Uchaguzi 2020 Nilitegemea Upinzani wafanye Siasa za mitandao tu

Uchaguzi 2020 Nilitegemea Upinzani wafanye Siasa za mitandao tu

Wakuu, Sikutegemea kabisa Chadema waitishe mikutano ya hadhara na kuruhusu mikusanyiko kama inayo endelea sasa, Wote tunajua kuwa hawa ndugu zetu walikuwa wanapiga mayowe kuwa Convid19 itatumaliza kama hatua za haraka zisipo chukuliwa, Mwenyekiti wao Freeman mbowe alienda mbali zaidi na Kumtaka Mheshimu Rais aweke Full or partial lockdown na curfew mbalimbali, Ila ni ajabu sana hawa watu hata bado swala la corona halijaisha ila wanaifurahia nchi yao bila face mask wala Social distancing rules, Wana enjoy kweli kweli na wanajichanganya haswa na Raia,

Hii maana yake ni kuwa tanzania is free from Corona, We are safe and strong, Lakini hawa Wapinzani wana enjoy hizi political rallies na mikusanyiko kwa ujasiri na ushupavu wa Mheshimiwa Rais Magufuli, Rais asingechukua maamuzi haya na kuwasikiliza hao vibaraka leo pengine ingekuwa wanalia lia kuwa wamefungiwa ndani kwa ajili ya Corona wapinzani wameshindwa kutoa hata credit kwa Rais Magufuli sisi hatuna habari lao waendelee kuenjoy mikutano ya kisiasa na mikusanyiko na hata face mask tu hawavai na wajue tu wako salama chini ya Amiri jeshi mkuu Magufuli

Katika kipindi Tanzania inahitaji Rais mwenye maamuzi basi ni wakati huu Rais Magufuli anatosha sana na Miaka mitano atapata, Nchi haiwezi kuongozwa kwa kerere za activists wa Twitter na JF

Kasi Kasi Zaidi
JPM mitano tena
 

Attachments

  • Chato33.jpeg
    Chato33.jpeg
    182 KB · Views: 1
Mungu amempiga upofu Magufuli asiione corona ili asije akapata kisingizio cha kukataa kukabidhi nchi kwa Lissu kwa kisingizio cha watu kuwa kwenye kizuizi cha corona.
 
Kwa ubatizo naoufanya Lissu naamini mpaka October utakuwa umeachana na Ujima wa fikra.
 
Back
Top Bottom