Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.
 
Picha zangu nilizopigwa nikiwa nimemezwa na chatu ziliuzwa sana pale uyole picha moja iliuzwa buku.

Cha ajabu sikufaidika hata na shilingi katika picha zile ambazo watu walineemeka kibiashara kupitia shida yangu.
 
Dah! aisee siku yako yakufa haikuwa imefika, ila pia hiyo mbinu ya kulala chali humpa wakati mgumu chatu kukumeza kwa sababu anakosa namna ya kujivingirisha kwenye mwili wako ili akuvunje na kukumeza.

Pia, chatu yupo katika kundi la nyoka wasio na sumu ndio maana jeraha lake unaweza osha na maji kama huduma ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana. Mbeya sehemu gani? Na hao waliopata ujasiri wa kukupiga picha badala ya kukuokoa ni kina nani? Walitumia simu au Camera za kawaida?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbeya karibu na reli ya tazara maeneo ya kambi ya jkt mbeya walikuwa na huo mtindo zamani wanapiga picha matukio halafu wanauza picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…