Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu.
Kuna kijana alipewa nafasi ya kuuliza swali akataka kujua ufafanuzi wa aya na inaonekana alikusudia aya mbili za surat naml (27:39-40). Kijana yule kwanza nampongeza maashaallaah anajua kusoma quran, alianza kwa kuzisoma hizo aya na bahati mbaya akaishia aya ya 39 sasa kama ujuavyo pale watu ni wengi na muda wenyewe siyo rafiki basi alipoambiwa aache kunukuu aya aulize swali lake moja kwa moja ndipo akawa kama amevurugwa kiaina akaomba tu kujua kiumbe anayetajwa alikuwa ni jini au mwanadamu?
Sote tunakubaliana kwanza kuongea mbele za watu ni mtiti na mara nyingi mtu unaweza ukawa una maswali mengi sana kichwani lakini siku ukikutana na anayefaa kuulizwa maswali yote yanayeyuka hukumbuki au unakumbuka mengine lakini ukashindwa kuwa na mpangilio sahihi. Ilionekana kama halieleweki swali lake na isivyo bahati ni kwamba hata mwongozaji hakumwelewa kijana alikusudia nini. Angemwelewa huenda angeweza labda hata kulifupisha swali na kuliweka sawa ili DR ZAKIR NAIK atoe majibu badala yake akamsitisha tu bwanamdogo kwamba swali lake mbona jibu lake lipo hapohapo aliposoma... kiumbe huyo alikuwa ni jinni. Ikawa ndio imeisha hiyo kijana wa watu akaondoka kwa fedheha
Kusoma quran kuna raha yake na mara nyingi sisi tusio na elimu tukikuta habari au mambo yanayovutia unatamani kujua mwendelezo wake na hapo ndipo unakuwa na shauku ya kuwauliza Mashekh. Swala hili hata mimi binafsi niliposoma aya hizo kwa mara ya kwanza zilinivutia sana na nilitamani sana nimjue kiumbe huyo wa pili kwenye aya ya 40 alikuwa nani ukiacha yule jini kwenye aya ya 39. Bahati mbaya ni kwamba habari hiyo inapatikana sehemu moja tu hiyohiyo haijarudiwa popote pengine
Nilipata nafasi ya kumuuliza Sheikh mmoja akasema yule anayetajwa kwenye aya hiyo ya 40 surat naml ni binadamu jina lake ni Asif (isivyo bahati nakumbuka hilohilo jina moja tu) alikuwa ni mwanawazuoni mkubwa katika mji ule wa mfalme Sulemani. Quran imesema alikuwa na elimu ya kitabu maana yake hakuwa jini. Kwa wasiojua nasummarize hapa chini kisa cha Nabii Suleiman kwa ufupi kuhusu kuletewa kiti cha malkia wa sheba. Nitaandika kwa kifupi sana kwa kadri nitavyojaaliwa
Aliuliza nabii sulaiman nani kati yenu ataniletea kiti chake huyo malkia. Akajibu na kuahidi jini mmoja miongoni mwa majini wenye nguvu kwamba angekileta kiti hicho kutoka Sheba kabla Sulaiman hajasimama hapo walipo kwenye kikao. Mara akajibu na kuahidi mwenye elimu ya kitabu kwamba yeye atakileta kiti hicho kabla Sulaiman hajapepesa jicho lake (yaani kufumba na kufumbua macho). Kweli shwaa Sulaiman anakiona kiti hicho hapo mbele yake! Sheba na sehemu alipokwepo Sulaiman ni sehemu mbili tofauti tena mbali kweli kweli lakini mtaalamu mmoja alifanya hayo aliyoyafanya kwahiyo ukisoma vitu kama hivi lazima usisimkwe na kutaka kujua zaidi
Allah ndiye mjuzi zaidi