Nilivunja kimdoli cha kibata kando ya barabara nikapigwa kwenzi

Nilivunja kimdoli cha kibata kando ya barabara nikapigwa kwenzi

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
971
Reaction score
1,165
Sisemi vibaya! Ila hawa ndugu zetu ni wababe sana kwa watembea kwa miguu! Majuzi juzi tu natoka Msimbazi napita kando ya barabara nakumbuka kulikuwa na mdada anauza korosho na karanga, kwa mbele kidogo kulikuwa na mauzo ya kapeti ya mnada!

Kumbe lile kapeti kwa mbele bwana kuna jamaa anauza vimdoli vya watoto kulikuwa na train ya plastic na vibata vya vile vya ufunguo! Katika tembea yangu jamaa wa kapeti walikuwa wamenikinga kidogo, bwana wee!

Si nikakanyaga kibata kimoja kilichokuwa kinakuja barabarani! Kikapasuka na kunichoma, ile kushangaa nikachezea kwenzi kama masihara😁 kibaba kilikuwa sijui cha Mbeya kile maana kilikuwa kimepanda halafu mbavu nikashindwa kuunguruma! Bahati nzuri wapenda haki wakatetea nisilipe kosa lake mwenyewe anafanya mishe kwenye road ya watembea kwa miguu bila tahadhari..! Hiyo ndo ilikuwa ponea yangu..

Sina maana nawachukia ndugu zetu! Ila tuisikilize serikali, na serikali iwasikilize ndugu zetu.
 
Back
Top Bottom