Nilikuwa nimelala chali, "tembo" akanigandamiza sana kifuani

Mgandamizo ulifanyika kwa sekunde kama kumi. Nilipotambua kuwa huo mgandamizo ni wa kichawi na kwamba njia pekee ya kushinda ni kumuomba Mungu, mgandamizo ulitoweka ndio nikaweza kuamka na kusimama.
Sawasawa... Ukafanyiwe x-ray usijekuta umeumia kifua kwa ndani alafu hujui,,,
 
Hahahaha!! Moja ya side effects za kunywa double kick bila kula na mawazo.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Tena kwangu mimi bora kahaba anayeuza mwili maana kwanza atapata raha ya ngono pili atapata pesa za kusaidia mahitaji yake. Lakini mchawi usingizi hapati na akirudi kuwanga hana hata mia. Shwaiin
Hawa viumbe ni washenzi sana kuna mwaka tupo Dodoma nyumba ya jirani alishikwa mchawi akiwa hovyo sana
 
Niliwahi kukimbia nyumba, nikaacha na kodi, nilirudi baada ya miezi 3 kubeba vitu vyangu.....shwain kabisa yule maza hausi.
Duh, pole.
Ila kukimbia nyumba sio ufumbuzi wa kudumu, kwakuwa Shetani na wachawi wake wanaweza kukufuata popote utakapohamia. Hivyo ni bora kusimama tu kiume na kupambana nao kwa uweza wa Mungu.
 
Sorry mkuu kwani cku hyo mlikula chakula gani kabla ya kulala
 
Sawasawa... Ukafanyiwe x-ray usijekuta umeumia kifua kwa ndani alafu hujui,,,
Hahaa. Pesa itapotea bure kwenda kupima. Mambo ya kichawi huwa hayaonekani kwa X-ray wala Ultrasound.
 
Tena kwangu mimi bora kahaba anayeuza mwili maana kwanza atapata raha ya ngono pili atapata pesa za kusaidia mahitaji yake. Lakini mchawi usingizi hapati na akirudi kuwanga hana hata mia. Shwaiin
Wanarudi na baridi kama kisu kilicholala nje
 
Hahahaha!! Moja ya side effects za kunywa double kick bila kula na mawazo.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Namshukuru Mungu tangu tumboni mwa mama yangu hadi leo sijawahi kunywa divai(wine) wala kileo(fermented/strong drink). Hivyo hesabu ushuhuda huo kuwa ni halisi, sio double kick side effects.
 
Sijanasibisha kulala chali na uchawi lakini wataalam wa afya wanasema kulala chali si kuzuri, wengine hukoroma, wengine huhisi wamekabwa, aah wataalam wanajua zaidi.
Ni kweli wataalam wanajua zaidi ila hawajui yote. Hivyo wakati mwingine akili za kuambiwa na wataalam tuchanganye na zetu. Mtu anapopanda kitandani anaweza kuchagua alale kiubavu au kifudifudi. Lakini usingizi ukishamchukua, hawezi kuchagua tena alaleje. Mtu anapokuwa usingizini hajijui tena kama amelala chali au la. Na pia tunatofautiana. Kuna watu hawawezi kulala mwanzo mwisho bila kujigeuza geuza. Hata hivyo kama wachawi wameamua kukugandamiza, ukilala kiubavu si watakugandamiza hivyo hivyo tu? Jambo muhimu kama nilivyosema tukumbuke kuomba ulinzi wa Mungu kabla ya kulala. Mungu akiwa upande wetu hakuna awezaye kuwa juu yetu. Tutalala salama, tukiwa chali au la.
 
Usipende kulala chali hakuna cha uchawi wala shangazi yake ulozi
Kama unaamini Mungu yupo, amini pia kwamba shetani na wachawi wapo. Biblia inasimulia vizuri mambo waliyoyafanya wachawi wa Misri. Soma sura ya 7 ya kitabu cha Kutoka. Uchawi upo, hata hivyo hatuhitaji kuogopa. Jina la Yesu lina nguvu sana kuliko uchawi/ushirikina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…