Nilime nini kati ya nanasi, machungwa, maembe na mapapai?

Nilime nini kati ya nanasi, machungwa, maembe na mapapai?

Mkuu kwa kuchakata kwangu nanasi is the best maana ni rahisi kulima hayaitaji garama kubwa kuyalea pia kidogo yaweza kukaa kwa mda mrefu ukitafuta wateja ukilinganisha na machungwa au papai,

Yangu ni hayo ila sijawai kulima hayo madude mwisho wangu ni mbogamboga,
 
Wasalaam!
Waungwana naombeni ushauri wa zao linalostawi zaidi kwa mikoa ya Pwani/ Tanga na lenye faida kwa mkulima. Zao lipi linafaa zaidi kati ya nanasi/ machungwa/ maembe mapapai?
Natanguliza shukrani

Hayo matunda utapata hasara tu kwani watanzania awali matunda mpaka waumwe. Lima tu mahindi na mpunga au mihogo.
 
Mkuu kwa kuchakata kwangu nanasi is the best maana ni rahisi kulima hayaitaji garama kubwa kuyalea pia kidogo yaweza kukaa kwa mda mrefu ukitafuta wateja ukilinganisha na machungwa au papai,

Yangu ni hayo ila sijawai kulima hayo madude mwisho wangu ni mbogamboga,
Asante kwa ushauri wako! Kama hutajali waweza share na mimi kuhusu kilimo cha mbogamboga?
 
Nakushauri lima Papai hasa hybrid
1.miezi 8 unaanza kuvuna mfululizo hadi miaka 3
2.haishambuliwi na wadudu hasa Miche niliyonayo
3.haina gharama za matunzo zaidi ya maji palizi na Mbolea
4.utawahi kurudisha gharama tofauti na mazao mengine.

5.mipapai mmoja matunda hadi 120
Heka moja mipapai 1200

Piga hesabu za roughly kila mwezi uvune matunda 700x500 =350,000 kwa mwaka ?
Uje nikuuzie Miche
Pia pita masokoni uulize Papai wananunua bei gani
0755404226 dsm kiluvya
 
hekari ni kubwa kushinda ekari hivyo basi miche 1200 ni kwenye ekari sio hekari.

ww unakabilianaje na uchavushaji hafifu maana ni changamoto kubwa kwenye hizi mbegu za kisasa.

maana vipapai vingi vinaanguka hivyo ile idadi ya mapapai 100 kwa mche inakuwa ndoto
 
bora ulime papai? tena tegea mvua za vuli uzuri wa papai ni kwamba unavuna mara nyingi alafu kila mti mmoja unavuna mapapai mengi kwa mpapai mmoja pia una weza kupanda papai na mazao mengine ukiwa unasikilizia yakue

athari yake
yana hitaji maji mengi dawa na uangalizi wa hali ya juu
yanakaa muda mrefu miezi 8 hadi kumi na mbili

yakiiva yanahitaji soko la uhakika
 
Mapapai hapana mpendwa wangu. Labda kama wewe ni risk taker.
Yanaweza kukupa pressure. Hasa ikitokea bahati mbaya inyeshe mvua ya mawe, uwiiiii.
Halafu pia yana ugonjwa fulani yanadonolewa yakishazaa.
Mengine unaweza kulima, kwanza yanasoko (Azam ni mnunuzi mzuri kama una mzigo mkubwa)
 
Asante kwa ushauri, ngoja niachane nayo kwanza
 
Back
Top Bottom