Nilitahadharisha kuwa Simba ni mbovu ila mnazidisha chumvi

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Kipindi kama cha wiki mbili zilizopita, nilileta uzi juu ya tuwatahadharisha wachambuzi uchwara kuwa ni kweli Simba yaweza kuwa mbovu ukilinganisha na Simba ya miaka 2 iliyo pita, ila ubovu wake mmeuzidishia chumvi kupita kiasi.

Kiufupi simba sio mbovu kiasi hicho kama wachambuzi wetu wanavyo tuaminisha, yaani ukisikia wachambuzi wanavyo iongelea simba, kama huijui Simba waweza sema simba inazidiwa mpaka na Gwambina.

Niliwaambia kuwa hata simba akonde vip hawezi kuwa paka hivyo pamoja na ubovu wake mnao usema ni kosa kubwa kuichukulia poa maana itakudhalilisha.

Horoya waliichukulia simba kawaida sana yakawakuta ya kuwakuta.

Ushauri wangu kwa wachambuzi wetu jifunzeni kuchambua kitaalamu na sio kuchambua kwa kufuuta upepo unapo elekea alafu kuweni na akiba ya maneno maana huu ni mpila lolote laweza kutokea na mkabaki na rundo la aibu.

Mfano kuna mchambuzi mmoja aliahidi kuacha kazi iwapo Sakho ataitwa timu ya taifa ila sasa hivi anashindwa ajifiche wapi kwa aibu.

Narudia tena kuweni na akiba ya maneno huu ni mpila na una maajabu yake.
 
Uzi wako umeficha contents nyingi sana muhimu, mfano majina ya hao wachambuzi uchwara... Sehemu ipi ilitiwa chumvi sana, nani aliahidi kuacha kazi, uzi gani uliuleta wiki 2 nyuma, hata link umeshindwa kuweka.

Angalizo: Kushindwa kuweka details hizo juu na ww unaangukia kwenye wachambuzi uchwara, mnaochambua baada ya matokeo. Mfano Simba angefungwa jana ungekuja na sura yako halisi
 
Kipindi kama cha wiki mbili zilizo pita, nilileta uzi juu ya tuwatahadharisha wachambuzi uchwara kuwa ni kweli Simba yaweza kuwa mbovu ukilinganisha na Simba ya miaka 2 iliyo pita, ila ubovu wake mmeuzidishia chumvi kupita kiasi...
Nilichogundua shabiki wa simba wengi Wana ugonjwa wa utimamu wa akili unaitwa baipola. Wanabadilika kulingana na vipindi vya upepo.. Simba wangefungwa Jana Leo hii ungesema Nn?. Nkaanze matibabu kima nyie
 
kwa hiyo unataka hata timu ikishinda watu wakwazike na matokeo? Bila shaka wewe wakulete mirembe hapa yawezekana wewe ndo hallucination.
 
Nilichogundua shabiki wa simba wengi Wana ugonjwa wa utimamu wa akili unaitwa baipola. Wanabadilika kulingana na vipindi vya upepo.. Simba wangefungwa Jana Leo hii ungesema Nn?. Nkaanze matibabu kima nyie
Nimesha kwambia simba inaweza kuwa mbovu lakini sio kwa kiasi mnacho iongelea.
 
Nilichogundua shabiki wa simba wengi Wana ugonjwa wa utimamu wa akili unaitwa baipola. Wanabadilika kulingana na vipindi vya upepo.. Simba wangefungwa Jana Leo hii ungesema Nn?. Nkaanze matibabu kima nyie
Waliosema Nani Hana mbinu kweny game za kimataifa ni mashabiki wa simba sio?
 
nilimsikia mchambuzi wawasafi juzi juzi havi anachambua kimataifa mechi ya mancity😄

alikuwa anachambua haland jinsi anavyo fumania nyavu akamsifia sana mwisho kilicho fanya nicheke sana alisema hivi

"kunasiku haland alifunga mabao mengi tuu fest half mabao 3 ila walivyo enda mapunziko kwenyechumba Cha kubadilishia nguo haland alikuwa Hana furaha kabisa😅

lafiki yake akamfata kumuuliza inakuwaje amefunga goli nyingi na bado hanafuraha?

halandi akajibu Brooke nasikitika Kuna nafasi mbili zawazi nimezikosa ndio Mana sinafuraha😅😅😅"

nikajiuliza kumbe mchambuzi kwakuangalia tuu anaweza kujua wachezaji wanaongea Nini? tena kwenye tv?
kiukweli sikuamini uchambuzi wake huo ila wadau inawezekana kufahamu wachezaji wanachoongea wee ukiwa kwenye tv wao vyumbani?
 
Tunashukuru kwa uchambuzi wao jana umetusaidia sana
 
Umeongea ukweli..kwa sasa kwenye uchambuzi kuhusu Simba huwa namsikiliza MBWADUKE tu kwa sababu anatumia data/ takwimu na facts
 
Tunashukuru kwa uchambuzi wao jana umetusaidia sana
 
Tunashukuru kwa uchambuzi wao jana umetusaidia sana
 
na wewe mkuu unaenda na upepo ulivoona kashinda ndio unakuja kuwasuta wachambuzi wenzio, ungewakanusha jana asbh ingekuwa na maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…