mediaman
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 451
- 688
Wakuu, hii ni habari ya kweli kabisa. Hivi majuzi niienda mji fulani nikakutana na kisa cha ajabu sana. Baada ya kufika katika mji huo mwenyeji wangu alinipokea na kunikaribisha kwake. Baada ya kufika kwake nikatambua kuwa anaishi katika vyumba viwili katika nyumba ya kupanga.
Tulipokuwa tunaongea sebuleni huyo ndugu(mwenyeji wangu) aliniambia kwamba hiyo nyumba wapangaji huwa hawakai muda mrefu, wanahama wenyewe ili kukwepa vitendo vya kichawi wanavyokutana navyo baada ya kuanza kuishi katika nyumba hiyo. Ila yeye akaniambia ameweza kuishi hapo kwa muda mrefu kutokana na kuzingatia sana sala na maombi. Sikumwelewa vizuri hadi ilipofika saa ya kulala kama saa sita hivi usiku. Tuliagana muda huo, yeye akaenda kulala chumba chake na mimi nikabaki sebuleni kwenye kitanda alichokuwa ameniandalia hapo.
Kabla sijalala nikasema moyoni "huyu mwenyeji wangu si amesema kinachomsaidia kuishi hapo na kushinda uchawi ni maombi, ngoja basi na mimi kabla sijalala niombe Mungu anilinde."
Kabla ya kuanza kuomba nikajiambia, "Ah, ngoja nipumzike kwanza kidogo ntaomba baadaye." Nikajitupa kitandani. Baada ya dakika kama moja tu nikiwa kitandani nimejilaza chali, nikahisi ghafla kitu kizito sana kinanikandamiza kifuani. Nilihisi kama vile nakandamizwa na miguu ya tembo. Mgandamizo ulikuwa mzito sana, ila sikuona mtu wala mnyama! Nikaona hapo kuna hatari ya kifua changu kuwa kama chapati. Nikakumbuka yale maneno aliyonisimulia huyo mwenyeji wangu kuhusu wachawi, ndio nikatambua nimevamiwa na wachawi wanaotaka kuniua. Nikatoka haraka kitandani, nikasimama na kuanza kumwomba Mungu kwa bidii(ila kwa sauti ya chinichini nisimshitue mwenyeji wangu au wapangaji wengine kwenye nyumba ile). Niliomba sana Mungu anilinde, huku nikiwakemea wachawi watoke hapo kwa Jina la Yesu. Niliomba kwa zaidi ya saa moja, baada ya hapo ndio nikajilaza tena kitandani. Nililala shwari mpaka asubuhi, sikusikia tena mgandamizo wala nguvu zozote za kichawi.
Hakika, kama Maandiko matakatifu yasemavyo, tukimpinga Shetani kwa Jina la Yesu anakimbia(Yakobo 4:7) na pia maombi ni silaha ya kumshinda Shetani na mawakala wake(wachawi).
Katika Waefeso 6:11-18 tunaambiwa:
"Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote"
Hivyo, nakutia moyo ndugu, ukikutana na vitendo vyovyote vya kichawi/kishirikina, popote pale, usiogope wala usifanye haraka kuhama nyumba; muombe Mungu, anasikia, atakulinda na kukuokoa na hila za mashetani wanaopanga kukuangamiza.