dikir kab can
JF-Expert Member
- Mar 20, 2018
- 1,499
- 2,667
muda mzuri kabisa wa kula majanga uliyoyachuma na ndugu zako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ndo ulitengeneza mazingira achukiwe.Mzuka wanaJF dume rijali la JF mwenzenu nipokatika majutoo jamanii kamsaada...
Nilikuwa na mke mzuri, mwanamke aliyekuwa nguzo ya familia yangu. Alijitoa kwa kila hali, akahakikisha kila kitu kinaenda sawa, lakini mimi niliamua kumwacha kwa ajili ya ndugu zangu. Leo nipo peke yangu, nimepoteza kila kitu, na najuta sana.
Ndugu zangu walikuwa na chuki naye. Waliona kama yeye ndiye kikwazo cha kila kitu. Kila walipohitaji pesa, niliwaambia waongee naye kwanza. Nilifanya hivyo kwa sababu nilijua kuwa yeye ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusaidia, lakini badala ya kumheshimu walimchukia.
Mama yangu alipohitaji pesa, ilikuwa lazima mke wangu aridhie kwanza. Kila aliposema kuwa hana, ndugu zangu waliniona kama mtu aliyeshindwa kuwasaidia kwa sababu ya mke wangu. Walinichochea dhidi yake, wakaniambia kuwa anajenga kwao badala ya kujenga kwetu, kuwa ni mbinafsi na hataki ndugu zangu waishi maisha mazuri.
Mwanzoni nilipuuza, lakini chuki yao kwake ilizidi. Niliweza kuona jinsi wanavyomchukia, jinsi walivyoamua kufanya kila kitu ili aondoke. Mwisho wa yote, mama yangu na dada zangu wakaja na mpango wa kuhakikisha naachana naye. Walijaribu kila njia, walinitishia laana, walimfanyia visa, na mwishowe shangazi yangu alikuja na dawa.
Bila kujua, nikaanza kumchukia. Nilianza kuona kila kitu kama kasoro. Nilianza kumpiga, kumtukana, na kumkosoa kila alichofanya. Tulianza kuwa kama maadui ndani ya nyumba yangu mwenyewe.
Siku moja nilirudi nyumbani na nikakuta chakula hakijaandaliwa. Niliambiwa kuwa mke wangu alikuwa amekataa kupika, kwamba hata hataki ndugu zangu waingie jikoni. Sikujua kuwa alikuwa mgonjwa, nimempiga vibaya sana hadi ndugu zake walipokuja kumchukua. Hakurudi tena.
Baada ya kuondoka kwake, nilihisi nimepata ushindi. Ndugu zangu walishangilia kuwa hatimaye wamemtoa mke wangu kwenye maisha yangu. Lakini sikuwa najua kuwa nilikuwa nimevunja maisha yangu mwenyewe.
Ndipo ukweli uliponijia. siku hizi nipo tu humu JF najinafasi kamoyo kanguu jamanii