ephen_
JF-Expert Member
- Oct 28, 2022
- 14,949
- 54,485
Ni ya ukweli au ya kutunga?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni ya ukweli au ya kutunga?
Tuweke wazi kuwa hii ni chai ndio tuendelee kufuatiliaWatu wa story kali, iko complete from a to z. Tag others tuburudike, ina mafunzo pia, visa............ Sharing is caring
Sina hata uhakika , vip lakin?Ni ya ukweli au ya kutunga?
FreshSina hata uhakika , vip lakin?
OkNILIPEWA KAZI IKAZUA KIZAAZAA.
Episode 1: Maandalizi ya Mitihani na Simu ya Ajabu..
Ilikuwa asubuhi saa nne, ndio muda naamka hostel na niliamshwa na mlio wa simu kutoka kwa rafiki yangu, Jonas. Tulipanga kukutana kwa ajili ya kujadili mambo ya mitihani kwani tulikuwa na wiki tatu tu kabla ya kuanza mitihani yetu ya mwisho.
Nilijitayarisha haraka na kutoka nje. Hali ya hewa ilikuwa ya baridi kama kawaida ya Mbeya, hivyo nilivaa koti langu jepesi na kuelekea nje. Nilipokutana na wanafunzi wenzangu wakiota jua nje, tulianza kutaniana kama kawaida.
Marchey: "Eh bwana eeh, haya mapacha ya Mbeya hayajawahi kubadilika, kila siku jua linaota saa sita mchana!"
Mwanafunzi 1: "Hah! Wewe ndio ulikuwa usingizini mpaka saa nne, ndio maana unajiona kama umekosa jua."
Mwanafunzi 2: "Ama kweli, Marchey unajua hata vipindi vingine umekuwa kama sio wako. Unatumiaje muda wako wa ziada?"
Marchey: "Hah! Si mnajua tu mambo ya project za Mzee Kijana... Nimekuwa busy sana."
Baada ya utani huo, nilielekea kwenye mgahawa wa karibu kupata kifungua kinywa. Nilipokuwa nakunywa chai yangu ya moto, simu yangu iliita tena. Niliitazama na kuona namba isiyojulikana.
Marchey: "Hello?"
Simu: "Marchey, ni mimi Mzee Kijana. Nakumbuka ulifanya kazi nzuri sana kwangu ile mara ya mwisho. Nimepata kazi nyingine, nataka ufanye uchunguzi mdogo kwa ajili yangu."
Marchey: "Ah, Mzee Kijana! Vipi tena? Mambo ni mazuri lakini? Kazi gani hiyo sasa?"
Simu: "Kuna mtu anaitwa Mr. X, nataka umfuatilie kidogo, angalia shughuli zake za kibiashara. Unakubali?"
Marchey: "Mzee Kijana, unajua nipo na mitihani mbele yangu sasa. Ila nitajaribu kuangalia wakati wangu wa ziada."
Simu: "Asante sana. Ni muhimu sana, usisahau. Tutawasiliana baadaye."
Niliendelea na kifungua kinywa changu huku nikifikiria kuhusu kazi hiyo. Nilijiuliza kwa nini Mzee Kijana ameniomba kufuatilia mtu huyu kwa sasa. Ilikuwa kazi tofauti kabisa na zile alizowahi kunipa awali za kuedit vitu, kuscan na kutengeneza mifumo midogo. Lakini nikaweka kando mawazo hayo na kuelekea library kukutana na Jonas kwa ajili ya maandalizi ya mitihani.
Jonas: "Hey Marchey, habari ya asubuhi? Umekuja na plan gani leo?"
Marchey: "Eh bwana eeh, kuna kazi mpya nilipewa na Mzee Kijana, inabidi niwe makini na muda wangu sasa. Lakini kwanza, tuanze na haya maswali ya mtihani."
Tulikaa library kwa masaa kadhaa tukijadili na kujiandaa. Baada ya hapo, niliamua kufanya uchunguzi kidogo kuhusu Mr. X. Nilianza kuangalia data zake na kugundua kuwa alikuwa na shughuli nyingi za kutiliwa shaka.
Niliporudi hostel jioni hiyo, nilikuta tena simu yangu inaita.
Marchey: "Hello?"
Simu: "Marchey, Mr. X anaonekana kuwa na shughuli hatari. Usicheze na hii kazi. Ukihisi chochote kibaya, acha mara moja."
Marchey: "Mzee Kijana, kuna kitu unajua na hujaniambia?"
Simu: "Nimeshakuambia yote. Baki macho, kijana."
Nilihisi wasiwasi kidogo lakini niliamua kuendelea kwa umakini. Kadri nilivyoendelea na uchunguzi wangu, ndivyo nilivyozidi kugundua kuwa Mr. X alikuwa na uhusiano na kundi la kigaidi. Hapo ndipo nilipoanza kuhisi kuwa maisha yangu yako hatarini.
Wiki iliyofuata ilikuwa ngumu, maandalizi ya mitihani pamoja na kazi ya uchunguzi iliyonizidi. Nilijaribu kushiriki shughuli za kawaida za chuo, lakini kila mara nilihisi kama kuna watu waninifuatilia.
Jonas: "Marchey, unaonekana na mawazo sana siku hizi. Kuna kitu kinaendelea?"
Marchey: "Jonas, hakuna kitu bwana... Labda presha tu ya mitihani."
Jonas: "Usijali, tunamalizia hizi siku chache halafu tunarudi nyumbani. Utapata muda wa kupumzika na familia."
Marchey: "Ni kweli, nitakoma kidogo haya mawazo yote."
Baada ya mitihani ya kufunga mwaka wa kwanza wa masomo, nilijitayarisha kurudi nyumbani Mwanza. Nakumbuka ilikuwa saa tano mchana tarehe 23 Juni 2019, nilikata tiketi yangu na kusubiri safari katika kituo cha mabasi cha Mbeya.
Nikiwa nimekaa nikisubiri basi, niliona gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser likipita taratibu. Nilihisi kama kuna watu wananiangalia. Nilijaribu kujipooza kwa kudhani ni mawazo tu, lakini hisia zangu ziliniambia kuwa kuna kitu si cha kawaida.
Marchey: "Mzee Kijana alisema niwe macho... Lakini nadhani ni mawazo tu ya mitihani yanayonisumbua."
Nilipanda basi kuelekea Mwanza. Safari ilipoanza, nilihisi kama kuna mtu ananifuatilia. Nilikuwa nimekaa karibu na dirisha, nikawa naona gari ile ile nyeupe ikitokea mara kwa mara kwenye njia. Nakumbuka ilikuwa saa kumi na moja jioni tuliposimama katika kituo cha mapumziko kijijini Isenye.
Marchey: "Kuna kitu kinanishitua hapa... naona bora nishuke kidogo."
Nilijifanya kama nataka kwenda kujisaidia, kisha nilishuka na kuanza kutembea polepole kuelekea msituni. Nilijua kuwa nikikimbilia moja kwa moja, wangenitilia shaka. Nilipofika msituni, nilianza kukimbia bila kuangalia nyuma.
Marchey: "Ninahitaji usalama wangu kwanza... lazima nijifiche."
Nilipofika mbali kiasi, nilisimama kupumzika na kujificha kwenye kichaka. Nilisikiliza kwa makini ili kuhakikisha hakuna anayenifuata. Nilipokuwa na uhakika kuwa niko salama, nilianza kufikiria njia ya kutoka eneo hilo na kufika nigeuze kwenda Dar es Salaam maana ndio ilikuwa plan yangu endapo wataendelea kunifuatilia.
Nikawa kama nimekumbushwa na mtu... Nikamkumbuka mtu ambaye sijui hata kwanini nilimkumbuka... (Anaitwa sophie)
Niliamua kutumia ujuzi wangu wa IT kutafuta msaada. Niliingia mtandaoni na kudukua database ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, nikapata mawasiliano ya Sophie. Nilikumbuka tulivyokutana kwenye mashindano ya wanafunzi wa IT, na nilijua kuwa yeye pekee angeweza kunisaidia.
Marchey: "Sophie... najua utaweza kunisaidia. Sasa ni wakati wa kumtafuta."
Niliwasiliana naye kupitia barua pepe na ujumbe mfupi, nikimuelezea kwa ufupi kuhusu hali yangu na kumkumbusha tulivyokutana. Baada ya majaribio kadhaa, hatimaye alipokea ujumbe wangu na tukaanza mawasiliano.
Marchey: "Sophie, ni Marchey. Nakumbuka tulikutana kwenye mashindano ya IT. Niko kwenye hali mbaya sana sasa hivi... Nahitaji msaada wako."
Sophie: "Marchey? Oh, ndiyo... nakumbuka. Kuna nini kimetokea?"
Marchey: "Ni hadithi ndefu... Lakini kwa sasa, nahitaji kujificha. Naomba unisaidie."
Sophie: "Usijali, nipo hapa kusaidia. Niambie upo wapi na nitakuja kukuchukua."
Nikiwa bado msituni, nilijua kuwa lazima nipate njia ya kufika Dar es Salaam bila kugundulika. Sophie alikuwa tumaini langu pekee. Nilijificha vizuri huku nikiandaa mipango ya safari yangu ya kwenda Dar es Salaam kwa usalama.
Marchey(niliwaza): "Huu ndio mwanzo wa kizaazaa kikubwa zaidi maishani mwangu... Lakini najua nitavuka."
***********
Ilikuwa ni usiku wa saa nne nikiwa bado msituni nikijaribu kutuliza akili yangu baada ya kukimbia sana mchana kutwa. Nilihisi njaa kali lakini usalama wangu ulikuwa kipaumbele. Wakati huo, nilikuwa na simu yangu ndogo tu ya kawaida ambayo iliweza kunisaidia kuwasiliana na Sophie.
Marchey: "Sophie, nimeweza kujificha kwa sasa... lakini sitakuwa salama hapa kwa muda mrefu. Niko maeneo ya Isenye."
Sophie: "Usijali, Marchey. Nitajitahidi kufika haraka. Nitachukua gari na nitakutafuta."
Marchey: "Asante sana, Sophie. Nitajaribu kutafuta sehemu salama zaidi kujificha kwa muda."
Baada ya mawasiliano hayo, nilijua kuwa lazima nipate sehemu bora zaidi ya kujificha kabla Sophie hajafika. Niliamua kuelekea upande wa pili wa msitu, nikijaribu kujiepusha na njia kuu. Nilitembea kwa muda, hatimaye nikapata kichaka kirefu kilichokuwa na miti mikubwa, ambacho kilionekana kama sehemu nzuri ya kujificha.
Nakumbuka ilikuwa karibu saa tano usiku nilipojificha kwenye kichaka hicho. Nikiwa hapo, nilijaribu kutafakari kuhusu yote yaliyotokea. Nilijiuliza jinsi gani maisha yangu yalibadilika ghafla kutokana na kazi moja niliyopokea kutoka kwa Mzee Kijana. Niliogopa polisi kugundua kuhusu kazi hiyo, hasa kwa sababu nilijua wanaweza kugundua shughuli zangu zote za awali na hatimaye kunifuatilia zaidi.
Marchey: "Huu ni mtihani mkubwa sana... lakini lazima niondoke hapa salama."
Baada ya muda, nilisikia mlio wa gari ikikaribia. Niliinuka kwa tahadhari na kutazama kwa makini. Ilikuwa gari ya Sophie. Alikuwa amepambana kuja usiku huo na kuniokoa.
Sophie: "Marchey, niko hapa! Njoo haraka."
Nilitoka haraka kutoka mafichoni na kuelekea kwenye gari. Nilipoingia ndani, nilihisi faraja kubwa. Sophie alionekana na wasiwasi lakini alijitahidi kutabasamu ili kunifariji.
Sophie: "Sijui umefikaje hapa, lakini ni vizuri tuko pamoja sasa. Tuende Dar es Salaam mara moja."
Marchey: "Asante sana, Sophie. Siwezi kueleza jinsi nilivyohisi salama baada ya kukuona."
Tulianza safari ya kuelekea Dar es Salaam usiku huo huo. Njiani, Sophie aliniuliza maswali kuhusu hali yangu na kwa nini nilihitaji msaada wake ghafla. Nilimuelezea kwa ufupi, nikiogopa kumweleza kila kitu kwa undani.
Marchey: "Ni hadithi ndefu, Sophie. Ilianza na kazi moja niliyopokea kutoka kwa Mzee Kijana... Nilijikuta nikihusishwa na shughuli za kigaidi bila kujua. Sasa naogopa kuwa wananifuatilia."
Sophie: "Pole sana, Marchey. Nadhani umechukua uamuzi sahihi kwa kuondoka huko haraka. Tutafika Dar es Salaam na nitakusaidia kujificha kwa muda."
Tulipofika Dar es Salaam, ilikuwa saa kumi usiku. Sophie alinipeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwake. Nyumba yake ilikuwa ya kupanga, yenye chumba kimoja cha kulala na sebule moja. Nilihisi aibu kidogo kwa kuwa nilijua nitakuwa mzigo kwake, lakini nilikuwa sina chaguo.
Sophie: "Marchey, utalala sebuleni. Nitakupatia kila unachohitaji. Usijali, tutaona jinsi ya kushughulikia hali hii kesho."
Marchey: "Asante sana, Sophie. Nashukuru sana kwa msaada wako."
Nililala kwenye sofa sebuleni huku mawazo mbalimbali yakipita kichwani. Nilijiuliza ni lini nitapata utulivu tena maishani mwangu. Lakini nilijua kuwa na Sophie karibu, nitaweza kushinda changamoto hii.
Asubuhi iliyofuata, tulianza kupanga jinsi ya kujificha na kuepuka magaidi. Sophie alionekana na matumaini zaidi, na kunipa nguvu ya kuendelea kupambana.
Sophie: "Marchey, tutatumia ujuzi wetu wa IT kuwafuatilia magaidi hao na kujua siri zao. Lakini kwanza, tunahitaji kujificha vizuri."
Marchey: "Ndio, Sophie. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunakuwa salama na kuwazidi ujanja."
******
Hapo ndipo nilianza kujifunza kuwa maisha ni mapambano ya kudumu... na safari yangu ya kizaazaa ilipoanza rasmi.
###########
sory mkuu, namna unavyosimulia inaonekana kabisa haina haja ya kuweka convo baina yako na wahusika wengine, inaonekana kama vile inajirudia hivi,,rejea nadhani utanielewaKuna ukweli uliotiwa chumvi