Nilitembea na ndugu yake.....

Mhh hao watoto sio wako kweli babu DC?

Hapana mdogo wangu...Toka tulipoachana sikuwa hata kumgusa mkono. Ila jamaa pamoja na kujua hayo hakuwahi hata siku moja kumwamini huyo mke wake....Na mbaya zaidi alimwacha akakimbia na KCC (kitu kama Beki 3 hivi)!!
 
Nitaonana nae badae, sijamwambia nataka kumwambia nini ila nimemwambia nina jambo muhimu la kuongea nae.
Nahisi bado hajaambiwa chochote.
Nitawapa feedback na nashukuru kwa ushauri wenu
Ni wazo zuri kumwambia kama ulivyoshauriwa na wote.
Kwa siku za baadae, jaribu kuepuka kauli ya kumwambia mpenzi wako "Nina jambo muhimu nataka kukueleza/ Nataka kuzungumza na wewe...". Kisaikolojia ya mahusiano ni bora kila suala kulizungumza katika hali ya kawaida kabisa bila ya "kutoa onyo" kabla ili kupunguza/kuepuka "tensions".
Kila la heri.
 
hebu kaa nalo, mwache dogo yake akatoe siri hiyo bt jiandae kujibu! Kumbuka ndugu ni ndugu!
 
Unaweza kutueleza kwa nini ungeanza mbele?

Mkuu nisingejisikia comfortable pale nitakapokuwa namwona waif anachekeana na Kaka (ndugu) ambaye najua wazi walikuwa na uhusiano kabla yangu. Pia nisingeweza kumwekea mipaka waif eti asiwasiliane na huyo mtu (siamini juu ya kumwekea sheria mwenza wangu). Kwa mantiki hiyo basi, njia mwafaka kwangu ingekuwa kuachana naye kwa amani tu kuliko ku-jeopardize maisha yangu kwa presha za bure.
 
Nitaonana nae badae, sijamwambia nataka kumwambia nini ila nimemwambia nina jambo muhimu la kuongea nae.
Nahisi bado hajaambiwa chochote.
Nitawapa feedback na nashukuru kwa ushauri wenu

Kila la heri ujiandae pia kujibu maswali magumu toka kwa mpenzio.
 
Mwambie tu hilo halina mkwara...ila ukimwambia tayari umempa kisosi asije geuka...
 

Je ingekuwa ni wewe ambaye uliwahi kuwa na uhusiano na binti ambaye kwa sasa ndo huyo GF wako ungemwacha kwa sababu hiyo? Na katika suala hiyo la DP, utamwacha kwani yeye ana kosa gani?
 
Wanaume navyowajua wana wivu mbaya sana. In most cases hawawezi kuvumilia wanaumia sana wakijua jamaa aliyekuwa nawe before them. Sasa na hivi ni ndugu maanake mtakuwa mnakutana mara kwa mara. If you could keep it a secret mi naona powa kwani si mliachana hata akijua siku za usoni utamwambia kuwa hukutaka kumpa presha. As long as uhusiano ulikwisha kati yenu, na jamaa hajawahi kukwambia umtajie majina ya uliyokuwa nao before him; bora unyamaze. My ex boyfriend nilimwambia jina la jamaa yangu kabla yake akanambia NK bora usingesema it hurts me so much to know that this guy had also enjoyed what I have. Ilimuuma kwa kuwa alikuwa anamjua na hakuwa ndugu yake. Mume wangu wala sijamwambia jina la jamaa yangu before him. Na kuna siku nilimuona kwenye TV anafunga ndoa (kaoa dada maarufu) nikauchuna. Akabaki kuniuliza why are you so interested with this wedding, nikamwambia namfahamu huyu kijana; wala sikumpa details ya nini kumpa presha.
 
. Akabaki kuniuliza why are you so interested with this wedding, nikamwambia namfahamu huyu kijana; wala sikumpa details ya nini kumpa presha.
Du kuna watu mna mioyo ya bati, yaani unaangalia harusi ya ex wako with interest?ningekuwa mm hapo nimekwisha nuna na kuchange mood siku nyingi.
 
Je ingekuwa ni wewe ambaye uliwahi kuwa na uhusiano na binti ambaye kwa sasa ndo huyo GF wako ungemwacha kwa sababu hiyo? Na katika suala hiyo la DP, utamwacha kwani yeye ana kosa gani?

Swali la kwanza sijakuelewa, ila swali la pili ni kama nilivyotanabaisha kuwa sintomuacha kwa kinyongo wala ugomvi au kwamba alikosea bali nitajiweka pembeni kwa kuwa najua sintoweza kuhimili maumivu ya moyo yatakayoweza jitokeza huko mbeleni..

NB: Hongera Da Prety kwa kufanikiwa kuutua mzigo, cha muhimu tuombe Mungu jamaa yako aweze kutafakari vyema na kuchukua uamuzi ambao hautakuwa mbaya kwa upande wako, natumaini mtaendelea vyema na mahusiano yenu na Mungu awajalie upendo na uvumilivu miongoni mwenu. Nimejifunza jambo kutokana na hiki kisa chako.
 

Nyumba Kubwa issues zako ni tofauti na ya Da Pretty. Wewe kama usingemwambia, wala asingejua. Lakini Da Pretty kama hatamwambia, it is likely that that huyu ndugu atasema. He may not say now, but might say later. Hapo swali la boyfriend litakuwa why you did not tell me then? Tena kumwambia, Da Pretty atakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kujua if the her boyfriend really loves her. Kama kweli anampenda kwa dhati sidhani kama atampotezea. In deed anaweza kum trust Da Pretty hata zaidi.

Kama alivyosema Da Pretty: "Ni nafasi yake kuamua na ni bora achague kuliko ningemficha ajue baadae."
 
Sasa ninune wakati ni mimi ndie niliyempiga chini. Isitoshe wakati yeye anaoa mie nilikuwa nimeshaolewa for 3 years!

Du kuna watu mna mioyo ya bati, yaani unaangalia harusi ya ex wako with interest?ningekuwa mm hapo nimekwisha nuna na kuchange mood siku nyingi.
 
Kama urafiki ulikwisha; kwa nini akija kujua baadae awe mkali???. Na kama hajawahi kuuliza majina ya maboyfriend wa zamani kwa nini akija kujua baadae akasirike? Afu mimi najua wanaume si wambea, hamna atakaye mwambia. Unamwambia ili iweje. SI mlishahachana! Na nijuavyo mimi utashangaa anamwambia jamaa anakasirika na kumwambia why are you telling me? To make me jelous! Ok now tell me the names of all men that you have been sleeping with may be you have slept with more relatives. Tena ndio urafiki uko mwanzo nakwambia jamaa anaweza kumwacha si kwa kuwa ametembea na jamaa yake ila kwa kuwa amemwambia.
Maana hata mimi sioni nia ya kumwambia. Tena amesema undugu ni wa kubandika na gundi.

 

Nani alikwambia wanaume sio wambea? Acha kabisa. Inawezekana hata huyo ndugu asimwambie, lakini boyfriend aka kujua tuu. Wanaume ni wambea usiseme. Kuna mambo wanaume wanaambiana wao kwa wao, but you will never know.
 
Kutakuwa na tatizo tu kama hao mashemeji wana more story to tell than past relationship. Kama wanajua mengi mabaya kuhusu mdada hapo ni issue. Lakini kama alikuwa ni mtulivu, na what happened ni relationship like any other broken relationships, sioni shida hata wakileta umbea baadae. Swali linakuja; kwa nini mdada ali break up na huyo ndugu? Je dada ametulia? Maana unawezakuwa na past relationship lakini jamaa uliye break nae bado akawa hana baya la kusema juu yako; na bado anaamini you are a good girl. Ila kama mliachana kisa alikufumania, hapo funga virago maana watasema tu kuwa kaka umeingia mkenge.

Nani alikwambia wanaume sio wambea? Acha kabisa. Inawezekana hata huyo ndugu asimwambie, lakini boyfriend aka kujua tuu. Wanaume ni wambea usiseme. Kuna mambo wanaume wanaambiana wao kwa wao, but you will never know.
 
Reactions: EMT
nyumba kubwa;]Kutakuwa na tatizo tu kama hao mashemeji wana more story to tell than past relationship. Kama wanajua mengi mabaya kuhusu mdada hapo ni issue. Lakini kama alikuwa ni mtulivu, na what happened ni relationship like any other broken relationships, sioni shida hata wakileta umbea baadae. Swali linakuja; kwa nini mdada ali break up na huyo ndugu? Je dada ametulia? Maana unawezakuwa na past relationship lakini jamaa uliye break nae bado akawa hana baya la kusema juu yako; na bado anaamini you are a good girl. Ila kama mliachana kisa alikufumania, hapo funga virago maana watasema tu kuwa kaka umeingia mkenge.

NK tatizo kwetu wanaume hatupendi kuamini kuwa yazamani yamepita na hayatajirudia tena kutokana na watu wengi tunaowaona wakijikumbushia na watu wao wa zamani. Mara kwa mara nyie wadada mnakataa kukiri hili jambo, kama mwanaume najuwa kw mtu mliechana na kwa amani bila tatizo alama huwa haifutiki. Kinachohitajika ni ustarabu tu wa kuheshimu ndoa uliyo nayo na mke unayempenda. Ustaarabu siyo kwa wote maana kuna wanaume wanang'ang'ania mpaka basi. Na jinsi mlivyoumbwa kwa huruma nyie wadada unashtukia tu ulishachojowa unahamaki hujuwi kilichotokea. Ukianza kufikilia hali kama hiyo, na unajuwa kuna uwezekano wa huyo ngugu yake huyo bwana kuwa anakuja kumtembelea lazima jamaa apate pressure. Haamini kama kutakuwa na usalama kama akitembelewa na ndugu yake. Mbaya zaidi, Pretty atakuwa shemeji yake na hivyo kutaniana kupo. Kwa hali hiyo hata kama jamaa akiwakuta wanaongea kitu cha kawaida tu ataanza kufikiria kuwa wanataka kukumbushia.

Kwakweli ni hari ngumu sana jamaa atakuwa nayo. Hata kama ni mimi najuwa ningejisikia vibaya. Chukulia mfano mumeo alikuwa na mahusiano na ndugu yako na ukaja kujuwa hata kama ni baadaye. Utakuwa na amani siku huyo ndugu akija kukutembelea? Mda wote utakuwa unamwangalia huyo dada na mumeo machoni pindi wanapokuwa wanaongea japokuwa ni mashemeji kwa mda huo. Ni vema usijuwe watu waliyopita kwa mwenzi wako maana inashusha confo unapoonana nao ukiwa na mwenzi wako.
 
Poa DP,

Nadhani umetekeleza wajibu wako...Kama kweli anakupenda na yuko realistic hatakuacha kwa sababu umekuwa mkweli kwani hata akienda wapi atapata story hiyo hiyo!
 
huyo jamaa namshauri aachane na kicheche #******#
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…