Nilishindwa kulala usiku baada ya kusoma 'Sheria mpya ya Usalama wa Taifa'. Nimeumia sana kama mwananchi wa kawaida

Sheria haifai kama ni kweli
Yaani mtu anaweza kukuua tu kwa wivu wa mapenzi kwa mfano,halafu aka fabricate ulikuwa unahatarisha usalama wa taifa na hawezi kushitakiwa kwa mauaji?
Ni hatari sana hii
Sio kuuwa tu hata akawa tishio na mali yako pia.
 
Mmh hatari sana. Na hivi bungeni wako wao tu nikujipigia tu. Anyway, wao waemdelee hakuna jinsi.
 
Sheria hii inakuja nyakati ambazo kuna malalamiko kuwa usalama wa Taifa hawapo competent kwa maslahi mapana ya Taifa wana bias zaidi kulinda chama tawala.

Wengine husema ni Usalama wa CCM sio usalama wa Taifa kama watu wasemavyo ni Polisi CCM na sio Polisi Tanzania
 
Sheria mpya ya Usalama wa Taifa', Kwanini Wabunge wapishe kama haifai?
Waikatae tu
 
Na hiyo ndiyo democrasia yetu 😅😅😅
 
Hata huu uzi watu huogopa kuchangia kwa kuhofia usalama wa Taifa. Dah....!
 
Duh kweli kabisa tunakoelekea Mungu ndo anajua alafu hii sheria imempa mamlaka mengi DG Eti ata ikuingia kwenye majengo Yao ni kosa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mada zingine bora nikae kimya tu kuliko nijifanye mjuaji kumbe sijui sheria wala lolote juu ya usalama wa taifa hili.
Wajuzi/wajuvi tuleteeni ufafanuzi tujifunze.
 
Mtoa mada Angeweka na link ya hiyo sheria ingekua POA Sana Yaan[emoji4]
 
Kwa hiyo nisifanye mambo yangu ya msingi kisa nawaogopa wasioogopeka
Ntakutanana nao wapi kwanza

Halafu kama wameajiri watoto wa vigogo au wakubwa unafikiri watakuja kukaa kwenye local bar kusikiliza mlevi anashangilia badala awe kwenye kumbi zenye hadhi huku akijirusha au hata hapa karibu Paris tu

Hakuna taharuki itakayotupata ila ni mauza uza yako tu Mkuu
Ishi maisha ya furaha bila kufuatilia ya watu
 
Asante kwa kutujuza kinachoendelea.

Kwa Kweli Kama ni kweli itakuwa mtihani mkubwa!
 
Mbona nakumbuka huwa inasemwa kuwa “ hakuna mtu aliye juu ya sheria” ?

Au maana yake ni nini?
 
Wengi wanajidanganya kwamba kwenye Siasa hakuna masuala ya Mungu ! Yaani hapo Mungu hagusi !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…