Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Hii Hii Suma Jkt mkuu? El nino ipi hiyo ya 2008, Mimi kama mdau wa uyole miaka hiyo nasema hii story yako ni chai!
 
Nikiwa darasa la tatu. Before hapo nilikuwa naziona flip phone za Samsung ziko vizuri lakini sikumbuki kunotice camera. Siemens na Nokia nilizokuwa naona hazikuwa na camera.
Mkuu mimi 2004 ndio nilimaliza degree, inamaana wewe hata mtandao wa tritel na celtel hujawahi kuisikia
 
Wengi husema elnino wakimaanisha mvua Kali

Nilivyomsoma sijaona uongo kwenye stori take ila labda Kama imemtokea mtu wa karibu yake

Sent using Jamii Forums mobile app


Ila chatu wa kutaka kummeza mtu mzima mmmhhhh???
Mtoto labda ila so mtu mzima
Mzee chatu ili akumeze ni lazima awe amejiviringisha kwenye mwili wako sasa unasemaje hujaona uongo? Kwahiyo unataka useme chatu ana mbio kuliko binaadam? Kilichomfanya asikimbie ni nini ikiwa chatu hajajiviringisha kwenye mwili wa jamaa?
 
Siku nyingine ukikumbana na chatu lala chini halafu angalia uwezekano wa kupata kijiti kikavu (hapa ujasiri unatakiwa) anza kukivunja kidogo kidogo (hata mara 10) ukiwa pale pale chini....Chatu atajiondokea zake, ukishagundua kaondoka amka timua mbio..
Kwanini ulale chini na si kukimbia?
 
Picha zangu nilizopigwa nikiwa nimemezwa na chatu ziliuzwa sana pale uyole picha moja iliuzwa buku.

Cha ajabu sikufaidika hata na shilingi katika picha zile ambazo watu walineemeka kibiashara kupitia shida yangu.
Pôle Sana mwana wa pepaa,ilikuwa Kijiji gani? Uyole naifahamu sana nimeishi pale karibu miaka 5
Ngulubhi Ali mghosi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.
Inaweza kua kweli japo we jamaa unaweza ukawa ni mtu MUONGO kuliko watu wote hapa East Africa

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Back
Top Bottom