NILIPEWA KAZI IKAZUA KIZAAZAA.
### Episode 6
Endelea...
Nilikuwa naendesha shughuli zangu za kila siku...
Siku moja nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu Alex.
"Marchey, vipi bro?" Alex alionyesha kuwa na furaha na kuchangamka...
"Poa blood, vipi wewe?" Nilijibu.
"Fresh tu yaan... Nina habari njema, nimepata kazi ya kutengeneza mfumo wa shule moja ya sekondari hapa Dar. Unaikumbuka ile Shule X?"
"Yeah, naijua. VP mfumo gani bro na umepataje hilo deal?"
nilisema, nikihisi furaha sana na msisimko maana nilijua alex ni mtu anaependa kunishirikisha deals kama hizo...
"Kuishi vizuri tu na watu bro... Skia sasa, Nataka tushirikiane tufanye pamoja. Unaonaje?"
"Bila kupingwa bro... usiwe na shaka, nitafurahi sana tukishirikiana wote si unajua sina mchongo wowote... Ni lini tunaanza kwanza?"
"Ma jobless haturembi bro... Kesho asubuhi, tufanye kudesign hiyo kazi mara moja. Nitakupitia nyumbani saa mbili. Then tutajua kazi nyenyewe tunaanza kesho hiyo hiyo au vp"
"Sawa bro, asee ujue unaniokoa sana asee... tutaonana kesho basi."
Tulimaliza mazungumzo yetu na nikaanza kujiandaa kwa ajili ya kazi hiyo. Nilikuwa na furaha kubwa kwa sababu ilikuwa ni fursa nzuri ya kujiongezea kipato na kufanya kazi na rafiki yangu....
#Simu kutoka kwa Sophie
Siku ya pili, tulianza kazi yetu ya kutengeneza mfumo wa shule. Tulikuwa katika harakati za kumalizia mambo muhimu ya siku ya kwanza ambayo hatukukamilisha... unaambiwa tulifanya kazi kama tumetumwa na kijiji😂...
Tulipokuwa tukiendelea na kazi... Kuna wakati nilipopokea simu kutoka kwa Sophie...
"Marchey, unaendeleaje, Vp hali yako?" Sophie aliuliza.
"Nzuri tu, vipi wewe? Mbona umebadilika sana tofauti na zamani?"
"Mambo ya mimi kubadilika hayakuhusu... Niko poa. Nilikuwa nataka kukuambia kuwa baada ya siku mbili, nitakuwa na sherehe nyumbani kwangu kwa ajili ya mgeni wangu kutoka Arusha. Anaitwa Hassan, na ndiye mpenzi wangu," alieleza Sophie kwa madharau mpaka Alex akagundua nilipandwa na hasira...
Nilihisi moyo wangu ukiuma. "Oh, sawa. Nitakuwepo." Nikajibu kiume short and clear nae akakata simu bila kujibu kitu...
Nikawa najiuliza nimemfanyaje huyu mtoto... Pia nilijuta kumwonesha kuwa nilimpenda maana hizi dharau lisingekuwepo...
Alex aliona uso wangu umebadilika na akauliza, "Nini tatizo?"
"Nimealikwa kwenye sherehe na Sophie. Mpenzi wake anakuja kutoka Arusha," nilimjibu, sauti yangu ikiwa na huzuni.
"Tulia bro, itakuwa sawa, afu tutaenda kuua kwa mazawadi pale ili hata huko aendako atakukumbuka..." Alex aliniambia huku akijaribu kunifariji na kunipiga piga begani...
******
#Ujumbe Kutoka kwa Grace
Baada ya kumaliza kazi ya siku hiyo, nilipokea ujumbe kutoka kwa Grace. Ujumbe huo ulikuwa na picha ya Master Go akiwa ameuwawa...
"Master Go amekamatwa kwa kuiba milioni 5... Na niliandika ripoti fake na kumchonganisha na boss. Boss akamuua,"
ulisomeka hivo ujumbe kutoka kwa Grace....
Nikashtuka, nikamwonyesha Alex. "Tazama hii, Alex."
Alex alishtuka sana...
"Hii ni mbaya, sasa naona kabisa team yetu ishakufa... Grace amekuwa mkatili sana," alisema Alex kwa mshangao.
"Sasa tunafanyaje?" Niliuliza, nikihisi wasiwasi.
"Tunapaswa kuwa makini. Hatujui Grace atafanya nini tena," Alex aliniambia.
Tulifanya kazi kwa bidii na baada ya siku chache, tuliweza kukamilisha mfumo wa shule ya sekondari. Mfumo ulikuwa na vitu vingi muhimu na ulikuwa mahiri sana.
Tulipokabidhi, tulilipwa zetu mpunga ambao sikuwahi kulipwa kwa kufanya kazi ya uhalali... ilikuwa milioni 2.
"Mfumo nimeupitia na nimeridhika nao... vijana mpo vizuri sana na naahidi kuwashirikisha kwenye kazi kama hizi siku nyingine... Hii ni kazi nzuri sana," alisema mkuu wa shule na kutuambia kuwa hela zetu anatuma muda huo huo kwenye account yetu ambayo tulimpatia na tukaona ujumbe wa malipo...
"Asante sana," nilijibu kwa furaha.
Kila mtu alikuwa na furaha wakati huo tukirudi maghetoni tukiongea njiani...
"Tutagawana vipi pesa?" Alex aliuliza.
"Tutagawana sawa, milioni moja kwa kila mmoja," nilimwambia bila kujali yeye ndio alinipa deal😂
"Hahahaha najua unachofikiria... usijali ndio maana nilikushirikisha maana wewe una ujuzi mkubwa na umefanya kazi kubwa kuliko mimi... hiyo ni sawa kabisa usijali"
alisema Alex, na tuligawana pesa zetu tulipofika home...
******
Siku moja, nilikuwa natembea mjini usiku wa saa tano. Niliona gari linanifuatilia kwa muda wa kama dakika 20 hivi kila nilipoelekea... Nilishtuka na kuanza kuongeza speed... na jamaa walivyojua kuwa nimegundua wakaamua kulianzisha vurugu wakati naanza kukimbia....
Ni Watu waliovaa vinyago walishuka kutoka kwenye gari na kuanza kunikimbiza kwa miguu, wakipiga risasi hewani... Mpaka sikuamini kivipi maskini kama mimi naandamwa hivi...
Nilijaribu kukimbia kwa nguvu zangu zote, nikadondisha simu yangu ndogo lakini sikujali kuiokota...
niliomba miguu yangu nisaidie japo niwaache hawa wajuba ka umbali kidogo nijifiche...
mtaani watu waliposkia milio ya risasi ni mtafutano tu na me nikajichanganya kwa watu nikazama vichochoroni kwenye mitaro...
Nilijificha kwenye mtaro kama kichaa, nikiwa naogopa sana... Na sikutoka nililala humo...
Kesho yake asubuhi, saa kumi na moja, likiwa bado giza, nilitoka kwenye mtaro na kuanza kufuata njia ya kurudi nyumbani kwa machale...
Nilifanikiwa kufika nyumbani kwangu na kuwasha PC yangu
Nilimtumia ujumbe wa email Alex haraka na kumuomba aje mara moja nyumbani kwangu...
Baada ya dakika kama hamsini hivi Alex alifika na nikamsimulia kila kitu...
"Daah msela wangu dunia inakuandama sasa, Hii ni hatari, lazima tufanye kitu," alisema Alex.
"Kuna muda mpaka nawaza kuhama, nahitaji mipango ya haraka nichomoke bro" nilimjibu.
Wakati huo Nilikuwa na milioni sita (6,000,000/=) kwenye akaunti yangu, nikijumlisha milioni moja tuliyogawana na Alex na zile milioni tano alizonitumiaga Grace kwa ajili ya msiba wa Tony...
"Nataka nihame Dar, maana sina amani kuendelea kuishi mjini hapa," nilimwambia Alex.
"Uko sahihi, itakuwa bora ukihama kwa muda hata kama utarudigi baadae hali ikiwa shwari... Maana saivi hapana kwa kweli," alisema Alex.
Siku hiyo sikumshirikisha Sophie, kwani nilihisi kuwa hayupo upande wangu tena na sikumwambia chochote kuhusu kilichonitokea...
#Mimi na Alex kwenda supermarket kununua zaga...
Jioni nilimpigia Alex na tukakubaliana tukaenda kununua zawadi kwa ajili ya mgeni wa Sophie. Tulinunua zawadi ya pamoja na tulitumia kama laki tatu hivi...
"Hii ni zawadi nzuri," alisema Alex.
"Ndiyo, itamfurahisha Sophie na mgeni wake bwana shemeji..." nilijibu nikiwaza basi tu kwa vile Sophie aliwahi nisaidia sana huko nyuma....
Siku ya sherehe ilifika na kulikuwa na watu wengi kidogo kama thelathini na kitu hivi...
#Usilolijua ni sawa na usiku wa giza...
Kumbe bana sijui ulikuwa ni mtego, au ni aliona hii ndio chance ya kuninasa windo lao...
Wakati huo kumbe wajomba wale walikuwepo kando wakisoma ramani...
naam! Wale wazee wa pilika walionivamia usiku walifika pale pale kwenye sherehe....
Niligundua walipokuwa wakinifuata na mmoja wao akachomoa bastola nikashtuka kumuwahi kwa ujasiri ili nimsukume maana alikuwa karibu yangu...
Mjeda sijui alijiamini nini tu yaani na hakufunika sura yake na kitu chochote...
Akaniwahi bhana akafyatua chuma na kuniparaza kwenye bega... Watu wakapiga kelele... zikapigwa nyingine juu kama nne hivi na wale wajeda wengine... Watu walipiga kelele na kuanza kukimbia...
Yule jamaa aliniparaza lakini nilifanikiwa kumsukuma akaanguka chini na pale pale wale wengine wakawa wanakuja upande wangu...
Kidume nikazama ndani nyumbani kwa Sophie...
Nimeingia mule nikijua leo ndio mwisho wangu...
Wazo likanijia kuwa nijiokoe vinginevyo nitakufa kweli...
Wakati huo kumbe Sophie alikuwa ndani akiongea na simu na aliponiona akakata simu kuniangalia...
Nikampush pembeni nikavunja kioo cha dirisha na kiti nikaruka upande wa nyuma ya nyumba...
Nilivyotoka nje nilikimbia na kupotelea vichochoroni, haraka sana nikafika nyumbani kuchukua PC yangu na suruali mbili, nikaweka kwenye mfuko na kukimbilia mafichoni kwa jamaa mmoja niliyekuwa napenda kucheza naye games na yule jamaa alizoeaga mititi kama hii, ko nilipomsimulia skanipa pole tu pale akasema nimecheza kama nipo kwenye game mwenyewe na hakushtuka sana...
Maana yeye alishawahi kushika chuma mara kadhaa na alishawahi kumtaitisha mtu akatoa mali kwa kumtushia bastola...
Kesho yake asubuhi nilienda stendi na kukata tiketi nikiwa na mpango wa kusepa kabisa niondoke Dar rasmi...
Nilikuwa Nimetibiwa kidogo kwenye duka la dawa jeraha langu...
Kesho yake asubuhi sana saa 11 nikapanda chuma na nikaanza safari ya kuelekea Shinyanga...
Mpaka siku hiyo ya pili sikumtafuta Alex wala Sophie... Na cha ajabu Sophie hakunitafuta kabisa wala kunitumia ujumbe wa email... Lakini Alex alinitafuta kwa email lakini sikumjibu chochote nilitaka nihakikishe nimefika shinyanga kwanza ndio nitamjibu...
Nikiwa kwenye gari muda huo, Grace alinitumia ujumbe wa email akisema "Marchey, acha kuwa mgumu wa kufa. Unajua naingia gharama kubwa kiasi gani kuagiza watu waje kukuua."
Nikashangaa sana nikajibu...
"Haaaah! Grace huyu huyu nnaekufahamu... Tunaweza kuongea vizuri, Grace. Kwa nini unataka kuniua?" nilimwambia.
"Usijali, Marchey. Nitakuua muda ukifika..." alisema Grace kwa hasira.
Na mimi sikujibu chochote hofu ikanijaa tena...
Niliamua kuendelea na safari yangu, nikiwa na matumaini ya kuanza maisha mapya mbali na Dar
***************
#Kuwasili Kahama (Shinyanga)
Baada ya siku mbili, nilifika Mkoani Shinyanga mji mmoja panaitwa Kahama, pale pamejaa wafanya biashara wadogo wadogo na wakubwa wa madini ya dhahabu...
Nilimtafuta rafiki yangu niliesoma nae o-level, anaitwa Ezekiel, ambaye alikuwa akifanya biashara ya dhahabu huko.
Baada ya kupata mawasiliano yake nikamcheck...
"Oy Eze, vipi rafiki yangu? Mnyama Marchey don apa".
"Fresh asee niajeee mjuba?"
"Kama kawa mwana, nipo kahama now ndo nafika apa fanya kunihifadhi sina pa kuchili "
"Aseee acha utani nakujua Marchey! Umefika fikaje Kwanza... Af umepotea sana... Sema uko Sehemu gan kwanza" Ezekiel alisema kwa furaha.
"Ahahahaaa nipo maeneo ya Government huku karibu na soko dogo la dhahabu... Nilikuwa natembea tembea kidogo si unajua..., naomba nihifadhi kwa muda bro...,"
Tuliwasiliana na baadae akaja pale na Toyota Land cruiser kali mpaka nikaduwaa...
"Daah maisha ushayakill bro unamiliki mpaka ndinga kali hivi..."
"Hahaha, na ukiona ndinga utasemaje sasa... Hata hivyo sio yangu ni ya boss wangu..."
Tuliongea pale na akanichukua kwenda kwake alikuwa na mke mzuri sana yaani...
Nikapumzika pale baadae tukaingia Town kula misele kwanza... Huku nikimueleza kuwa nahitaji kupata kazi yoyote nifanye kwa mwezi mmoja...
Ukweli jamaa alikuwa na pesa nyingi sana japokuwa nae alikuwa na boss wake lakini alikuwa akiendesha biashara zake mwenyewe za kuuza na kununua dhahabu...
"Hakuna shida, nipo bro me kukusaidia nitakusaidia Kuna kijiji kimoja nje hapa, naweza kukupeleka ukapige mishe za dhahabu ," alisema Ezekiel.
"Asante sana kaka, nikipata kazi itanisaidia sana," nilimjibu.
"Poa, Tutakwenda keshokutwa asubuhi, ili kesho ujiandae, maana week hii nasafiri kwenda kuuza dhahabu nje na hapa" alisema Ezekiel.
Nilimshukuru na kuanza kujiandaa kwa kazi hiyo mpya. Sikumweleza chochote kilichonitokea huko dar...
#Maisha ya Mgodini
Sasa me nilijua nitapata kazi ya uhakika kumbe kazi yenyewe ni ngumu balaa...
Ezekiel akanipeleka kijiji kimoja nikafanye kazi...
(Ukumbuke wakati huo nina Milioni 5 na laki 7 mfukoni lakini sikutaka kuitumia kabisa...)
Nikafika mgodini bhana nianze kazi...
Kazi ya mgodini haikuwa rahisi. Nilitumia muda mwingi kuchimba dhahabu kwa kuingia kwenye mashimo yaliyochimbwa na ni hatari sana, wakati mwingine nilikuwa nafanya kazi ya kupembua dhahabu maana nilijifunza na kupembua kulikuwa kunalipa kidogo...
Kazi ya kutafuta dhahabu kutoka kwenye mawe ni miongoni mwa kazi ngumu na za kiume...
Japokuwa nilianza kupata pesa kidogo za kujikimu lakini mwili wangu ulianza kukonda...
Nikawa najiuliza mbona huyu Jamaa ananitafutia kazi ngumu hivi halafu yeye anatembelea gari?
Wakati mwingine nawaza nianze kununua dhahabu na kuuza nitumie ile milioni 5, lakini napo naogopa isije kutokea siku moja Grace akataka mzigo wake😂
Ebana eeeh nikasema haya maisha siyawezi... Na hapo nilikuwa na week 3 napata vihela kidogo tu vinaishia Kwenye kulipia kodi na wakati huo nilianza kutuma pesa kidogo nyumbani, lakini sikuwaambia kuwa niko Shinyanga mgodini, maana kwanza ni karibu na nyumbani...
Siku moja nikaamua Nimcheck Ezekiel...
Nikamtumia ujumbe
"Oy kaka Ezekiel, kazi hii ni ngumu sana, naona bora nianze kununua dhahabu tu na kuuza" nilimwambia...
Akajibu...
"Ni kweli, lakini inakulipa kidogo kidogo... Jaribu kuvumilia Utaona matokeo yake baada ya muda," Ezekiel alisema.
"Ni kweli kaka, lakini saivi hadi mwili wangu umekonda, na siingizi pesa yoyote ya maana " nilimwambia.
"Usijali kaka, Usiwe na wasiwasi,"
Ezekiel alikuwa akichukulia hii issue simple sana...
Nakumbuka wakati Ezekiel ananipelek mgodini alinikabidhi kwa wajeda fulani wanielekeze kazi, nilifanya nao kazi baada ya kuzoea nikawakataa kwa tabia zao maana nilijua wangeniambukiza...
Wale jamaa walikuwa wanapata sana pesa na kwenda bar kulewa na kufanyia ngono wananunua wanawake wanaojiuza...
Yaani ni pesa kama milioni moja wakipata wanafyeka siku moja tu...
Mmoja alikuwa anaitwa John, Peter, na Michael. Walikuwa wakipata pesa ni kula Maisha haswaa...
Ikabidi niwacheck wanipe mchongo wa namna ya kuuza na kununua dhahabu...
Wakanipa mchongo mzima...
Nikachukua ile milioni tano, Milioni tatu nikanunua boda boda mpya na kumkabidhi bro mmoja nilijuana nae akawa ananipa elfu kumi kwa siku...
Ile milioni mbili nikawekeza kwenye biashara ya kuuza na kununua dhahabu...
Nikawa nanunua kwa wachimbaji wadogo wadogo naenda kahama mjini kuuza napata faida kubwa tu...
Maisha yakakubali nikapata pesa tena nikaongeza boda boda mpya nyingine mbili jumla zikawa tatu...
******
Siku zikasonga na nikawa nishamdelete Sophie kwenye Maisha yangu kwa alichonifanyia...
Alex yeye kama kawa nilikuwa namcheck lakini sikuwaambia niko wapi...
Siku moja, nilipokea email kutoka kwa Sophie.
"Marchey mambo vip, unaendeleaje Vp hali yako?"
Nikamjibu
"Nipo vizuri, Sophie. Vipi huko?"
"Me naendelea vizuri. Lakini me nimechanganyikiwa, mwanaume ambae nilimpenda sana na kumkabidhi maisha yangu yote, Hassan nimemfumania akiwa na mwanamke mwingine na tayari huyo mwanamke ana ujauzito wake," Sophie alisema na kunitumia picha za huyo mwanamke...
Moyoni nikasema Kula chuma iyo 😂...
Nikamjibu kwa dharau
"Pole, Kuwa mke wa pili maana mwenzio kakuwahi kushika ujauzito"
Akajibu
"Marchey, naelewa jinsi gani nilikukosea, lakini ilikuwa ngumu sana kwa mwanaume ambaye nilimpenda," alisema Sophie.
Nikajibu tena,
"Naelewa, ndio maana nimekwambia Pole,"
Akajibu
"Asante kwa kunielewa," alisema Sophie na sikujibu chochote maana alinionyesha dharau sana...
#A Message from Bad girl Grace
Utafikiri nilikuwa na gundu... Na nilihisi huenda Grace na Sophie wanashirikiana...
Kesho yake Nilipokea email nyingine kutoka kwa Grace. Ikiwa na Picha ya mkuu wa magaidi akiwa maiti tayari...
"Grace, umefanya nini?" nilimuuliza kupitia email.
"Nililipa viajana pesa waue hiyo paka... Paka ilikuwa na maneno machafu utafikiri imenizaa... nikaona bora ikakutane na Master Go wakuandalie chumba chako huko kuzimu ili ukifika upate pa kulala" Grace alijibu.
"Grace wewe ni mnyama sana, sijui una roho gani we mwanamke" nilisema.
"Sasa sijui nikufate huko huko uliko, au nikuchonganishe tu wakuue huko huko," alisema Grace.
"We unajua me niko wapi?," nilimuuliza kwa uoga.
"Najua, Marchey. Mimi nina akili kuliko wewe, yaani wewe ulipoishia mimi ndio naanzia hapo," alisema Grace na kunifanya niogope sana... Kisha sikujibu chochote nisije kuharibu mambo...
Nikawa naogopa sana na nikachanganyikiwa nikauza boda boda mbili kwa milioni 5...
Nikaongeza milioni mbili jumla zikawa saba nikamcheck Grace na kumuomba nimrudishie...
Alikubali na nikamtumia Milioni 7 na laki 5 lakini hakunijibu chochote kila nikituma ujumbe...
Nikaendelea kumuuliza kama pesa imefika na baada ya week moja akanijibu...
"Pesa imefika acha kujichoresha mtoto wa kiume"
Na mimi nilikasirika sikujibu kitu...
********
Matatizo yakaanza tena bhana...
Baada ya siku mbili tu, Sophie aliniandikia email nyingine.
"Marchey, nimeachana na Hassan. Siwezi kuvumilia tena," aliandika.
"Sawa," nilimjibu kifupi tu.
"Asante. Najua nitakuwa sawa," alisema Sophie.
"Sijui, hayo ni mawazo yako," nilisema.
"Asante kwa ushauri wako," alisema Sophie.
"Nimekushauri nini hapo?" Nilijibu
"Si umenijibu au?" Alijibu Sophie
Mimi: " Sophie haya yote uliyataka wewe... Sometime mimi napatwa na hasira... Unaponishirikisha masuala yako ya mahusiano unanikosea, na unajua kabisa na mimi niliwahi kuomba nafasi kwako, lengo lako ni kuniua sindio?"
Sophie: "Samahani Sana Marchey, nisamehe bure... Nataka nirudi kuwa sophie wa Zamani, ila sasa nisamehe tu"
Mimi: " Nimekusamehe, una kitu kingine labda?"
Sophie: "Marchey mimi sasa nimeamua kubadilika na niko serious na kazi sasa... Nimeamua kuacha yote na kama bado una hisia na mimi basi utanisamehe sitaki tena mwanaume "
Marchey: "nimekwambia nakutaka? Au ndio unafikiri nitakutaka tena? Sahau kabisa na ufute Kwenye akili yako, alafu kingine mimi saivi nishabadili mfumo wa maisha, we dili na kazi yako kama ulivyosema kama kusalimiana tutakuwa tunasalimiana"
Sophie:"Lakini Marchey mbona kama hujanisamehe?"
Na mimi sikumjibu tena na alituma email nyingi sana...
Sio kwamba nilikuwa sina hisia nae, ila ni vile tu nilikuwa najibu kwa hasira ukizingatia nimepigwa milioni 7 na bad girl 😂
Baada ya week moja Sophie akatuka tena ujumbe
"Marchey, naomba msamaha kwa yote yaliyotokea. Grace alinitishia," aliandika Sophie kwa ufupi sana...
Basi siku hii nikaamua kumjibu
"Sophie, nimesamehe yote. Ila Ni vizuri nikwambie ukweli kuwa wewe endelea na maisha yako, lakini hatuwezi tena kukutana,"
Akajibu "Unaniumiza sana Marchey"
Kidume nikavunga tena kutomjibu😂
********
#Alex Augua
Nilipokea taarifa kuwa Alex alikuwa amelazwa hospitalini. Sophie ndiye aliyekuwa akimuuguza.
Ikabidi nimcheck Sophie
"Sophie, vipi hali ya Alex? Nimeskia anaumwa" nilimuuliza kupitia simu.
"Marchey, hali yake ni mbaya. Tumbo linauma sana, na kuna uwezekano akafanyiwa upasuaji kwa maelezo ya daktari" alisema Sophie.
Basi nikawa natuma pesa kidogo za matibabu kila ikihitajika...
"Asante sana, Marchey, natamani sana tungeishi wote hivi kumuuguza rafiki yetu" alisema Sophie.
"Hakuna shida. Nitafanya kila liwezekanalo, lakini mimi kufika huko kuja kumuona tutakuwa tunasalimiana tu" nilisema.
"Uko mbali, lakini umefanya mengi kunisaidia mimi na Alex, hivi kwani uko wapi Marchey?" alisema Sophie.
"Niko Sehemu salama, hakikisha alex anakula vizuri, nitakucheck baadae" nilimwambia kisha nikaendelea na shughuli zangu...
#Najisukia bomu hatari
Siku moja Nikiwa Kahama kufanya biashara ya dhahabu, nikasema niende nyumbani kwa eze kumsalimia japo hata shemeji, nimefika pale naambiwa Ezekiel (eze) hayupo kasafiri na boss wake wameenda China kuna wachina walikuwa wakifanya kazi na boss wake...
Basi nimekaa pale napiga stori na shemeji alikuwa kanizoea kidogo na anaona ka aibu kwa mbali...
Nakumbuka ilikuwa saa kumi na mbili jioni nataka niondoke nikatafute lodge nilipie nilale alafu kesho yake asubuhi niondoke kurudi mgodini...
Shem akaniomba japo nioge na anasema kaagiza msosi apike kwa ajili yangu japo nile ndio niondoke...
Niligoma goma pale badae nikalainika bhana... Akaniandalia maji pale nikaenda kuoga...
Sasa bhan maji si nilichemshiwa utafikiri mimi ndio mume...
Natoka kuoga hivi ananiambia nikae sebuleni kusubiri msosi...
Shem alikuwa peke yake hakuwa na mtoto...
Akaandaa msosi pale mezani tukaanza kula...
Sasa mimi nikiwa nakula nashangaa mwenzangu anakula huku akinichungulia kwa siri ninavyokula...
Baadae akawa hana aibu tena ananiangalia machoni na mimi nikikutana machoni naona aibu wote tunaangalia chini... Wakati huo ka taarifa ka habari ITV kanaendelea saa mbili usiku...
Bana eeeh shetani akanivaa... Nikawa nawaza siendi kutafuta lodge nalala hapa hapa...
Mara akaniuliza...
Shem: "kwani shem lazima ukatafute lodge, hiyo hela si utunze tu utalala hapa hapa kesho utaondoka au"
Marchey: "Hapana shem nitaenda kulala lodge wala usijali" lakini moyoni nasema aendelee kunibembeleza...
Shem alikuwa pisikali moja figure ya maana ila sio kubwa saaana...
Shem :" aaah Lakini nilitaka ubaki tu ulale kile chumba maana si unajua nyumba nzima kulala mwenyewe tena mtoto wa kike naogopa..."
Marchey: " Mmmh kwani siku nyingine huwa unawezaje kulala?"
Shem:"Ni kwa sababu leo tumeongea kwa muda mrefu ko nimezoea nikilala mwenyewe nyumba yote hii leo nitaota ndoto mbaya na huenda nisilale kabisa"
Wakati huo akili yangu isha lose control...
Si nikaropoka...
Marchey: " basi poa usijali me nitalala"
Shem:"kweli Shem... Shem... Sawa nashukuru sana... Tutaangalia TV leo wote mpaka saa 6 kwa kuwa upo... Au haupendi movie?"
Marchey: "Napenda kiasi, tutaangalia usijali..."
Kilichoendelea ni tofauti kabisa......
Movie yenyewe sikuangalia hata nusu saa.....
Siku hiyo sikulala huko kahama kwa shemeji, badala yake nililala mgodini kule kijijini.....
Nilijikuta nikiingia katika mahusiano ya siri na Shem mke wa Ezekiel, aliyeitwa Linda.
######