Nilishindwa kumsaidia Mariamu

Nilishindwa kumsaidia Mariamu

Mwaka jana tulimpoteza Staff mwenzetu kwa ajali ya pikipiki pale JNIA, aligongwa na gari akiwa kwenye pikipiki akirudi Nyumbani kwake. Siku hio ya Ijumaa aliniita na kuniambia kuwa kuna jambo anataka kuniambia, lakini nilikua busy kidogo nikakwambia naomba tuongee Baadae Tukitoka. Dah, dakika arobaini Baadae tunapigiwa simu kuwa amefariki dunia, nakumbuka I was the first kufika Amana kuutambua mwili.

Matukio haya mawili la mleta Mada na hili la kwangu limenifundisha kuwapa muda wenzetu, rafiki zetu na jamaa zetu. Kama ningeenda nikamsikiliza tukapiga story mbili tatu Huenda angechelewa kuondoka kidogo na kuchelewa eneo la Kifo chake.

Mpe muda rafiki yako, tusijipende wenyewe kupitiliza Sana.
yah, upo sahihi kabisa mkuu
 
inasikitisha sana, ila ndo maisha tutafanya nini zaidi ya kumuombea huko alipo.
 
Rafiki na ndugu yangu mpendwa,

Nilikuja nyumbani kwenu kama tulivyohaidiana ili nipate kukuaga lakini kwa bahati mbaya nimekukosa, nilikuja kukuaga kwa kuwa hutaniona tena kwani nasafiri safari ya mbali sana. Baada ya kusubiri sana nimeamua kurejea nyumbani na ili kufanikisha safari yangu, wakati nakuja kwenu nilipitia maduka kadhaa ya dawa na kununua vidonge vya klorokwini vipatavyo 40 , naamini vidonge hivyo vitafanikisha safari yangu kwa amani ili nipate kupumzika .

Naogopa na nahitaji mtu wa kuzungumza nae lakini simuoni,kwani nipo katika ulimwengu wa peke yangu na mbele yangu kuna giza nene , sijui msaada wangu utatoka wapi? Kaka yangu mpendwa, wewe ndio rafiki yangu uliye kuwa karibu na mimi wakati wote , ukinipa moyo wa kuzikabili changamoto za maisha , lakini sasa naona imefika tamati, sina budi kurejea kwa mola wangu. Najua ni dhambi kwa mwanadamu kukatisha uhai wake kikatili namna hii, kama ulivyowahi kunisomea maandiko matakatifu katika biblia lakini kwa suala langu naamini hii ndio njia muafaka , naomba Mungu anisamehe.

Naomba unisamehe kwa kukusababishia maumivu moyoni kwa kuondoka kwangu ghafla katika uso wa hii dunia, lakini sababu kubwa iliyosababisha hili litokee nadhani unaifahamu. Nasema unaifahamu kwa sababu umekua karibu na mimi kwa muda mrefu tangu tulipokutana sekondari tukiwa kidato cha kwanza mpaka tulipomaliza kidato cha nne.

Ulikuwa ni zaidi ya rafiki na ulitumia muda wako mwingi ukinifariji na kunipa moyo hasa baada ya lile jaribio la kutaka kujiuwa la 2013 wakati tukiwa kidato cha tatu kushindikana. Ingawa naogopa, lakini nadhani hii ndio njia sahihi ili kuepuka haya maisha ninayoishi, maisha ya upweke niliokua nayo, hakuna hata mmoja miongoni mwa ndugu zangu aliyekuwa karibu pale nilipohitaji msaada zaidi yako wewe , hakuna aliyewahi kunifuta machozi pale nilipokuwa nahitaji msaada zaidi yako wewe na kibaya zaidi hakuna hata aliyewahi kusikia kilio changuzaidi yako wewe.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikipiga makelele ya kuomba msaada lakini sauti yangu imekuwa ikiishia mwituni, hakuna anayejali, na sasa nimeamua , ngoja niondoke labda watafurahi , maana wataishi kwa amani . Naamini hata kushindwa kwangu kuendelea na kidato cha tano ilichangiwa zaidi na matatizo ya kifamilia niliyokuwa nayo ambayo unayafahamu.

Kaka yangu na rafiki yangu mpendwa tangu tulipoachana mara baada ya kumaliza kidato cha nne na wewe kupangiwa kuendelea kidato cha tano mkoani Dar es salaam, uliniacha na upweke mkubwa nisijue pa kukimbilia ili kupata faraja . Kwani mateso yalizidi mno hapa nyumbani nilishindwa kujua mustakabali wa maisha yangu ya baadae na hakuna aliyeonesha kujali.

Nashukuru sana kwa misaada uliyonipa wewe binafsi na ile niliyowahi kupewa na wazazi wako, naomba ufikishe shukrani zangu na waambie kwamba nawapenda sana. Naomba usinililie, na amini kuwa naondoka hapa duniani nikiwa nakupenda sana , na kwangu utaendelea kubaki ndugu na rafiki yangu mpendwa. Nakutakia maisha mema hapa duniani na baki salama

Ni mimi rafiki yako na mdogo wako,

Mariamu;

Jana tar.22 imetimia miaka mitatu tangu rafiki yangu huyu roho yake iachane na mwili , baada ya kuamua kukatisha maisha yake. Alikuwa bado ni binti mbichi ambapo ndio kwanza alikuwa ametimiza miaka 20 , lakini kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa kwa mama yake wa kambo akishirikiana na baba yake mzazi aliamua kukatisha uhai wake.

Kwangu mimi huu ulikuwa ni msiba mkubwa kwani alikuwa ni zaidi ya rafiki.Nakumbuka ndio nilikuwa nimerudi kutoka Dar kuja kufanikisha mipango ya kuhamia katika moja ya shule binafsi iliyoko hapa mjini Morogoro.Siku mbili kabla ya rafiki yangu huyu kuutoa uhai wake kwa bahati nilikutana naye sokoni lakini akiwa anaonekana kuwa mnyonge na asiye na furaha , alikuwa amefuatana na binti mmoja ambaye alinitambulisha kuwa ni mdogo wake.

Alinivuta pembeni na kuniambia ni bora tumeonana kwani anayo mazungumzo marefu na mimi hivyo alitaka kujua ratiba yangu ili aje nyumbani tuongee . Nilimwambia aje nyumbani siku mbili baadae yaani ijumaa ya tarehe 20 ambayo ndiyo nitakuwa na nafasi ili tuongee , lakini kwa bahati mbaya siku hiyo nilikwenda Dar kupeleka form flani kule shuleni nilikokuwa nasoma na ili nirudi siku hiyohiyo.

Hivyo ilipofika siku hiyo kabla sijaondoka kuelekea stendi ya Msamvu kupanda basi kuelekea Dar niliacha maagizo kwa mama kuwa rafiki yangu huyo akija anisubiri . Ni kweli alifika pale majira ya saa nne asubuhi hivi na na baada ya kuambiwa nimeenda Dar , alikosa raha, hata hivyo mama alimshauri anisubiri kwani nitawahi siku hiyohiyo. Kwa mujibu wa maelezo ya mama yangu, alikuwa akiuliza mara kwa mara kama nitarudi saa ngapi, mpaka mama yangu akawa na wasiwasi , ikabidi amuulize kama anashida kubwa na mimi , ndipo akamjibu mama yangu amekuja kuaga kwani anasafiri na hivyo ameona ni vyema aje kwangu kuniaga mimi rafiki yake.

Mama yangu akamthibitishia kwamba ningerudi mapema siku hiyohiyo. Mpaka kufika saa nane mchana nilikuwa bado sijarudi , akaomba apewe karatasi na kalamu ili aniachie ujumbe . Alipoletewa ndipo akaniachia huo ujumbe niliouandika hapo juu. Nakumbuka nilirudi Morogoro majira ya saa kumi na mbili jioni kwani siku hiyo usafiri kutoka dar huko shuleni nilikokuwa nikisoma mpaka stendi mjini ulikuwa ni mgumu kidogo.

Nilipofika nyumbani mama alinipa ile barua aliyoniachia rafiki yangu, na nilipoifungua na kuisoma sikuamini kile kilichoandikwa katika barua ile , nilishitukia napiga yowe kubwa, hadi mama akashituka . Niliongozana na mama hadi manzese alipokuwa akiishi, huyo rafiki yangu, tulifika pale majira ya saa mbili usiku , na tulikutana na umati mkubwa wa watu.Ni kweli rafiki yangu amekufa! Nilishikwa na butwaa.

Basi hivyo ndivyo alivyojitoa uhai rafiki yangu huyo. Msiba huo ulibaki kuwa kumbukumbu katika maisha yangu ,kwa binti mdogo kiasi kile kujitoa uhai uhai mapema namna ile . Kwa kifupi nilifahamiana na mariamu nilipojiunga kidato cha kwanza , baada ya kufaulu darasa la saba. Tulitokea kuwa marafiki na nilimpeleka nyumbani na kumtambulisha kwa wazazi wangu, na kutokana na kuniamini ndipo akanisimulia madhila aliyokuwa nayo .

Mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka mitano na anasemekana mama yake alifariki kutokana na Depression(kwa kitaalam) baada ya kuwa ameteswa sana na mumewe yaani baba yake.Mara baada ya mama yake kufariki , baba yake akaoa mke mwingine ambaye anasemekana kuwa ndiye aliyekuwa akimzuzua baba yake mpaka kufika kumtesa mama yake. Huyo mama yake wa kambo alikuwa akimtesa sana kwani aligeuzwa kuwa mtumishi wa ndani pale nyumbani kwao na baba yake hakuonekana kujali sana kwani kwa kushirikiana na baba yake walikuwa wakimtesa na kumsimanga kuwa atakuwa Malaya kama mama yake, kitu ambacho si kweli kwani hakuwai kuwa na uhusianona wanaume kama walivyokuwa wakimtuhumu.

Pamoja na mateso yote hayo lakini alijibidisha na masomo hadi akafaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule ya serikali , kitu ambacho hakikumfurahisha mama yake wa kambo . Kuanzia hapo mateso yalizidi na baba yake kwa kawaida hakuonekana kujali.

Nakumbuka nilimsaidia sana katika kumfariji na kumpa moyo na hata pale baba yake alipokataa kumpa pesa za matumizi ya shuleni na mahitaji mengine , mama yangu alimpatia hiyo ni baadda ya kuwa nimemsimulia mama yangu juu ya mateso anayoyapata rafiki yangu huyo.

Hata nilipokuwa nikienda kwao kumtembelea mama yake hakuonekana kufurahia na muda mwingi alionekana kufokafoka bila sababu ya msingi . Kuna wakati mama yangu alimshauri ahamie kwetu ili kuepukana na mateso yale lakini alikataa katakata kwa madai kuwa baba yake atamuua. Habari za huyu binti ni ndefu sana na nikisema nisimulie nadhani nitawachosha .Hata hivyo bado ninayo maswali mengi sana juu ya lile tukio.

Hivi kama ningewahi kurudi si labda ningeweza kuokoa maisha ya rafiki rafiki yangu huyu? AU kuchelewa kwangu kulikuwa ni makusudi maalumu ili hili tukio rafiki yangu kujiua litokee ?

Apumzike kwa amani na mwanga wa wa milele umwangazie EE Bwana….Ameen!..
Inasikitisha sana pole brother na apumzike kwa amani mdogo wetu. Watoto/wadogo zetu wengi wanapitia katika hali kama hii tumuombe Mungu sana atupe mioyo ya kujali shida na mapito ya wenzetu na tuwasaidie kwa kadri Mungu atakavyotuwezesha kwani tkifanya hivyo hata Malaika Mbinguni watafurahi na kushangilia
 
Inasikitisha sana pole brother na apumzike kwa amani mdogo wetu. Watoto/wadogo zetu wengi wanapitia katika hali kama hii tumuombe Mungu sana atupe mioyo ya kujali shida na mapito ya wenzetu na tuwasaidie kwa kadri Mungu atakavyotuwezesha kwani tkifanya hivyo hata Malaika Mbinguni watafurahi na kushangilia
well said blood
 
Story ya kutunga. Zunguka Tanzania nzima hakunaga vidonge vya Chroloquine madukani.
 
Inasikitisha sana ila maisha yanachangamoto nyingi sana kiukweli
 
yaani marehemu aliogoma kuhamia kwa rafiki yake kwasababu alihofia baba yake atamuua then baada ya mateso kuzidi akaona bora ajiue .....kiukweli sijamuelewa kabisa marehemu.
 
Back
Top Bottom