Waheshimiwa wadau wenza , nimefatililia michango yenu 1 baada ya nyingine, atlist Kongosho amejaribu.
Isichukuliwe kwmb wale waliotuzaa akili zao zilikua finyu laa ! Na sisi ndiyo tuko bora zaidi.
Haukuwekwa utani pasipo kusudio maalumu.
Navyofahamu shabaha ya utani mf.
Mzee Kaniki , ni Mz. Maarufu eneo analoishi, Mz mwenye pesa , na ni mwenye jina kubwa, ameoa na ana watoto.
Kupitia umaarufu wake , na mipesa yake , anatumia loophole hiyo kutembea na vibinti.
Vibinti ambavyo vingine ni vidogo kupita binti zake.
Inafika hata member wa familia yake wanatambua unajisi huo wa Baba yao.
Mz. Kaniki ameshatengeza mazingira ya kuogopwa sana na watu wa hom kwake,
na yote ni kuweka kinga , rejea tabia yake.
Na ndivyo itakavyokua hakuna atakaethubutu kumsema/kumkanya aache unajisi ndani ya watu wa nyumbani kwake. Hapo sasa watani ndiyo hufanya kazi/jukumu la kumfikishia ujumbe Mzee sampuli ya Kaniki. Iko mara mbili, familia ya mnajisi huweza ikawaomba watani private wafikishe msg kwa mlengwa , ama kama watani wamejua kwa vyanzo vyao, pia humfikishia msg Mzee muharibifu. Maneno kama mf.
- Una nini we Mzee cha maana we Mzee !
- Unajifanya una pesa ? Huna lolote maskini mkubwa.
- Alafu mchezo wako na vibinti vyetu tumeshaujua ! Subiri tuje tukukamate utaozea jela !
Ofcoz hilo la mwisho litamgusa na atajua tena bila mashaka kua uchafu wake ushatambulika.
Na hatimae atalazimika kuuacha unajisi wake.
Na hivi ndy ilikua purpose ya WATANI/UTANI.