Habari,
Hivi karibuni nimeingia kwenye uhusiano mpya na kijana ambaye ninahisi ananipenda kweli.
Tunakaribia mwezi wa pili katika uhusiano sasa, ni mvumilivu na hana haraka na mwili wangu.
Ni rafiki mzuri na amenitambulisha kwa rafiki na ndugu zake wengi maana karibu kila weekend nakutana na watu wapya.
Kilichotokea jana kanitambulisha ndugu yake ambaye nilimbana sana kujua undugu wao akaniambia bibi zao ni ndugu. Huyo kijana tunafahamiana vizuri japo tulijifanya hatujuani ni kua alikua shemeji yangu kipindi cha nyuma nimewahi kuwa na uhusiano na kaka wa huyo kijana niliyetambulishwa.
Wapendwa, nashukuru sana kwa ushauri wenu ambao kwangu nasema ni mzuri.
Nimependa mawazo yote....
Tumetoka na kijana tukapiga story zetu nyiiiingi wala hakuniharakisha niseme nilichomuitia!
Wapendwa!!
Nimejikanyaga wee lakini hatimaye nimesema,
nimetua mzigo na hapa nina mawazo!!
Ni kweli kaniuliza maswali mengi na magumu na kikubwa
kataka kujua uhusiano wangu na huyo kijana hadi sasa upoje.
Nimejieleza na nimempa sababu za kujieleza lakini cha msingi NIMEWEKA WAZI.
HAJANIBU LOLOTE KUHUSIANA NA HILO JAPO MASWALI NIMEULIZWA SANA NA NAHISI KAMA VILE ANA KINYONGO!
Kanirudisha nyumbani ila sijajua anawaza nini,
nampenda sikutaka kumkosa ila kwa hili sitajuta kwa sababu nisingeweza kufuta historia.
Ni nafasi yake kuamua na ni bora achague kuliko ningemficha ajue baadae.