NILITAMKIWA MANENO>>>KWA KIASI YAMETIMIA>>>

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
13,085
Reaction score
15,197
Hapo zamani za kale nilikuwa na Toyota Stout....nilikuwa nabeba mizigo ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Huku na kule nikaanza kupiga trip za night kwa nigh....t chaka kwa chaka,,sababu ma trafiki walitaka nitia umaskini.

Katika safari hizo nilikuwa ninafika pori fulani kuna Mzee mmoja alikuwa ni mwenyeji katika pori hilo.

Zamani hizo kulitokea (operesheni sogeza),,,raia walirundikwa pahala pamoja kuanzisha vijiji na kuacha maeneo yao ya asili.

Mzee huyu aliona isiwe taabu akarudi maeneno yake ya asili na kuendelea na shughuli zake za uzalishaji,,,kurina asali,,,kuwinda ,,,kulima na kuchoma mkaa(ambayo ndiyo ilikuwa dili yangu pamoja na mitikasi ya mbao)..

Sasa huku na kule kila nikizuka pori mzee simuoni,,,nikaamua kwenda pahala anapoishi,,,nikamkuta mkewe akanijuza mwamba yupo ndani hoi...anaumwa,,,duuuh...nikaingia ndani kwake,,,walahi khali yake ilikuwa mbaya sana...sikupoteza muda nika ahirisha shughuli zote nikamtia mwamba kwenye stout,,,chap kwa haraka mpaka Hospitali ya Mkoa ule...

Kwa kifupi mzee alikuja kupona na kuwa na afya njema na mwili wake kurudi kama zamani.

Tukawa tunaendelea na mitikasi ya pori kwa pori.

Kila baada ya wiki mbili nazuka chaka.

Siku hiyo nazuka chaka nakuta kaniandalia mbuzi kuku na asali...pia kuna wazee kibao,

Waliandaa bonge la sapraizi pamoja na pombe ya asali.

Baada ya kula...... na mioyo kuchangamka...... wakaniketisha kwenye kiti cha ngozi ,,,sijui ni ya mnyama gani...wakanifunga nguo mithili ya shuka/rubega.

Wakaanza kutamka maneno ambayo siyafahamu...sababu ni kabila tofauti...wakazidi kutamka..nikatemewa na mate,,,

Baada ya hapo yule mzee(mwamba rafiki) akanitafsiria kwa uchache kwamba ni baraka...

Miaka ikapita,,,siku zikasonga,,magumu mengi nikawa nakutana nayo maishani,,,lakini ninavyo chomoka chomoka...mpaka inafika pahala watu wanajua aidha mie mwanga/mchawi..au nina fundi/mtaalam kiboko,,,au pengine ni aina ya manabii,,;

N,B,
CHUNGA SANA WATU WANATAMKA NINI JUU YAKO.
 
Hii niliyonukuu, ulizuka wakati simu zimeshaanza kutumiwa na raia?

Maana haiingia akilini, uzuke bila taarifa na ukute wameandaa sherehe.

Labda kama ulikuwa unaenda kwa ratiba mfano Kila jumatatu, na Mzee akawa ameikariri ratiba.

Japo pia, ukikariri ratiba, binadamu anaweza pata changamoto muda wowote.
 
KIla Jumatano lazima nizuke.....dili zetu zilikuwa kama magendo fulani hivi.....
 
Hapo zamani za kale nilikuwa na Toyota Stout....nilikuwa nabeba mizigo ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Huku na kule nikaanza kupiga trip za night kwa nigh....t chaka kwa chaka,,sababu ma trafiki walitaka nitia umaskini.

Katika safari hizo nilikuwa ninafika pori fulani kuna Mzee mmoja alikuwa ni mwenyeji katika pori hilo.

Zamani hizo kulitokea (operesheni sogeza),,,raia walirundikwa pahala pamoja kuanzisha vijiji na kuacha maeneo yao ya asili.

Mzee huyu aliona isiwe taabu akarudi maeneno yake ya asili na kuendelea na shughuli zake za uzalishaji,,,kurina asali,,,kuwinda ,,,kulima na kuchoma mkaa(ambayo ndiyo ilikuwa dili yangu pamoja na mitikasi ya mbao)..

Sasa huku na kule kila nikizuka pori mzee simuoni,,,nikaamua kwenda pahala anapoishi,,,nikamkuta mkewe akanijuza mwamba yupo ndani hoi...anaumwa,,,duuuh...nikaingia ndani kwake,,,walahi khali yake ilikuwa mbaya sana...sikupoteza muda nika ahirisha shughuli zote nikamtia mwamba kwenye stout,,,chap kwa haraka mpaka Hospitali ya Mkoa ule...

Kwa kifupi mzee alikuja kupona na kuwa na afya njema na mwili wake kurudi kama zamani.

Tukawa tunaendelea na mitikasi ya pori kwa pori.

Kila baada ya wiki mbili nazuka chaka.

Siku hiyo nazuka chaka nakuta kaniandalia mbuzi kuku na asali...pia kuna wazee kibao,

Waliandaa bonge la sapraizi pamoja na pombe ya asali.

Baada ya kula...... na mioyo kuchangamka...... wakaniketisha kwenye kiti cha ngozi ,,,sijui ni ya mnyama gani...wakanifunga nguo mithili ya shuka/rubega.

Wakaanza kutamka maneno ambayo siyafahamu...sababu ni kabila tofauti...wakazidi kutamka..nikatemewa na mate,,,

Baada ya hapo yule mzee(mwamba rafiki) akanitafsiria kwa uchache kwamba ni baraka...

Miaka ikapita,,,siku zikasonga,,magumu mengi nikawa nakutana nayo maishani,,,lakini ninavyo chomoka chomoka...mpaka inafika pahala watu wanajua aidha mie mwanga/mchawi..au nina fundi/mtaalam kiboko,,,au pengine ni aina ya manabii,,;

N,B,
CHUNGA SANA WATU WANATAMKA NINI JUU YAKO.
Walivokutemea mate,inawezekana wakakuambukiza magonjwa hatari siku nyingine
 
Inaonekana ni kama vile Dawa yetu imeanza kupungua nguvu na tulikukataza kuito hii siri,

Sasa itabidi urudi tena huku Kijijini ili tukutemee mate tena.
 
Back
Top Bottom