

2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1)
Naomba utueleezee zaidi tafadhali.

3. Si maarufu Dar wala Dodoma. sijui atakaa ikulu ya wapi.
Kwani hapa wananchi wanachagua umaarufu ama uwezo wa kuongoza? Mwaka 1995 BWM hakuwa maarufu na bado alichaguliwa. Kweli watanzania tumeishiwa kiasi hiki mpaka tunachagua watu kwa vigezo vya umaarufu na sio utendaji wao wa kazi?

4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu)
Mavadhi au mavazi?

5. Hana sera yeyote ile ya uchumi.
Slaa kama Slaa hana sera ya uchumi kwa sababu hagombei kama mgombea binafsi bali kwa kutumia ticket ya CHADEMA kwa hiyo nadhani mjadala unatakiwa uwe kuhusu sera ya uchumi ya chama chake.

Hayo ni machache tu lakini udhaifu wake ni mwingi mno.
Haya machache uliyoyaweka hayana mshiko tuongezee hayo mengine.
 
Zawadi ngonda pole kwa nadharia zako. Katika mambo uliyotaja ya kujitoa chadema ujaongea neno la maana ila tu umepangilia maneno vizuri kutoka katika kamusi ya kiswahili. Ni aibu kwa mtu mzima kusema maneno kama ayo. Ni bora ungezua tuhuma dhidi ya Mh. Dr wa kweli alaf ukafanya sababu ya kujitoa kuliko kuandika tu unachojisikia. Wenye akili timamu watashangaa mambo yako. Haukuwa mkereketwa kwani mkereketwa ina maana yake sio ili mradi kujiita mkereketwa tu. Zawadi wapo wengi kama wewe wasioweza siasa wamekaa kimya,sio lazima uwe ktk siasa waweza jaribu kitu kingne. Zawadi ukijitoa kabidhi kadi ili baada ya uchaguzi tujue Chadema imepoteza Mamluki wangapi. Ila usiseme umetimiza haki yako ya kisiasa au kidemokrasia,hamna haki yoyote inayosema kuwa ni haki ya 'kujitoa'. Huo ni uamuzi Zawadi wala sio demokrasia. Ushauri ntakupa bure,kumbuka Tanzania tuna maadui wanne: ujinga,maradhi,...na ufisadi. Jaribu kumfukuza adui aliyekujia Zawadi!
 
huyu Zawadi ngoda anahitaji medical attention ....as a medic nipo tayari kumtibu bure
 
Kwanza nakupongeza sana, na kwa ukweli una alama 10/10 kwa upande wangu.

Sioni aibu kusema kwa siku mbili toka hii thread iwe hewani, hakuna aliyejibu hoja zangu. Mtu mwingine aliyekaribia kujibu hoja ni 'babadesi' kuhusu mavazi ambae yeye nilimpa alama 2/10. Waliobaki wengi wamenitisha na kuishia kutukana tu. Matu.si si asili yangu na hata kama utaniona nimetoka nje ni kuhusu kutofautiana kimtazamo tu na wala si ma.tusi

1. Nakubaliana nawe ila mgawanyo unaouzungumzia nimatokeo ya kukubali ubepari ambapo watanzania wote tumakubali reform hiyo. lakini Mh Slaa akiingia madarakani mgawanyo utazidi mara mbili kwa sababu hatapata support bungeni na atalazimisha kukaa na wabunge 30% kwa nguvu. Ktk nchi zilizooendele mambo yakienda kombo wanajiuzulu mfano(Baruso- Italy)- sasa huyu atafanya nini.

2. Na 30% hawezi kuleta demokrasia hilo sina haja hata ya kulijadili.

3. Umetoa mfano wa Mkapa, lakini unajua Mkapa aliua wangapi Dar. Wengine hata alikuwa hasalimiani nao kwa kushikana mikono, ukweli Makamba na Mahita ndio walikuwa wasemaji wakuu wa Mkapa Dar. Unaweza ukafikiri hilo Dogo, lakini hata Mwl alitumia mbinu nzuri sana ya kuishika Dar (ni mjadala mrefu huu staingia kiundani). UD walipoandamana wakati wa Mwinyi aliwaita wazee wa Dar na kuwa hutubia, halikadhalika Kikwete mambo yalipomuendea kombo na wafanyakazi. Gadafi alihamisha makao makuu kwenda Tripoli baada ya kuchukiwa kule makao makuu-fuatilia.

4. BabaDesi kashamaliza, mimi sina la kusema. Hivi unahisia gani ukiyaona mavazi ya fuatayo: Mgambo, JKT, Polisi, JWTZ. Tunaweza kuiwa katika hisia tofauti, lakini mimi huwa najua kuna jambo limetokea. Wahuni huwaita wazee wa kazi.

5. Nakubaliana nawe, lakini hapa kazi ipo. Kusema bungeni ni kitu kingine lakini kuwa katika utendaji ni jambo jingine kabisa. Hii ni jinsi mimi ninavyomuona huyu Mheshimiwa, na ndio maana nimesema mara nyingi kuwa bado ninamkosa kama mbunge. Hapa tunaweza tukatofautiana lakini si kitu na ndio maana ya kura.

Any way nimejibu kifupi sana ili nisiwachoshe wasomaji.
 

Wee interview ilikwendaje ile kazi ya housegirl kwa Mwaarabu wa JF?
 
nafkiri amesema alikuwa mkereketwa wa chadema na wala si mwanachama wa chadema.. sasa mnamuuliza uwanachama wake atoe ushahidi si wa waelewi.. kwani hata hao watu wachache watakaopigia kura chadema October 31st sio wote ni wanachama wenye kadi za chadema.

CHAGUWA KIKWETE CHAGUWA CCM ..
 
 

Useless..
Mi ni mtz na sijakubali hiyo reform..

Mushrikin..umekuwa sheikh Yahya?? lolz..hizo 30 % umezitoa wapi, na ataigawa nchi mara 2 umeitoa wapi? whats is ur supporting argument?

BTW, Baruso ndio kinyangarika gani..? bwe he he he..
2. Na 30% hawezi kuleta demokrasia hilo sina haja hata ya kulijadili.
Ni kweli huezi kujadili assumption kwa sababu ina-exists kwenye kichwa chako tu, it is not a real data.

Pointless..makazi ya rais hayana mafungamano yeyote na popularity ktk eneo la Ikulu, unless kama kiongozi mhusika aliingia Ikulu kwa mtutu au ujambazi wa kura. Kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia hana shaka kwenda popote,kuishi popote au kukutana na yeyote..and by the way huna empirical data kuthibisha kwamba ktk wagombea wetu ni yupi yupo popular wapi so far, unless utuambie wewe ni mfuga majini.
4. BabaDesi kashamaliza, mimi sina la kusema. Hivi unahisia gani ukiyaona mavazi ya fuatayo: Mgambo, JKT, Polisi, JWTZ. Tunaweza kuiwa katika hisia tofauti, lakini mimi huwa najua kuna jambo limetokea. Wahuni huwaita wazee wa kazi.
Pumba.

Kumbukumbu (verifiable) zinaonesha Chadema wameanza kuvaa hayo mavazi kitambo sana na si kutokana na msukumo wa Slaa kugombea urais. Kuifungamanisha hoja hii na Slaa kugombea urais dhahiri ni ukichaa. Btw, hata kama Chadema wangevaa kombati za kikomandoo, labda tuchungulie ni nani so far ameshamwaga damu?? wanajf watajibu kwa niaba yako.
Thibitisha hoja yako ya awali kwamba Slaa hana sera ya Uchumi, usipaparike kama kuku kishingo alopigwa jiwe la utosini.
Any way nimejibu kifupi sana ili nisiwachoshe wasomaji.
..si lolote si chochote
 

Heshima kwako admissionletter,

Good analysis.JF inahitaji watu kama wewe wenye uwezo wa kutoa majibu yanayoendana na hali hasi ya Tanzania.
 
Utakuwa Umenyimwa Viti Maalumu Umeanza Kuropoka sasa teh teh teh
Kuna Wakati Kukaa Kimya Ni Busara Kuliko Kuropoka ropoka
Hujaeleza Sababu Za Msingi Hapo Juu Umeweka Umbea Tu
:dance:
 
Tanzania hatutaki kuongozwa na Rais maarufu, tunataka kuongozwa na RAIS BORA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…