Mimi mbona nikiangalia naona hamna shida ubaya uko wapi ? labda ile nyeupe.
Ukienda kwa wanzetu nzuri ni moja tu ile inayotaka kufanana na nyeusi.
Anyway mawazo yangu tu
Shida wana simba ni kusikiliza sana maneno ya watu, afu ukute hao wanaongea ni uto.
Timu toka imeanza msimu huu haikuwa vizuri, tukalalamika tatizo kocha, hata kabla ya mechi ya Simba na Yanga tulikuwa tukilalamika na baadhi ya uto wakasema shida ni kocha.
Katolewa tunasema viongozi wamekurupuka, yani hatueleweki nini tunataka.
Hii inatokana kusikiliza maneno ya watu ambao uto ndio uongea sana.
Kwenye jersey ni hivyo hivyo, mnawasikiliza Yanga sana.
Leo tunajifanya kumkumbuka Barbara, eti yeye alikuwa mzuri, wakati mashabiki ndio tulikuwa tunasema atoke mpaka ameachia ngazi.
Afu leo tunajifanya kumkumbuka, yani hatuelewi nini tunataka, yani kila kitu kulalamika.