Ni sawa na kuweka akiba BENKI-Ni maneno sahihi kabisa, lakini lazima ujue ni BENKI ipi unaweka, DECI au NBC, NMB au CRDB.
Unaweza kupata kigugumizi utapoambiwa uchague kati ya NBC, NMB au CRDB. Lakini kamwe hutashikwa na kigugumizi ikiwa uchaguzi ni kati ya DECI na Benki hizo nyingine.
Sina aibu kusema kuwa kumpa kura yako Mh Slaa ni sawa na kuweka pesa yako DECI.
Kumchaguia Kikwete ni sawa na kuweka pesa yako NBC, NMB au CRDB.
Uchaguzi ni wako.
Mimi si FISADI wala Mtoto wa FISADI, bali ninachojua ni kuwa kukuwa kwa uchumi nchi zote za Afrika ni kati ya 5-8%. Sisi uchumi wetu mwaka jana pamoja na mtikisiko wa uchumi ulikuwa kwa 6.5%, hivyo mambo si mabaya. Sasa kwanini tusimchague Kikwete.
Jamani tuwe na shukurani wakati mwingine, tutapata laana!