SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Binafsi sikuwa mfuasi wa sera, mitizamo na style za kuongoza za Rais Magufuli. Nilimpinga waziwazi na sikuacha kutoa nyongo pale nilipoona anafanya mambo ambayo siyo, hasa yale ya kutumia madaraka yake vibaya na kuvunja sheria alizoapa kuzilinda.
Lakini lilipokuja suala ya ugonjwa wa COVID-19, kuna misimamo aliichukua ambayo inawezekana aliichukua kujilinda yeye na utawala wake usianguke ila upande wa pili wa shilingi, inawezekana baadhi ya misimamo ile ilikuwa sahihi kwa maslahi mapana ya nchi.
Hivi sasa, mataifa ya Magharibi yanamwaga mapesa ya misaada ya kutisha hapa Tanzania. Hii yote imekuja baada ya sisi kukubali kubadilisha misimamo na mitazamo yetu kuhusu ugonjwa wa COVID-19.
Naona kama kwa serikali ya Rais Samia kufanya kilichofanya, kuna mambo kama nchi tumeyapoteza na tunaweza tusije kuyapata tena.
Kwenye maeneo mengine nadhani Magufuli alikuwa anaiharibu nchi hata kama alikuwa ana nia nzuri. Huo utaendelea kubaki kuwa msimamo wangu.