Nilishiriki mapokezi ya ndege boeing 737 - MAX 9

Nilishiriki mapokezi ya ndege boeing 737 - MAX 9

Hili nakubaliana nawe kabisa.
Ndani ya CCM ili ufaidi,unatakiwa kuwa na akili "below average" na kuwa na kauzuri kiasi kwa wadada.
Nothing more.
Kwa utaratibu wa Chama chetu na kwa jinsi anavyovutia, nakuhakikishia kuwa huyu binti muda si mrefu anaanza kula mema ya nchi hii. Hatuhitaji watu wenye akili kubwa kabisa
[/QUOTE
 
Unapambana sana!

Nataka nikupime kama una uwezo wa kuwa kiongozi katika Tanzania hii iliyopo kwenye dunia ya ushindani.

Nisaidie kwa mawazo yako. Unadhani Tanzania ijike kwenye maeneo gani na ifanye nini ili kuhakikisha inakuwa Nchi ya Uchumi wa Kati au Juu katika miaka 50 ijayo?
Muonee huruma mkuu huo uwezo anautoa wapi
 
Shirika la hizo ndege miaka nenda linazalisha hasara tu badala ya faida! Na hii ni kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kila mwaka, kutoka ofisi ya CAG! Ila viongozi wako hata hawakomi! Wanaendelea tu kununua hizo ndege.

Hivi watakuwa wamerogwa au!! Maana kwa sisi tunaofanya biashara, hakuna kitu tunakiogopa kama kile cha kufanya biashara isiyo na faida!! Au ni kwa sababu hizo hela wanazo zichezea, hawazitolei jasho?
Piga hesabu ya kufufua shirika jipya, hesabu za ndege mpya na gharama zake za uendeshaji utapata idea kwa ndege mpya unaaza lini kuzalisha faida.

Siyo biashara ya kuuza genge hiyo, utegemee faida leo na kesho.
 
Nikushauri kitu Janeth, usitusimulie tunayoyafahamu. Badala yake jikite kwenye sera, ilani na mwelekeo wa chama (ccm).

Nasikitika sana kuona UVCCM tumekuwa hivi. Hatupo kwenye dhima ya uvccm hatukilindi chama tena bali tunalinda viongozi au makada. Hilo sio lengo la uvccm.

Kulinda maslahi ya viongozi au makada maarufu ni dalili za kuwa corrupt, na sio uzalendo hata kwa taifa. Kwa sasa wanajiita chawa, usiwe miongoni mwao.

Cc: Janeth Thomson Mwambije
 
Piga hesabu ya kufufua shirika jipya, hesabu za ndege mpya na gharama zake za uendeshaji utapata idea kwa ndege mpya unaaza lini kuzalisha faida.

Siyo biashara ya kuuza genge hiyo, utegemee faida leo na kesho.
Kulikuwa na ulazima wowote ule wa serikali kulifufua hilo shirika huku ikiwa na rekodi mbovu ya kuyqsimamia na kuyaendesha mashirika yake mengine?

Ni kwa nini wasingeingia ubia na sekta binafsi kwenye huo ufufuaji?

Una uhakika hata baada ya miaka 20 tangu hizo ndege ziliponunuliwa kwa mabilioni ya fedha za walipa kodi, zitazalisha faida, au zitaendelea tu kutengeneza hasara?
 
Sio kwa ubaya Sio kwa ubaya
Naomba mnisaidie kunielewesha katika hili,
Kwenye ripoti kadhaa za CAG mfano ripoti ya 2021/2022 kumeonekana kuwa ATCL inaingiza hasara, sio Bilioni 30.63 au ile bilioni 150 ndani ya miaka mitano! Je mko na mipango ya kupata faida au ndo Mama anaupiga mwingi!?
Sio kwa ubaya Sio kwa ubaya
Hiyo inayoitwa hasara si hasara kama hasara bali ni fursa.
 
Kulikuwa na ulazima wowote ule wa serikali kulifufua hilo shirika huku ikiwa na rekodi mbovu ya kuyqsimamia na kuyaendesha mashirika yake mengine?

Ni kwa nini wasingeingia ubia na sekta binafsi kwenye huo ufufuaji?

Una uhakika hata baada ya miaka 20 tangu hizo ndege ziliponunuliwa kwa mabilioni ya fedha za walipa kodi, zitazalisha faida, au zitaendelea tu kutengeneza hasara?
Mpaka 2027 ndege zote zitakuwa zimebaki mbovu
 
Kulikuwa na ulazima wowote ule wa serikali kulifufua hilo shirika huku ikiwa na rekodi mbovu ya kuyqsimamia na kuyaendesha mashirika yake mengine?

Ni kwa nini wasingeingia ubia na sekta binafsi kwenye huo ufufuaji?

Una uhakika hata baada ya miaka 20 tangu hizo ndege ziliponunuliwa kwa mabilioni ya fedha za walipa kodi, zitazalisha faida, au zitaendelea tu kutengeneza hasara?

Shirika hilo kwa Tanzania hii usifikiri kuna siku utasikia limeingiza faida.
.tumeshindwa mabasi ya mjini tu, ambayo hayana ushindani wa kibiashara tutaweza midege, ambayo ina upinzani wa kimataifa?

Sahau neno faida huko.
 
Sio kwa ubaya
Je hizi harasa ni kwamba chama tawala hakina la kusema au? Maana kama ingekuwa CHADEMA ndo yupo madarakani kwa hakika CCM wangesema tu? Na Sio kwa ubaya mwananchi kuuliza sio jambo baya
Fursa hizo hawawezi kusema lolote.
 
Mtoa mada anaandaa content vizuri lakini upande wa kujibu hoja anakimbia
 
Nilifanikiwa Kushiriki Kwenye Mapokezi Ya Ndege Mpya (Boeing 737 - Max 9) Ya Shirika La Air Tanzania (Air Tanzania Company Limited) Ambapo Mgeni Rasmi Katika Mapokezi Hayo Alikuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaaliwa, Kwa Niaba Ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kutokana na Mheshimiwa Rais Kutingwa na Majukumu.

Katika Mapokezi Haya, Mheshimiwa Waziri Mkuu Aliweza Kumpongeza Mheshimiwa Rais Kwa Juhudi Anazozifanya, Hususani Ndani Ya Miaka Hii Mitatu, Kwa Kuimarisha Sekta Mbalimbali Ikiwemo Sekta Ya Uchukuzi, Na Kutekeleza Ilani Ya Uchaguzi Ya Chama Cha Mapinduzi Ya Mwaka 2020-2025.

Pia Mheshimiwa Waziri Mkuu, Aliweza Kutujuza Mafanikio, na Umuhimu wa Sekta Ya Uchukuzi Nchini Kwa Maendeleo Ya Taifa Letu, Ikiwa Ni Pamoja Na, Kuwa Mchango Katika Kuhakikisha Ukuaji wa Uchumi Wetu Na Kuzalisha Ajira Nchini. Kuongeza Uwezo wa Taifa Kujitegemea Kiuchumi. Kuchochea Uzalishaji, na Kutumia Vyema Fursa za Rasilimali Zilizopo Hapa Nchini. Kuchochea Upatikanaji wa Fedha za Kigeni, Nchini. Na Ongezeko La Mnyororo wa Thamani Ya Mazao Ya Kilimo, Pamoja na Biashara, Na Kadhalika.

Lakini Pia Ameweza Kusema Ndege Ambazo Zimenunuliwa Kwa Kipindi Cha Miaka Mitatu Ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ambapo Tayari Ndege Tano Zimeshawasili Ikiwemo Ndege Ya Mizigo, Ndege Ya Sita Ikiwa Ni Boeing 737-9 Max Iliyowasili Leo, Na Ndege Nyingine Moja (Boeing 787-8 Dreamliner) Ambayo Inategemewa Kuwasili Hivi Karibuni.

Na Mpaka Sasa. Kuna Endelea Na Maboresho Ya Viwanja Vya Ndege Kwenye Mikoa Mbalimbali. Kubwa Zaidi Ni Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Msalato - Dodoma, Pamoja na Uboreshwaji wa Uwanja wa Pili wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere, Utaosaidia Kuifanya Tanzania Kuwa Kitovu Cha Anga, Afrika Mashariki.

Lakini Pia, Aligusia Mafanikio Ya Sekta Ya Uchukuzi Kwenye Reli (Ukamilisho wa Reli Ya SGR), na Usafiri wa Maziwa-Bahari (Ujenzi wa Meli Zinazokaribia Kukamilika Hivi Karibuni), Pamoja na Maboresho Ya Bandari. Kisha Akatoa Maelekezo Ya Usimamizi wa Shirika La Ndege, Ambalo Limetumiwa Fedha Nyingi Katika Uwekezaji.

Ulikuwa Wakati Mzuri.

#KaziIendelee 🇹🇿View attachment 2965988
VITI MAALUM BHANA
 
Back
Top Bottom