Nilikuwa nauchukulia poa urefu wangu kuona ni kawaida kumbe kuna priveledge kadhaa nazipata bila kujua

Nilikuwa nauchukulia poa urefu wangu kuona ni kawaida kumbe kuna priveledge kadhaa nazipata bila kujua

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Urefu wangu, mita 1.8x

Haya mambo nilikuwa nayachukulia poa sana nilidhani ni kawaida kwa kila mtu ila nimekuja kuyajua baadae sana

- Wale vibaka wa kumendea kuiba simu sijawai kusogelewa nao, nilikuwa nikisikia hizi story nadhani labda napita njia tofauti

- Watu hawapendi kuanzisha ugomvi na mimi, nilikuwa naona watu ni wapenda amani ila nikaja kustuka kwanini hata wakorofi wanapenda amani ?

- Sijui nieleze vipi lakini nikienda sehemu flani huwa ni kama kuna kaheshima hivi, watu hupenda kunisalimu lakini sina uhakika labda ni vile huwa napenda kuwa nadhifu.
 
Urefu ambao unaweza kusababisha uheshimike ni kati ya 150-165cm ukizidi hapo huheshimiki unashang'awa
Huo utakuwa labda urefu wako ndio unakufanya unajiona na wewe ni mrefu, hicho ni kimo cha kawaida sana.

hata polisi kwenyewe wanawake inabidi wawe angalau na urefu wa sentimita 165, kwa wanaume ni centimetre 178 (futi tano na inchi nane)
 
Umetokea wapi mkuu, huko uliko yaelekea watu wengi ni wafupi sana, sidhani kama kuna anaeweza kuwa polisi.

Polisi urefu kimo cha chini ni centimetre 178 (futi tano na inchi nane)
Sasa unaanza kuleta pumba! IGP camilus wambura yupo kwenye 150cm,Afande naibu kamshina david mishime yupo kwenye 152 huo ni mfano tu wa polisi wazito! sasa hiyo 178cm umetoa wap??
 
Sasa unaanza kuleta pumba! IGP camilus wambura yupo kwenye 150cm,Afande naibu kamshina david mishime yupo kwenye 152 huo ni mfano tu wa polisi wazito! sasa hiyo 178cm umetoa wap??
Mkuu unajua kwamba 150 cm haifikii hata futi 5 ?
 
Sasa unaanza kuleta pumba! IGP camilus wambura yupo kwenye 150cm,Afande naibu kamshina david mishime yupo kwenye 152 huo ni mfano tu wa polisi wazito! sasa hiyo 178cm umetoa wap??
Misime unamjua vizuri?, Wambura simjui vizuri ila Kwa Misime hapungui 180cm
 
Back
Top Bottom