mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Umeonaeee !Hata huu uzi watu huogopa kuchangia kwa kuhofia usalama wa Taifa. Dah....!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeonaeee !Hata huu uzi watu huogopa kuchangia kwa kuhofia usalama wa Taifa. Dah....!
Kiongozi hao wa5 wanaounda deep state ya nchi hii unawafahamu utuwekee majina yao hapaSio hii. Deep state nawafahamu. Ni kikundi cha watu hata hawazidi 5 wakifika 10 wengine ni bosheni tu sio kundi kubwa kiasi hiki
Ni makada wa CCM woteKwa nchi za wenzetu.. Vitengo vya usalama kidogo wana utu.. Kisha hata wakifanya kazi za hatari ikiwepo kueliminate mtu kunakuwa na mashiko..
Shida ni kwetu siasa ni nyingi...
Atakuja kuondolewa mtu wa kisiasa na sababu zisizo na kichwa wala miguu...
Raia wajiandae.. Yaani unapotezwa kiintelegensia.. Majibu yanatoka kwa usalama wa nchi... Afisa aliyehusika analindwa kisheria..
Wengi wa maafisa hawa wapo kichama na kishabiki na sio weledi wa kazi... Wataumiza watu wengi... Tusubiri
Watu walikuwa busy kueleza mabaya ya dikteta Jiwe kwa madai ya kwamba viongozi waliyopo sasa wajifunze wasirudie tena makosa kama ya Jiwe, ila kinachoendelea ni wazi viongozi waliyopo hakuna walicho jifunza.Mlisema jiwe ni DIKTETA sio!
Kula chuma hicho.
Hapa kuna shida kubwa ya kiungozi katika taifa letu. hii mbegu inayopandwa sasa kuna siku huko mbeleni tutaivuna wote pamoja kwa madhara sawa, na hao wanaodhani watakuwa salama baada ya kutungwa kwa sheria hizi. ikumbukwe hata Rwanda na Burundi hapo mwanzo mambo yalikuwa hivi hivi yaani kundi moja la watu kuona lina haki zaidi katika Taifa kuliko wengine na kujitungia sheria kedekede za kujilinda na hata ikibidi kuzima uhai wa wengine ili kubaki madarakani, lakini mwisho siku maangamizi yakatokea ambapo kila upande ulipoteza watu wengi kutokana na kuchukulia mambo for granted kama yanayoendelea hapa kwetu sasa hivi. Kuna watu wanadhani hii nchi ni ya kwao na kwamba pasipo wao kuwa madarakani bora nchi iwake moto. Kuna siku hizi sheria zitashindwa kuwalinda hata hao waliyozitunga na kuzibariki zitumike.Nimeona kama wasiojulikana wamewekwa rasmi kwenye mfumo wa kiutawala.
Kwanini?
Kwa sababu hakuna anayewafahamu maafisa usalama wa Taifa kwa uwazi. Wapo kwa kificho zaidi kama wasiojulikana. Hakuna anayefahamu mipaka ya maafisa wa usalama wa Taifa. Haijulikani wanaanzia wapi na kuishia wapi mipaka yao kimajukumu.
Mwekezaji mzawa ama wa kudumu anawezaje kuwekeza kwenye Nchi ambayo kuna mamlaka makubwa yasiyojulikana juu ya hatma yake kibiashara ama kimaisha ama uhai wake? Ni ngumu sana.
Wakuu, nimeogopa hili Taifa kuliko kawaida. Ni Taifa langu la kuzaliwa. Lakini siwezi tena kujivunia. Naogopa. Nadhani, busara ni kufanya utaratibu wa kuhamia Burundi, kule huenda kuna unafuu zaidi kuliko Tanzania.
Hawa huwezi kukabiliana nao kwa lolote lile. Utahatarisha maisha yako bila sababu. Wana mamlaka makubwa kuzidi hata ya Rais mwenyewe. Watakufanya lolote lile watakalo na huna la kuwafanya. Yaani, kitakachokuokoa ukijichanganya ni Mwenyenzi Mungu pekee ama huruma za tu za kibinadamu na si vinginevyo.
Unaweza tena kugombania nao demu? Thubutu.
Unaweza tena kujimbwafai ukiwa bar ukisema hii ni nchi yetu wote, usinitishe? Thubutu.
Unaweza tena kubishana Yanga na Simba kijiweni? Thubutu.
Unaweza tena kubishana ishu za Chadema na CCM kijiweni? Thubutu.
Nikiwa kama kiongozi wa Umma, kwa mfano: Kwa nini nisihakikishe mwanangu anaingia usalama wa Taifa ili apate kinga ya kudumu?
Hata hivyo, inasemekana mtaani waliojaa usalama wa Taifa ni watoto wa wakubwa. Inasemekana.
Je, huenda wakubwa na familia zao wameamua kujiwekea kinga za kudumu kwenye Taifa hili? Mungu anayajua. Itakubidi, uishi kwa kujikunyata maana hujui nani ni nani na anatekeleza majukumu yapi ya usalama wa Taifa.
Pamoja na hayo, kama Baraza la Mawaziri wameona sheria hiyo ipo kamili basi tena na iwe kama watakavyo. Kila mwananchi aangalie namna ya kujihami.
Huenda ni hofu yangu kwa kuwa sijaelewa vizuri sheria yenyewe. Kama hivyo, basi na uzi huu uondolewe isilete taharuki kwa wengine wasioelewa kama mimi.
"Unapowekewa kinga ya kutoshitakiwa ni kama vile umeambiwa fanya makosa kwa kadri uwezavyo ili mradi unafanya kwenye line ya majukumu yako kikazi. Ni kama vile umeondolewa umakini wako kazini........yaani ni sawa na kama umeambiwa huna sababu ya kuwa makini kazini kwako kwa sababu hata ukikosea hakuna kitu utafanywa maana ni makosa kazini".
Eeehhh Mungu Baba ingilia kati Taifa hili.
Naomba kuwasilisha!
Pia soma: Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya usimamizi wa Rais watua Bungeni
Tatizo lipo hapo, ni vipi tutajua hakua kwenye majukumu yake?Sheria haifai kama ni kweli
Yaani mtu anaweza kukuua tu kwa wivu wa mapenzi kwa mfano,halafu aka fabricate ulikuwa unahatarisha usalama wa taifa na hawezi kushitakiwa kwa mauaji?
Ni hatari sana hii
Polisi gani wana kinga ya kushtakiwa?Huu mswada hautapitishwa na wala hautasomwa Bungeni.
Ni sawa na ule ambao uliwapa Polisi kinga ya kutoshtakiwa