Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 893
- 1,021
Nilisema napita
1. Ninapenda anunavyo, hima kumbembeleza
Hasira za hovyo hovyo, jikoni nikimtweza
Nilivyomuwaza sivyo, hakika ameniweza
Nilisema ninapita, ila sasa nimezama
2. Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakamani
Ana yake mahabusu, kutoka siitamani
Jioni Alkasusu , aninywesha muhibani
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
3. Sijaomba ananipa ,bila pupa najiliya
Mihogo chuzi la papa, viungo anijaziya
Kiwanja kama Mkapa, ma goli twashangiliya
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
4. Pendo amenigandisha, digrii amezihitimu
Shingo akiizungusha , aah anipa wazimu
Pindi akilifundisha , haumalizi utamu
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
Abuuabdillah ✍️
0744883353
1. Ninapenda anunavyo, hima kumbembeleza
Hasira za hovyo hovyo, jikoni nikimtweza
Nilivyomuwaza sivyo, hakika ameniweza
Nilisema ninapita, ila sasa nimezama
2. Komwe nisipo libusu, ni kesi mahakamani
Ana yake mahabusu, kutoka siitamani
Jioni Alkasusu , aninywesha muhibani
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
3. Sijaomba ananipa ,bila pupa najiliya
Mihogo chuzi la papa, viungo anijaziya
Kiwanja kama Mkapa, ma goli twashangiliya
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
4. Pendo amenigandisha, digrii amezihitimu
Shingo akiizungusha , aah anipa wazimu
Pindi akilifundisha , haumalizi utamu
Nilisema ninapita , ila sasa nimezama
Abuuabdillah ✍️
0744883353