Nilisimamishwa mara 3 ndani ya mwezi mmoja, ndipo nikagundua tatizo hili

Nilisimamishwa mara 3 ndani ya mwezi mmoja, ndipo nikagundua tatizo hili

ChaliiBlog

New Member
Joined
Feb 23, 2016
Posts
3
Reaction score
1
Mwezi uliopita nimejikuta nikalipa fine nyingi sana za gari.

Mara ya kwanza nilisimamishwa na kukutwa nina deni la parking. Nikasema sawa, labda ni uzembe wangu.

Wiki iliyofuata nikasimamishwa tena. Kwa Kosa la kuto kulipia fine ya wiki iliyopita.

Wiki iliyofuata tena nikasimamishwa mda huu bima ilikuwa imeisha mda wake.

Hapo nikasema hapana, hii imezidi.

Nikaanza kutafuta kama kuna app au huduma inayoweza kunikumbusha kuhusu parking tickets, fines na bima. Niliziona chache, lakini hazikufanya kazi niliyokuwa nataka.

Kwa hiyo nikaamua kutengeneza yangu mwenyewe.

Nilitengeneza mfumo rahisi sana. Unaweka plate number ya gari lako, halafu mfumo unakagua mara kwa mara kama kuna parking tickets, fines za barabarani au bima inayokaribia kuisha. Ukigundua jambo lolote, unapata taarifa kupitia SMS na email. Kwa upande wa bima, unakumbushwa mwezi mmoja kabla haijaisha.

Nilipowaonyesha marafiki na watu wachache waliopenda wazo hilo, waliniomba niwaachie nao waitumie. Ndipo nikaamua kuiweka live kwa kila mtu.

Cha kushangaza, nilipoangalia gari langu lingine, nilikuta lina parking tickets 49 ambazo sikuzijua kabisa. Jumla ya deni ilikuwa TSh 24,500.

Kwa sasa mfumo unafanya mambo mawili:

• Unaweza kuangalia parking tickets za gari lolote papo hapo bila kusajili.
• Ukisajili gari lako, mfumo unaendelea kukagua parking tickets, traffic fines na tarehe ya kuisha kwa bima, kisha inakutumia taarifa kwa SMS na Email.

Unaweza kutumia hapa:

gariwatch.online

Huduma inagharimu TSh 9,900 kwa mwaka mzima.

Ukilinganisha na fine moja ya barabarani ambayo inaweza kuwa TSh 30,000 au zaidi, inaweza kujiokoa yenyewe kwa urahisi.

Kabla hujasajili, angalia kwanza kama gari lako lina parking tickets zozote ambazo hujui.

Ningependa kusikia maoni yenu. Je, hii ni kitu ambacho ungeweza kutumia? Na kuna huduma au taarifa gani nyingine ungependa kuona zikiongezwa?
 
Back
Top Bottom