Dennis R Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 267
- 372
Makaburi yamebomoka mizizi imekatika,
Limebaki shina tu,
Zile zama za zaman zimeisha,
Kiburi na dharau zilikuponza,
Ulipenda kutumia nguvu kuliko akili,
Ulikataa maonyo ukakumbatia kiburi,
Ulimkufuru Mungu maksudi,
Utupu wako uko wazi kila mtu anauona,
Maji yaliyopoa ndo yenye nguvu,
Yakupasayo aman yalifichwa machoni pako,
Nyumba yako imefunikwa na ukiwa,
Ghasia na mifarakano haitakoma kwako,
Utatumia nguvu kurudisha enzi zako,
Hutaweza sababu mizizi imekatwa,
Dhambi yako imeandikwa kwa kalamu ya chuma na ncha ya almasi.
Limebaki shina tu,
Zile zama za zaman zimeisha,
Kiburi na dharau zilikuponza,
Ulipenda kutumia nguvu kuliko akili,
Ulikataa maonyo ukakumbatia kiburi,
Ulimkufuru Mungu maksudi,
Utupu wako uko wazi kila mtu anauona,
Maji yaliyopoa ndo yenye nguvu,
Yakupasayo aman yalifichwa machoni pako,
Nyumba yako imefunikwa na ukiwa,
Ghasia na mifarakano haitakoma kwako,
Utatumia nguvu kurudisha enzi zako,
Hutaweza sababu mizizi imekatwa,
Dhambi yako imeandikwa kwa kalamu ya chuma na ncha ya almasi.