Niliomba passport, miezi karibia miwili imepita naambiwa taarifa zangu zimeliwa!

Niliomba passport, miezi karibia miwili imepita naambiwa taarifa zangu zimeliwa!

Heee wewe wa February unalalamika? Mimi ni wa Dec 2025 nikaenda March hapo wakaniambia bado.... lile jicho nililowapa waliogopa wote wakaniambia kwani imekuwa je? inikawauliza so mnaona ni normal kabisa kunijibu hivyo walifuatilia kwa ukaribu sana na kunijia na jibu system ina shida. Naenda tena hapo next week mapema tuu
Ni kweli mfumo wao umeanguka.
Tatizo sio kuanguka kwa mfumo,tatizo ni kutokuwa na "back up".
 
Duh! suala la uhamiaji lishakuwa kero ya kitaifa sasa maana kila mtu analalamika , nyuzi zimejaa kuhusu wao mamlaka zipo kimya.

Hii inchi 🚮🚮🚮
Oya toto tundu bakini tu hukohuko msije huku mtoni mkatujazia vyoo.

De mbusii
 
Mkuu hao ni watu wajinga wajinga ukishandana nao utakwama parefu kwenye mambo yako, na marafiki zangu wengi tu kipindi flan walikua wanafata mali China walikutana na hiyo changamoto baadae Agency moja inayosafirisha mali kutoka China kuja bongo wakawasaidia... unachofanya unasubmit documents zako zote na kiasi flan cha pesa baada ya muda mfupi kila kitu kinakua tayari. Mpaka saiv wengi wanafanya hivo.
Basi kwa tabia hii maendeleo ya nchi sahau ni kukomaa tu na individual development.

Samia atosha tukutane2030
 
Watumishi wengi serikalini wameshaona mishahara na posho ni lazima wapewe bila kujali utendaji wao.

uwajibikaji kwa wananchi wanaochanga kodi za kuwalipa mishahara, umekuwa mdogo sana,

Hivyo ili wakufanyie kazi inabidi uwape kitu cha ziada, (RUSHWA)

Toa kitu kidogo, huna mtetezi hapo, ukiwaambia ukweli utaitwa mchochezi unaezua taharuki

Mimi nilipokuwa Europe niliambiwa ubalozi hauwezi ku renew passport mpaka nirudi Afrika. Niliporudi Afrika , Immigration waliniambia niwaletee barua toka tawi langu la CCM, baadaye niende na wadhamini 3 . Kumbuka ni ku renew tu. Nilipoenda kwa Katibu wa Tawi aliniambia anataka pesa ya wino. Tena nilienda na Mzee wangu aliyekuwa CCM mkubwa , nikampa chochote. Nikaenda Immigration na wadhamini. Baada ya wiki nimeenda kuichukua , Yule kijana wa Reception amniambia ili aende kuichukuwa na yeye apate chochote . Hii ndio serikali ya CCM ilipotufikisha
 
Kuna taarifa kwamba mfumo wao umeingiliwa. Hata wao hawajui kinachoendelea. Taarifa zisizo rasmi zinadai kwamba ni matokeo ya michezo ya "wahuni" , ambayo hata uhamiaji hawajui malengo yake. Kwahiyo, vuta subira mkuu.
kama kweli kuna wahuni wameidukua wafanye kila mwezi kwa idara zote maana zina ma IT na wanalipwa

wachangamshwe kdg wamelala sana
 
Wakuu nilifanya application ya passport pale Kurasini mwezi February mwishoni, na nikaambiwa March 24 nifate passport Wizara ya mambo ya ndani!

Sikwenda hiyo tarehe na nimekuja kwenda Ijumaa iliyopita, lakni cha ajabu kirahisi tu naambiwa taarifa zangu zimeliwa, hivyo nirudi tena Kurasini!

Sasa maswali ninayojiuliza, inawezekana vip taarifa zipotee kirahisi hivyo, maana ya kujaza ile hardcopy ni nini hasa? Je hawana backup system ya taarifa zao? Hata kama kwenye taarifa zimeliwa kwanini wasirudi kwenye hardcopy wapigie simu wateja kuwataarifu kilichotoke?

NB: Wenye uzoefu ili suala linawezekana au ni namna ya kutaka kuibia watu hela? Mpaka sasa sijafanya action yeyote, naomba maoni yenu nichukue hatua gani! Application nilifanya 24 February mwaka huu!

Taarifa Nyingine: KERO - Suala la Mfumo au Mtandao wa Uhamiaji kuwa chini muda mwingi ni kero
Rushwa ndio inatafutwa hap, apo wanaopata ndani ya wiki moja mpaka wiki mbili.

Its sad taasis kama hiyo ime bormalize rushwa ili kutoa huduma zake za msingi

Inanuka rushwa, takukuru huwa wanakuwa wapi sijui
 
Heee wewe wa February unalalamika? Mimi ni wa Dec 2025 nikaenda March hapo wakaniambia bado.... lile jicho nililowapa waliogopa wote wakaniambia kwani imekuwa je? inikawauliza so mnaona ni normal kabisa kunijibu hivyo walifuatilia kwa ukaribu sana na kunijia na jibu system ina shida. Naenda tena hapo next week mapema tuu

Hata next week hupati.

WhatsApp Image 2026-04-14 at 10.33.10 AM.jpeg
 
Ni kweli mfumo wao umeanguka.
Tatizo sio kuanguka kwa mfumo,tatizo ni kutokuwa na "back up".
Kama ni kweli hawana back up itakuwa ni upumbavu uliopitiliza, idara yao nzima ya IT, mkuu wao na usalama wanaohusika na uhamiaji watatakiwa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu taifa.
 
Mimi nilipokuwa Europe niliambiwa ubalozi hauwezi ku renew passport mpaka nirudi Afrika. Niliporudi Afrika , Immigration waliniambia niwaletee barua toka tawi langu la CCM, baadaye niende na wadhamini 3 . Kumbuka ni ku renew tu. Nilipoenda kwa Katibu wa Tawi aliniambia anataka pesa ya wino. Tena nilienda na Mzee wangu aliyekuwa CCM mkubwa , nikampa chochote. Nikaenda Immigration na wadhamini. Baada ya wiki nimeenda kuichukua , Yule kijana wa Reception amniambia ili aende kuichukuwa na yeye apate chochote . Hii ndio serikali ya CCM ilipotufikisha
Oyaa wewe bado ni dogo tu unaishi kwa wazazi. Unavyoandika unajifanya mtu wa zamani. Wazenj bana.
 
Back
Top Bottom