Nilinusurika Kifo Baada ya Kuzama kwa Meli ya Titanic”

Nilinusurika Kifo Baada ya Kuzama kwa Meli ya Titanic”

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
ILIANZA nikiwatembelea wazazi na mjomba wangu wazee huko Jacksonville, Florida. Hii ilikuwa muda mfupi kabla ya mjomba wangu kufariki miezi michache iliyopita. Kama kawaida, tulienda kwenye Ibada ya Mashahidi wa Yehova siku ya Jumapili na kusikiliza hotuba iliyotolewa yenye Kichwa “Je, Utakuwa Mwokokaji wa ‘Siku za Mwisho’?”

Nilipokuwa njiani kurudi nyumbani, mjomba wangu alisema: “Hotuba hiyo ilinikumbusha nilipookoka msiba mbaya sana.” Alinyamaza kwa muda, kisha akaongeza: “Unajua, nilinusurika kuzama kwa Titanic.”

Baadaye nilimwomba mjomba wangu, Louis Garrett, anieleze kuhusu mkasa huo wenyekusisimua.

"Acha nirudi mwanzo," alisema. “Nilizaliwa mwaka wa 1900, huko Hakoor, Lebanoni, kijiji kidogo cha milimani kilicho umbali wa kilomita 130 hadi 140 kaskazini mwa Beirut. Familia yangu ilimiliki na kuendesha kinu cha mawe kinachoendeshwa na maji ambacho kilisaga ngano kuwa unga. Baba yangu alikuwa anafanya kazi ya kusaga hapo kijiji.

Mamlaka ya Serekali Iliatoa uamuzi kwamba familia yetu ilipaswa kuamia Marekani. Katika 1904 mama yangu na dada zangu wawili waliondoka Lebanoni. Baadaye, mwaka wa 1906, kaka yangu mkubwa aliondoka kwenda Marekani. Ilikuwa mwaka wa 1912, ili kukamilisha uhamiaji wa familia, kwamba baba yangu, dada yangu na mimi tulipaswa kuondoka kwenda Marekani.

“Mnamo Machi 1912, tulisafiri kwa meli hadi Marseilles, Ufaransa. Tukiwa huko, tuliandaliwa nafasi kwenye Meli ya Kifahari ya Titanic, hii ilikuwa ndiyo safari yake ya kwanza, kuelekea New York. Tarehe ya kusafiri kwa meli hiyo ilikuwa Aprili 10, 1912. Baba yangu alilazimika kuachwa huko Marseilles kwa sababu hangeweza kufaulu uchunguzi wa kimwili uliohitajiwa kwa sababu ya maambukizo ya macho aliyokutwa nayo.” Mjomba wangu alitabasamu na kusema: “Amebahatika sana!”

“Dada yangu alikuwa na umri wa miaka 14,” aliendelea, “na nilikuwa na umri wa miaka 12 tulipopanda Titanic. Tulihuzunika kumwacha baba yangu, lakini tulifurahi kuwa ndani ya meli ya R.M.S. Titanic, meli kubwa zaidi, yenye kasi zaidi na ya kifahari zaidi wakati huo—na pia ilisemekana kuwa haiwezi kuzama! Kulikuwa na zaidi ya watu 2,200 ndani ya meli hiyo, kutia ndani baadhi ya watu matajiri na mashuhuri zaidi wa wakati huo. Wengi walikuwa kwenye Titanic kusherehekea safari yake ya kwanza. Lilikuwa ni jambo la "hisia" sana. Kasi ya meli ilikuwa kama ilivyotarajiwa. Muda uliotarajiwa wa kuwasili New York ulikuwa Jumatano, Aprili 17. Maji yalikuwa shwari, hali ya hewa kwa kawaida ilikuwa ya baridi kwa Aprili.
....itaendelea.....
 
Uongo huu.....

Mbna naskia Ile movie ilichezwa kwenye swimming pool
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Nikajua story yako kumbe copy and paste toka jw. Swahili. Org
 
  • Kicheko
Reactions: 511
“Siku ya Jumapili, Aprili 14, siku yetu ya tano baharini, hali ya hewa ilibadilika kuwa baridi sana—baridi kali sana hivi kwamba si watu wengi waliokuwa kwenye Sehemu ya Deck. Tulisikia kwamba kulikuwa na Maonyo kubwa kulikuwa Mabunge mawe ya barafu katika eneo hilo. Hata hivyo aliyefikia maanani juu ya onyo hilo meli iliendelea na mwendo kasi wake.

Hata hivyo, nahodha wa meli nyingine ya California iliyokuwa inapita maeneo hayo ya Atlantiki ya Kaskazini, alitoa onyo kwa Naodha wa Titanic kuhusu milima ya barafu inayoonekana kwenye njia hiyo. Hili lilipuzwa kwasabu ya kujiamini kupita kiasi kwa Kapteni Smith, na wafanyakazi wenzake 700 na zaidi ya abiria 800.

..itaendelea...
 
Back
Top Bottom