Nilipokuwa mdogo nilijua hivi

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3,996
Reaction score
5,156
Nilipokuwa mdogo nilijua duka likifungwa mtu anashusha vitu vyote kwenye shelves anaweka chini.

Nilipokuwa mdogo nilijua TV ikiwa inaongea ikatokea umeme umekatika inaendelea palepale ilipoishia

Ulipokuwa mdogo ulijua nini?
 
1.Kuna baba mdogo wangu ni mwalimu.Siku amekuja kitusabahi nilimshangaa sana kuona anapanda daladala.
Nilijua walimu ni watu wenye pesa na heshima kubwa sana kiasi kwamba hawatakiwi kutembea kwa mguu au kutumia usafiri wa umma!

2.Nilijua mama hawezi kuwa na mwanume mwingine mpaka baba tu!

3.Ukienda chuo kikuu unajua kila kitu na huwezi kukosa kazi serikalini.

4.Wanaofanya kazi serikalini wote ni wanajeshi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…