Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wasalaam!
Waungwana naombeni ushauri wa zao linalostawi zaidi kwa mikoa ya Pwani/ Tanga na lenye faida kwa mkulima. Zao lipi linafaa zaidi kati ya nanasi/ machungwa/ maembe mapapai?
Natanguliza shukrani
Asante kwa ushauri wako! Kama hutajali waweza share na mimi kuhusu kilimo cha mbogamboga?Mkuu kwa kuchakata kwangu nanasi is the best maana ni rahisi kulima hayaitaji garama kubwa kuyalea pia kidogo yaweza kukaa kwa mda mrefu ukitafuta wateja ukilinganisha na machungwa au papai,
Yangu ni hayo ila sijawai kulima hayo madude mwisho wangu ni mbogamboga,
Hayo matunda utapata hasara tu kwani watanzania awali matunda mpaka waumwe. Lima tu mahindi na mpunga au mihogo.
Asanteni kwa ushauri wenu, nitaufanyia kaziKama unajikimu kimaisha kwa other sources of income, ni bora ulime machungwa au maembe kwa kuwa kupanda ni mara moja...
hekari ni kubwa kushinda ekari hivyo basi miche 1200 ni kwenye ekari sio hekari.Nakushauri lima Papai hasa hybrid
1.miezi 8 unaanza kuvuna mfululizo hadi miaka 3
2.haishambuliwi na wadudu hasa Miche niliyonayo
3.haina gharama za matunzo zaidi ya maji palizi na Mbolea
4.utawahi kurudisha gharama tofauti na mazao mengine.
5.mipapai mmoja matunda hadi 120
Heka moja mipapai 1200
Piga hesabu za roughly kila mwezi uvune matunda 700x500 =350,000 kwa mwaka ?
Uje nikuuzie Miche
Pia pita masokoni uulize Papai wananunua bei gani
0755404226 dsm kiluvya
Kama unajikimu kimaisha kwa other sources of income, ni bora ulime machungwa au maembe kwa kuwa kupanda ni mara moja...
Asante kwa ushauri, ngoja niachane nayo kwanzaMapapai hapana mpendwa wangu. Labda kama wewe ni risk taker.
Yanaweza kukupa pressure. Hasa ikitokea bahati mbaya inyeshe mvua ya mawe, uwiiiii.
Halafu pia yana ugonjwa fulani yanadonolewa yakishazaa.
Mengine unaweza kulima, kwanza yanasoko (Azam ni mnunuzi mzuri kama una mzigo mkubwa)