Nabii koko
Member
- Aug 16, 2022
- 21
- 15
Kuna mambo mengine mtu unaweza kufanya hapa duniani halafu baadaye ukigeuka ilikotoka ukajiuliza, hivi mi mimi kweli?
Unaweza kutenda kitu ukiwa unajua kabisa kwamba umeikosea nafsi yako, umewakosea binadamu wenzio na Muumba wako, lakini ukasema ache iwe!
Kwanini haya yote yanatokea? Mazingira anayokutana nayo mtu katika maisha ndiyo yanayomfanya awe vile alivyo.
Twende pamoja...
BAADA YA KUHITIMU CHUO KIKUU
Naitwa Najma Nelson. Nilisomea ualimu ngazi ya Shahada nikichukua kozi ya Sanaa katika Elimu (Bacholor of Arts in Education) katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini nikahitimu mwaka 2015. Nilikuwa na matumaini makubwa kuwa mara tu baada ya masomo nitaajiriwa na kuanza kufurahia mshahara wangu na walezi wangu.
Wazazi wangu walifariki nikiwa mdogo, hivyo jukimu la malezi alilichukua mjomba wangu.
Kwa bahati mbaya ilipita miaka miwili mfululizo bila kupata ajira kama nilivyotarajia. 'Anti' yangu alianza kunichoka lakini 'anko' ainipa moyo nisikate tamaa.
Kila awamu ajira chache sana zilitangazwa, nami sikuchoka kuomba lakini sikupata. Maisha yalizidi kuwa magumu nikajiona mzigo kwa walezi wangu kwani hata pesa ndogo ya kununua mahitaji madogo niliomba kwa kwa 'uncle' Chale.
Ndani ya hiyo miaka miwili nilikuwa nimejaribu kuomba nafasi za kufundisha katika shule mbalimbali bila mafanikio. Kila mwajiri alisema niache namba zangu kwamba watanitafuta; baadaye hakuna aliyehangaika na mimi.
NDANI YA UJASIRIAMALI
Ilifika kipindi sikuchagua kazi. Nilianza kuomba kazi yoyote iliyojitokeza, kila mahali nafasi zillikuwa zimejaa kwani sasa wasomi walitapakaa mitaani.
Nilibahatika kujiunga na kampuni moja ya mkoani Mbeya iliyofundisha shughuli za ujasiriamali.
Miezi mitatu baadaye kampuni hiyo ilihamishia makao yake Mwanza. Sikuweza kuwafuata lakini nilikuwa nimeiva, ila sikuwa na mtaji. Mjomba alishindwa kunisaidia kwa kuwa naye alikuwa na hali mbaya baada ya mali zake zote kupigwa mnada ili kufidia madeni benki.
NILIVYOBADILI JIINSIA
Kuna mzee aliyeitwa Goran alihitaji vijana watano wa kiume kwa ajili ya kuhudumia ng'ombe wake kijijini. Bosi huyo alikuwa na ng'ombe wa maziwa karibia mia tatu.
Tayari alikuwa ameajili wanaume wengine saba ambao bado hawakutosha. Kwa uhaba wa ajira na ugumu wa maisha ilinishawishi na mimi niombe kazi hii. Lakini kwa vigezo vipi ikiwa mimi ni wa kike?
Cha ajabu hata watoto wa kike wengine pia walijitokeza kuchangamkia tenda Kama mimi. Nilienda kwa machale.
Hakuna msichana waliyemjali kati ya waombaji. Ndipo nilipata wazo la kujifanya MWANAUME. Nilivua heleni na bangili nikavaa mavazi ya kiume nikaiingia kujaribu bahati yangu nikijitambulisha kama John Nelson.
Goran kakuhitaji vyeti wala vitambulisho hivyo alinirahisishia safari. Aidha kilichonibeba ni maumbile ambayo kwa asilimia kubwa yalielekeana na ya kiume.
Licha ya kuwa na umri wa miaka 23 nilikuwa na vijimaziwa vidogo mithiri ya ngumi ya mtoto vilivyofanya kifua changu kuwa 'flat' kiaina na mkalio ya kawaida. Nilinyoa nywele kihuni ili kubadili muonekano.
Ninachoshukuru ni kuwa sura yangu haisemi chochote kuhusu ahalisia wangu. Kilichobaki ni jinsia tu ambayo niliifanya siri. Nilipendelea kuvaa suruali hivyo haikunipa shida kuzoea. Sasa niliona bora niitwe mwanume ilmradi mkono uende kinywani hasa ukizingatia kazi hii ililipa. (Muonekano wangu: downloaded).
NDANI YA KAZI NA JINSIA MPYA
Kila siku tulidamkia kazi ya kukata majani na kuchota maji kwa ajili ya ng'ombe. Wakati mwingine tuliwapa pumba. Baada ya hapo tulikamua maziwa na kujaza kwenye gari maalumu lililopita kukusanya maziwa kila jioni na kupeleka kiwandani. Tulisafisha mazizi na kurudi kwetu tulikopangiwa nyumba na bosi.
Tulikuwa tukiishi watatu au wanne katika kila chumba. Kiukweli ilinipa shida kulala na wanaume chumba kimoja. Katika begi langu nilijaza nguo za kiume na vitu vichache vilivyomuhusu mwanamke mathalani nguo za ndani na pedi kwani nilihudhuria 'period' 'kama kawa.
'Nilipata ugumu hasa wakati wa kuoga. Kila mara baada ya kazi kuisha nilijitahidi kuwahi geto na kuoga kabla wengine hawajafika.
Nilifua nguo zangu za ndani bafuni nikiwa naoga na kuzianika mbali na geto na kuzitoa usiku. Nilihakikisha nililala na nguo na wakati wa kuvaa sikuruhusu jitu linichungulie, lisije likaona 'uhondo.'
Miongoni mwa vijana wawili nilioishi nao, yupo aliyeitwa Fred. Alikuwa akiniganda kama kupe akilazimisha urafiki nami. Katika kuwa naye karibu kuna vitu alianza kunishitukia.
Nafuu ilikuja pale mzee Goran alipotupandishia mishahara na kuruhusu kila mtu aishi nyumba yake. Waliooa walileta familia zao. Kwa wengine ulikuwa wakati wao mwafaka kutamba na wapenzi wao akiwemo Fred. Japo nilijifanya mwanaume, niliingiwa na wivu kumwona na mwanamke mwingine ila sikusema.
Asilimia tisini ya mazungumzo yao yalihusu wanawake. Walinishwishi niwe na mpenzi lakini mimi nilimwajili Daria kama binti wangu wa kazi ambaye alinisaidia kuuza duka. Duka lilisheheni bidhaa nyingi nilizotengeneza mwenyewe.
Baada ya mwaka mmoja na nusu biashara ilifikia thamani ya zaidi ya milioni tatu kutoka laki tano.
Siku moja jioni Daria akiwa amekwenda kuwasalimu wazazi wake kijijini
Nilipigiwa simu na baba yake akinipasha kuwa Daria alikuwa mjamzito. Ilinishitua sana na aliponiambia mimi ndiye niliyemjaza, tena kwa kumbaka.
Hakuna aliyeshangaa kwa sababu sikuwahi kuonakana na mwanamke mwingine zaidi ya binti wa kazi. Walisema kwamba nilijifanya ngumu kumbe natembea na msichana wangu wa kazi!
Kesi iliporindima mahakamani sikuwa na jisi ya kujitetea zaidi ya kuikana jinsia yangu kwa mara nyingine. Hawakuamini. Niliwaonesha cheti changu cha kuzaliwa, vitambulisho vyote pamoja na vyeti vya taaluma. Mjomba na shangazi waliniunga mkono.
Daria aliishangaza mahakama aliposema kuwa baba yake ndiye aliyemshinikiza anibambikie hiyo kesi ili nihukumiwe kwa sababu hakuridhia mwanaye kufanya kazi na mimi.
Alikuwa amekula mahari ya mwanaume aliyetaka amwoe Daria na asije kwangu. Ushahidi wa Daria mbele ya mahakama ndio ulionitoa kwenye hatia.
Nilimwangukia mzee Goran kwa kutokuwa mkweli. Alikuwa ananipenda sana kwa uchapaji kazi wangu hivyo aliniruhusu nirudi kama Najma Nelson na sio John tena.
Nilimrudisha Daria kazini akiwa na kitumbo chake aendelee kuwajibika huku akisubiria kijacho. Vihela nilivyopa baba yake vilimpoza akaziba mdomo. Niliongeza juhudi na umakini katika kazi na nikaanza kufikilia juu ya ndoa. (MWISHO).
WITO: Tusikate tamaa katika kutafuta. Elimu yetu isiwe kigezo cha kutofanya kazi nyingine. Tusichague kazi na tufanye kazi kwa uhalali. Kukosa ajira sio kukosa maisha. Mwisho, serikali hususani wizara husika ione haja ya kutoa Elimu itakayompa mwisho mzuri mhitimu katika UCHUMI wetu.

Upvote
3