Asante kwa ushauri wako! Kama hutajali waweza share na mimi kuhusu kilimo cha mbogamboga?
Kilimo cha mbogamboga ni moja kati ya kilimo rahisi kulima lakini kigumu kwa maana yakikifanya biashara
Moja kilimo cha mbogamboga kwa maana yakukifanya kuwa biashara yako kinakuitaji mda mwingi kuwepo bustani ivyo iliuweze kulima mboga mboga kibishara uwe na mda wakutosha kuzihudumia
Pili uwe na maji ya uhakika kwani kinategemea sana maji kwa mfano mchicha ni moja ya mboga zinazoitaji maji mengi
Tatu uwe na mbolea ya samadi pia mbolea ya viwandani kama kani ni nzuri sana kwa kupandia kwani inafanya mboga kuwa na afya nzuri, pia uwe na eneo zuri lisilo nakivuli na lenye rutba nzuri yakustawisha,
Nne, SOKO hapa niongee kwa experience yangu kwani ni kitu ambacho nimewai kukifanya kwanza kabisa mbogamboga zinamsimu wake kwa mfano kipindi cha kwanzia mwezi wa saba hadi tisa kwendea kumi mbogamboga ni nyingi sana watu wengi wanalima mboga ivyo kupelekea bei kuwa ovyo sana sokoni hii kwa wewe mlaji utoona hapa tunaumia tu niwakulima kwani hata mboga ziwenyingi vipi wauzaji kwenye vibanda wataendelea kuuza bei ile ile fungu kwa mia tano,
Shida inakuja kwetu sisi wakulima mboga sinakuwa nyingi mashambani tunalazimika kuuza kwa bei ya chini sana tena kwa kuombea maana kila mtu anakuwa amelima, hiki kipindi wanalima watu wengi kwa sababu ya maji yanakwepo mengi ya mvua yaliotwama kwenye mabwawa,
Hivyo basi kwa ushauri wangu ukitaka kilimo cha Mboga Mboga kiwe na tija kwako nibora kabisa ukawa na soko la uhakika lakuuzia ndio uanze kulima kwa mfano unaweza ukaenda labda kwenye mashule wanayokula mboga, mahotelini, na hata kwenye masoko ukafanya tafiti na kupata mtu ambaye atakuakikishia kununua mboga zako ndio uanze kilimo serious kwa ajili ya Biashara,
Nimalizie kwa kusema kilimo cha mbogamboga ni kizuri kwani hata kikikupa hasara sio kubwa Sana kulinganisha na mazao mengi labda mda wako utakaokuwa umepoteza pia nikizuri ukikosa wateja unakula unajenga afya yako, japo unakuwa ujafikia lengo lako pia mtaji wake ni mdogo
Zingatio: uchambuzi huu ama uzoefu wangu nimeutolea kwa jiji la dar,