Nililala na njaa kwa sababu ya mechi ya Simba na Yanga

Nililala na njaa kwa sababu ya mechi ya Simba na Yanga

Young Africans..Sahau Kambi..David Mwakalebela..Ken mkapa..Godwin Aswile..Salum Kabunda..Isa Athuman(Rip)..Nicodemus Ntekele(Rip)..Athumani China..Said Mwamba Kizota..Edibili Lunyamira..namba kumi nimemsahau mkuu..
Hivi china hakuwa tayari Simba? Na golini hakuwa Steven Nemesi kweli!
 
simba sports club..Mwamedi mwameja..Kasongo Athuman..Deo mkuki..Mustafa Hoza..George Masatu..Hussein Marsha..George Lukas..Gaga(Rip)..Edward Chumila..Dua Said.
Duu umenkumbusha akina Mustafa Hoza,kasongo,Mkuki n.k
 
Ha ha ha Constantine Kimanda alikuwa bonge la beki jamaa.
 
Mkuu miaka hiyo kulikua na vipaji haswa kuna mtu alikua anaitwa Michael Paul wa shinyanga kusajiliwa Simba Alinunuliwa mashine ya kusaga Nylon alikua anajua mpira huyu kifaa aisee huko tukuyu wana Stiven Musa..reli Moro Mbui Yondan..majimjaji Celestine Sikinde Mbunga(rip)..Nteze john Pamba Inocent Haule Zanzibar..daud kufa kunoga Lipuli..
Duuu kna Steve Musa! Haf mbona nakumbuka km hyo mechi Steve alicheza akiwa Yanga?
 
Nilikua sitoki kando ya redio. Hata kama betri zimekwisha, nitaokoteza zilizotupwa.Nazipondaponda na kuzipanda kwenye vipande vya mabua ya alizeti na kuunganisha waya wa + na - kwenye mkulima.
Ikifungwa timu yangu nakosa raha siku kadhaa.
[emoji1] duu betri za kupondaponda!
 
yaa miaka iyo nyumba nyingi betri za National zilikua zikianikwa katika nyumba na mpira tuanafatilia kweli Fat chini ya Ndolanga na Mwanakatwe katibu Aden Rage full sanaa sema mpira ulikuepo hela za viingilio wanaenda nazo nyumbani wanatangaza mapato baada ya wiki kupita..
Ha ha ha, baada ya wiki!
 
Alicheza yanga Mussa(Rip) baadae baada ya Athumani Abdalah China kwenda ulaya alicheza kiungo salvatory Edward namba sita
 
Mkuu Kichinjio upo sahihi hata mimi kwa sasa sijui kikosi chochote wakati tulikua tunajua vikosi vyote na magazeti hatusomi mpirani unaingia na hela huna duu ilikua hatari sana..
 
Mkuu izo Timu sijui Ghana..Ivory coast au Nigeria walikua wanafungwa nakumbuka kuna Timu moja kubwa ya Taifa ilifungwa goli moja lilifungwa na Innocent Haule mechi ilichezwa Zanzibar walikua wanajua mpira hao..
 
Ghana Taifa walifungwa mbili moja dk ya 80 naa mvua ikanyesha mechi ya kwenda kombe la Afrika mechi ikahaitishwa ichezwe kesho yake wachezaji hoi wakatutupia moja katika yupo marsha na Traole wao palichimbika aisee
 
Young Africans..Sahau Kambi..David Mwakalebela..Ken mkapa..Godwin Aswile..Salum Kabunda..Isa Athuman(Rip)..Nicodemus Ntekele(Rip)..Athumani China..Said Mwamba Kizota..Edibili Lunyamira..namba kumi nimemsahau mkuu..
Kwa kumbukumbu zangu kikosi kilikuwa hiki hapa: steven Nemes, Kened Mkapa, Willy Mtendamema, Chimanda Consitantine, Willy Martin, Method Mogella, Said Mwamba, Sakilojo Chambua, Sanifu Lazao, James Tungaraza na Edibily Lunyamila.
Hiki ndicho kilikuwa kikosi kamili japo sijakipangilia vyema. Hakika nakumbuka niliugua kabisa, kipindi hicho nilikuwa shule ya msingi nikiwa na miaka 14. Mdogo wangu na kaka yangu walikuwa washabiki wa Simba, yalikuwa maumivu kwelikweli.
 
Back
Top Bottom