Nilishiriki mapokezi ya ndege boeing 737 - MAX 9

Joined
Apr 11, 2024
Posts
24
Reaction score
55
Nilifanikiwa Kushiriki Kwenye Mapokezi Ya Ndege Mpya (Boeing 737 - Max 9) Ya Shirika La Air Tanzania (Air Tanzania Company Limited) Ambapo Mgeni Rasmi Katika Mapokezi Hayo Alikuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaaliwa, Kwa Niaba Ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kutokana na Mheshimiwa Rais Kutingwa na Majukumu.

Katika Mapokezi Haya, Mheshimiwa Waziri Mkuu Aliweza Kumpongeza Mheshimiwa Rais Kwa Juhudi Anazozifanya, Hususani Ndani Ya Miaka Hii Mitatu, Kwa Kuimarisha Sekta Mbalimbali Ikiwemo Sekta Ya Uchukuzi, Na Kutekeleza Ilani Ya Uchaguzi Ya Chama Cha Mapinduzi Ya Mwaka 2020-2025.

Pia Mheshimiwa Waziri Mkuu, Aliweza Kutujuza Mafanikio, na Umuhimu wa Sekta Ya Uchukuzi Nchini Kwa Maendeleo Ya Taifa Letu, Ikiwa Ni Pamoja Na, Kuwa Mchango Katika Kuhakikisha Ukuaji wa Uchumi Wetu Na Kuzalisha Ajira Nchini. Kuongeza Uwezo wa Taifa Kujitegemea Kiuchumi. Kuchochea Uzalishaji, na Kutumia Vyema Fursa za Rasilimali Zilizopo Hapa Nchini. Kuchochea Upatikanaji wa Fedha za Kigeni, Nchini. Na Ongezeko La Mnyororo wa Thamani Ya Mazao Ya Kilimo, Pamoja na Biashara, Na Kadhalika.

Lakini Pia Ameweza Kusema Ndege Ambazo Zimenunuliwa Kwa Kipindi Cha Miaka Mitatu Ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ambapo Tayari Ndege Tano Zimeshawasili Ikiwemo Ndege Ya Mizigo, Ndege Ya Sita Ikiwa Ni Boeing 737-9 Max Iliyowasili Leo, Na Ndege Nyingine Moja (Boeing 787-8 Dreamliner) Ambayo Inategemewa Kuwasili Hivi Karibuni.

Na Mpaka Sasa. Kuna Endelea Na Maboresho Ya Viwanja Vya Ndege Kwenye Mikoa Mbalimbali. Kubwa Zaidi Ni Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Msalato - Dodoma, Pamoja na Uboreshwaji wa Uwanja wa Pili wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere, Utaosaidia Kuifanya Tanzania Kuwa Kitovu Cha Anga, Afrika Mashariki.

Lakini Pia, Aligusia Mafanikio Ya Sekta Ya Uchukuzi Kwenye Reli (Ukamilisho wa Reli Ya SGR), na Usafiri wa Maziwa-Bahari (Ujenzi wa Meli Zinazokaribia Kukamilika Hivi Karibuni), Pamoja na Maboresho Ya Bandari. Kisha Akatoa Maelekezo Ya Usimamizi wa Shirika La Ndege, Ambalo Limetumiwa Fedha Nyingi Katika Uwekezaji.

Ulikuwa Wakati Mzuri.

#KaziIendelee 🇹🇿
 
Shirika la hizo ndege miaka nenda linazalisha hasara tu badala ya faida! Na hii ni kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kila mwaka, kutoka ofisi ya CAG! Ila viongozi wako hata hawakomi! Wanaendelea tu kununua hizo ndege.

Hivi watakuwa wamerogwa au!! Maana kwa sisi tunaofanya biashara, hakuna kitu tunakiogopa kama kile cha kufanya biashara isiyo na faida!! Au ni kwa sababu hizo hela wanazo zichezea, hawazitolei jasho?
 

Baada ya miaka 10, tutafilisika..!! Endeleeni kuzipokea ndege zinazotia hasara ya hivi kila mwaka..!!
 
Unapambana sana!

Nataka nikupime kama una uwezo wa kuwa kiongozi katika Tanzania hii iliyopo kwenye dunia ya ushindani.


Nisaidie kwa mawazo yako. Unadhani Tanzania ijike kwenye maeneo gani na ifanye nini ili kuhakikisha inakuwa Nchi ya Uchumi wa Kati au Juu katika miaka 50 ijayo?
 
Usinikumbushe! Huo ni uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mtu.

Nilisafiri nayo kwenda India wiki iliyopita. Naamini Samia alikuwa sahihi kutoipokea hiyo ndege. Kwa muonekano wa ndani, hapo kuna watu walibugia commission. Pili, naona Business Class imeondolewa Viti vya kulala! Hii si sawa, maana wengi kwa safari za usiku hupendelea kulala. Max zipo nyingi na zina Viti vya kulala! Kurudi ilibidi niondoke Jumatatu kwa vile inakwenda Dreamliner!

Nitakuwa wa mwisho kukubali kuwa hakukuwa na upigaji pale
 
Sio kwa ubaya Sio kwa ubaya
Naomba mnisaidie kunielewesha katika hili,
Kwenye ripoti kadhaa za CAG mfano ripoti ya 2021/2022 kumeonekana kuwa ATCL inaingiza hasara, sio Bilioni 30.63 au ile bilioni 150 ndani ya miaka mitano! Je mko na mipango ya kupata faida au ndo Mama anaupiga mwingi!?
Sio kwa ubaya Sio kwa ubaya
 
Hana uwezo huo
 
Kwa utaratibu wa Chama chetu na kwa jinsi anavyovutia, nakuhakikishia kuwa huyu binti muda si mrefu anaanza kula mema ya nchi hii. Hatuhitaji watu wenye akili kubwa kabisa
 
Na viatu ukavaa vya njano! Kweli chama unakipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…