huyo jamaa namshauri aachane na kicheche #******#
nyumba kubwa;]Kutakuwa na tatizo tu kama hao mashemeji wana more story to tell than past relationship. Kama wanajua mengi mabaya kuhusu mdada hapo ni issue. Lakini kama alikuwa ni mtulivu, na what happened ni relationship like any other broken relationships, sioni shida hata wakileta umbea baadae. Swali linakuja; kwa nini mdada ali break up na huyo ndugu? Je dada ametulia? Maana unawezakuwa na past relationship lakini jamaa uliye break nae bado akawa hana baya la kusema juu yako; na bado anaamini you are a good girl. Ila kama mliachana kisa alikufumania, hapo funga virago maana watasema tu kuwa kaka umeingia mkenge.
NK tatizo kwetu wanaume hatupendi kuamini kuwa yazamani yamepita na hayatajirudia tena kutokana na watu wengi tunaowaona wakijikumbushia na watu wao wa zamani. Mara kwa mara nyie wadada mnakataa kukiri hili jambo, kama mwanaume najuwa kw mtu mliechana na kwa amani bila tatizo alama huwa haifutiki. Kinachohitajika ni ustarabu tu wa kuheshimu ndoa uliyo nayo na mke unayempenda. Ustaarabu siyo kwa wote maana kuna wanaume wanang'ang'ania mpaka basi. Na jinsi mlivyoumbwa kwa huruma nyie wadada unashtukia tu ulishachojowa unahamaki hujuwi kilichotokea. Ukianza kufikilia hali kama hiyo, na unajuwa kuna uwezekano wa huyo ngugu yake huyo bwana kuwa anakuja kumtembelea lazima jamaa apate pressure. Haamini kama kutakuwa na usalama kama akitembelewa na ndugu yake. Mbaya zaidi, Pretty atakuwa shemeji yake na hivyo kutaniana kupo. Kwa hali hiyo hata kama jamaa akiwakuta wanaongea kitu cha kawaida tu ataanza kufikiria kuwa wanataka kukumbushia.
Kwakweli ni hari ngumu sana jamaa atakuwa nayo. Hata kama ni mimi najuwa ningejisikia vibaya. Chukulia mfano mumeo alikuwa na mahusiano na ndugu yako na ukaja kujuwa hata kama ni baadaye. Utakuwa na amani siku huyo ndugu akija kukutembelea? Mda wote utakuwa unamwangalia huyo dada na mumeo machoni pindi wanapokuwa wanaongea japokuwa ni mashemeji kwa mda huo. Ni vema usijuwe watu waliyopita kwa mwenzi wako maana inashusha confo unapoonana nao ukiwa na mwenzi wako.
Afadhali umeniunga mkono from men's view point, maana nilikuwa nikisema wanaume hawana chest ya kumezea wakijua uliyekuwa nae before watu wameona naongea kichina kwa kuwa mimi mwanamke. Sometimes we better keep secrets.
Hongera kwa kusema ukweli, however inabidi uoneshe how special you are to the guy. Kwa sababu sisi wanaume tuna wivu. Kwa hiyo baada ya yeye kufahamu huo uhusiano wako uliopita inabidi umuoneshe kuwa wewe upo kwa ajili yake tu na hapatatokea lolote baya baadaye kwa sababu ya past events. Kwa sababu inaweza kutokea kutoelewana au kupishana kisha jamaa akalink je ungemfanyia hivyo huyo ndugu yake au una take advantage ya upole wake. Pia umesema hana haraka na mwili wako, labda wewe umeweka condition za kumforce asiwe na haraka na mwili wako hivyo kumlazimisha akutambulishe kwa nduguze ili isitokee akaku dump cheaply kwa sababu umeshawajua ndugu zake.
Je huyo ndugu yake ndiye aliyefungua mlango maanake kwa baadhi ya wanawake aliyefungua mlango hurusiwa kuingia bila kubisha hodi mara atakapo kuingia tena, hii inaweza kuwa a matter of concern kwa baadhi ya wanaume.
Nakwambia mdada ana maswali mengi kweli ya kujibu. Mojawapo hilo la kwenye bold. Ndio maana ni heri kujinyamazia. Akija kujua mna watoto atakuacha? Na by that time amekwisha kujua na hana wasi wasi na tabia yako. At this early stage kukuacha wala hafikirii mara mbili kwani bado hajakolea (miezi miwili tu). Tatizo naloliona si kuwa atamwacha kwa kuwa kajua; ila dada anaweza kuwa kwenye uhusiano ambao ni full wasi wasi mpaka mwenyewe anaweza amua kubwaga manyanga.
Well tuombee mema kwani ameshamwambia. Ila kwa atakayekutana na similar situation mawazo toka hapa jamvini yatamsaidia.
Habari,
Hivi karibuni nimeingia kwenye uhusiano mpya na kijana ambaye ninahisi ananipenda kweli.
Tunakaribia mwezi wa pili katika uhusiano sasa, ni mvumilivu na hana haraka na mwili wangu.
Ni rafiki mzuri na amenitambulisha kwa rafiki na ndugu zake wengi maana karibu kila weekend nakutana na watu wapya.
Kilichotokea jana kanitambulisha ndugu yake ambaye nilimbana sana kujua undugu wao akaniambia bibi zao ni ndugu. Huyo kijana tunafahamiana vizuri japo tulijifanya hatujuani ni kua alikua shemeji yangu kipindi cha nyuma nimewahi kuwa na uhusiano na kaka wa huyo kijana niliyetambulishwa.
Wapendwa, nashukuru sana kwa ushauri wenu ambao kwangu nasema ni mzuri.
Nimependa mawazo yote....
Tumetoka na kijana tukapiga story zetu nyiiiingi wala hakuniharakisha niseme nilichomuitia!
Wapendwa!!
Nimejikanyaga wee lakini hatimaye nimesema,
nimetua mzigo na hapa nina mawazo!!
Ni kweli kaniuliza maswali mengi na magumu na kikubwa
kataka kujua uhusiano wangu na huyo kijana hadi sasa upoje.
Nimejieleza na nimempa sababu za kujieleza lakini cha msingi NIMEWEKA WAZI.
HAJANIBU LOLOTE KUHUSIANA NA HILO JAPO MASWALI NIMEULIZWA SANA NA NAHISI KAMA VILE ANA KINYONGO!
Kanirudisha nyumbani ila sijajua anawaza nini,
nampenda sikutaka kumkosa ila kwa hili sitajuta kwa sababu nisingeweza kufuta historia.
Ni nafasi yake kuamua na ni bora achague kuliko ningemficha ajue baadae.