Nilisema napita ,ila sasa nimezama

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Nilisema napita

1. Ninapenda anunavyo, hima kumbembeleza
Hasira za hovyo hovyo, jikoni nikimtweza
Nilivyomuwaza sivyo, hakika ameniweza
Nilisema ninapita, ila sasa nimezama

2. Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakamani
Ana yake mahabusu, kutoka siitamani
Jioni Alkasusu , aninywesha muhibani
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama

3. Sijaomba ananipa ,bila pupa najiliya
Mihogo chuzi la papa, viungo anijaziya
Kiwanja kama Mkapa, ma goli twashangiliya
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama

4. Pendo amenigandisha, digrii amezihitimu
Shingo akiizungusha , aah anipa wazimu
Pindi akilifundisha , haumalizi utamu
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama

Abuuabdillah ✍️
0744883353
 
Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakamani
Ana yake mahabusu, kutoka siitamani
Jioni Alkasusu , aninywesha muhibani
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
Usikute kuna vijana watatamani hii verse ingekua hivi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚...

Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakani
Ana yake mahabusu, kutoka sitamani
Nikiichakata mbususu, utamu hadi kichohoni
Nikisema napita, ila sasa nimezama.
 
Jikimwi atakupea, kisonono kitakuelemea!.
Shipa litakumea, komwe litakulegea!
si ulisema utapita, jikimwi amekupea!
😹😹 Kenzy una ufallah mwingi
 
Usikute kuna vijana watatamani hii verse ingekua hivi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚...

Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakani
Ana yake mahabusu, kutoka sitamani
Nikiichakata mbususu, utamu hadi kichohoni
Nikisema napita, ila sasa nimezama.
hahahah
 
Mkuu nakuona kwanza umefeli/
Hiyo mistari labda ujaribu beat ya singeli/
Umeshikwa pabaya kigoma mwisho reli/
Unatapa tapa mithili ya kuku mwenye kideri/
 
Mimi nimeambulia "Kiwanja kama Mkapa, ma goli twashangiliya". Sasa kweli kwa mdebwedo huo utamu utautoa wapi! Huyo atakuwa single mother au kahaba! Chai!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…