SoC02 Nilivyobuni kifaa cha kutatua changamoto ya malipo ya bili za Umeme kwa wapangaji

Stories of Change - 2022 Competition

kmasanja20

Senior Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
128
Reaction score
368
Kubuni na Kutengeneza Kifaa Kinachotatua Changamoto ya Malipo ya Bili za Umeme Kwenye Wapangaji Wengi.
Imeandikwa na: K. Masanja

1659466431531.png

UTANGULIZI
Sayansi na teknolojia katika Dunia ni dhana muhimu sana katika kuleta maendeleo. Licha ya kwamba katika nchi zinazoendelea kuna vikwazo mbalimbali kama kukosa mwendelezo na usimamizi, lakini kupitia taasisi mbalimbali za elimu na wataalamu hapa nchini Tanzania, watu wanaendelea kupata mwamko na kutumia ubunifu katika swala zima la sayansi na teknolojia. Makala hii inaeleza ni jinsi gani nimeweza kutumia elimu na ubunifu kutengeneza kifaa kinachotatua changamoto ya malipo ya vifaa vya umeme vinavyotumiwa na wapangajia zaidi ya mmoja mfano; Fensi za umeme, Taa za nje za ulinzi, Pampu za maji na Geti za umeme.​

TAARIFA YA TATIZO
Kwa mfumo uliopo, vifaa tajwa hapo juu, vinakua vimeunganishwa kwenye mita ya mpangaji mmojawapo, swala ambalo hupelekea mpangaji huyo kudai mchango wa malipo ya umeme wa matumizi wa vifaa hivyo. Kwa sababu mbalimbalii, baina ya wapangaji wamekua wakikimbia, kuchelewesha na kupuuza mchango wa malipo hayo, kitu ambacho kimepelekea upotevu wa muda kukusanya na kudai mchango, migogoro, kutelekezwa, kuhairishwa na kuachwa kwa huduma nzuri zinazopatikana au kutolewa na vifaa hivyo vya umeme.​

NJIA ZILIZOPO ZA UTATUZI WA MALIPO
Mpaka sasa kuna njia tofauti tofauti zimekua zikitolewa ili kujaribu kutatua tatizo la mgawanyo wa ulipaji bili za umeme kwenye apatimenti na nyumba za kupanga. Njia hizi zinatumia mita kama ilivyoelezwa hapa chini.​
  1. Mita shirikishi
    Hii ni njia inayotumiwa kwenye nyumba nyingi za kupanga ambayo wapangaji wote wanakua wameungwa kwenye mita moja. Hivyo ni wajibu wa mpangaji au mwenye nyumba anaeaminiwa kufanya mgawanyo na wapangaji wote kushiriki katika malipo.​
  2. Mita ndogo
    Hii ni njia bora kuliko ile ya kwanza inayotumia mita ndogo ndogo zinazoweza kupima na kuonesha matumizi ya umeme ya mpangaji mmoja mmoja na malipo kupewa yule anaemiliki mita kuu. Kielelezo namba 1, kinaonesha jinsi mita ndogo inavyotumika.​
1659466397762.png

Kielelezo namba 1: Mfumo wa matumizi ya mita ndogo za umeme.

CHANGAMOTO YA NJIA ZILIZOPO
Matumizi ya mita shirikishi na mita ndogo maranyingi huhusisha ukokotozi wa kutumia mikono au kichwa ambao unaathiriwa na makosa ya kibinadamu na kupelekea malipo ya bili yasiyo na uwiano hivyo kufanya njia hizi zisifikie lengo la kutatua changamoto iliopo.​

KIFAA KAMA SULUHISHO LA MALIPO YA UMEME
Baada ya kuona kuwa, njia zilizopo bado hazijakidhi mahitaji ya kutatua tatizo la malipo kwa wapangaji nikaamua kubuni na kutengeneza kifaa ambacho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha malipo ya bili ya umeme. Kielelezo namba 2, kinaonesha picha ya kifaa hicho ambacho kinaitwa Kichagua umeme (APS).​

1659466526514.png

Kielelezo namba 2: Kichagua umeme (APS)

TEKNOLOJIA YA KIFAA NA KILIVYO TENGENEZWA
Kichagua umeme (APS) ni kifaa ambacho moja kwa moja kitachagua nguvu ya umeme kutoka kwenye mita kuu za wapangaji, moja baada ya nyingine kwa muda fulani, ili kuhakikishwa kuwa kila mpangaji anachangia takribani kiasi sawa cha umeme kwenye vifaa wanavyochangia kimatumizi richa ya kua kila mmoja ana LUKU mita yake. Kila mpangaji atanunua umeme wake kama kawaida, wakati ule kifaa kitafanya kazi ya kuchagua umeme kutoka kila mpangaji kwa muda sawa na kupeleka kwenye mfumo wanaochangia matumizi. Kifaa hichi kimetengenezwa na sehemu kuu tatu ambazo zinashirikiana katika utendaji kazi;

Sehemu ya kwanza: Sensa, ambayo imeundwa na rezista zinazotegemea mwanga na diodi zinazotoa mwanga, hivyo kama kuna umeme, diodi zitawaka na rezistensi kwenye rezista itapungua na kuruhusu kiwango kidogo cha volti kwenda sehemu ya pili.

Sehemu ya pili: Kichwa cha kifaa, ambacho kimeundwa na kidhibiti kidogo (maikrokontrola) aina ya Arduino uno kinachopokea taarifa kutoka kwenye Sensa na kutoa maamuzi ya kuswichi yanayofanywa na sehemu ya tatu. Kinatumia lugha ya compyuta na maamuzi yanayotolewa yanategemeana na lugha iliyoandikwa.

Sehemu ya tatu: Swichi, ambayo imeundwa na rilei zinazofunga na kufungua kutokana na taarifa kutoka kwenye Sehemu ya pili. Idadi ya rilei inategemeana na idadi ya LUKU mita au wapangaji waliopo kwenye apatimenti moja. Kielelezo namba 3, kinaonesha muonekano wa kimuunganiko wa ndani na sehemu kuu za kifaa.​

1659466562559.png

Kielelezo namba 3: Muonekano wa ndani wa kimuunganiko wa kifaa.

MFUMO WA UTENDAJI KAZI WA KICHAGUA UMEME KWENYE NYUMBA
Katika mfumo wa utendaji kazi wa kichagua umeme-APS, ni muhimu kuzingatia kuwa, kifaa kitahakikisha, kila mpangaji atatumia muda wa masaa 24 tu kwa kila mzunguko kupeleka umeme kwenye vifaa wanavyochangia. Hivyo kwa wapangaji watatu, watatumia masaa 72 (siku 3) kukamilisha mzunguko mmoja, yaani katika hali ya kawaida ambayo kila mpangaji atakua na umeme, mzunguko utakua; Mpangaji- A, Mpangaji-B, Mpangaji- C, kwa mzunguko wa kwanza, na mzunguko utaendelea kujirudia. Muda ambao umeme wa mpangaji husika utakua unatumika, utaoneshwa na kiashiria cha taa ndogo kama inavyooneshwa kwwenye Kielelezo namba 4, ambacho (a) ni muda wa Mpangaji- A, (b) ni muda wa Mpangaji- B, na (c) ni muda wa Mpangaji- C.​

1659466662202.png

Kielelezo namba 4: Kichagua umeme kwa muda wa Mpangaji- A, Mpangaji- B, na Mpangaji- C.

Kunakipindi ambacho mpangaji husika anakua hana umeme, kipindi hiki kifaa kitachagua mpangaji anaefuata na kipindi tu umeme ukirudi kwa mpangaji ambae hakua na umeme, kifaa kitamrudia na kukamilisha muda ambao alikua amebakiza na mzunguko utaendelea kama kawaida. Kielelezo namba 4, kimetumia taa moja ya umeme lakini kichagua umeme kinaweza kutumiwa kwenye vifaa vingi kama vile; Taa za nje, Geti la umeme, na Pampu ya maji vinavyochangiwa na wapangaji kama inavyooneshwa na Kielelezo namba 5, hapo chini.
1659466717323.png

Kielelezo namba 5: Muonekano wa kichagua umeme-APS, kwenye huduma mbalimbali za umeme kwenye nyumba ya wapangaji wengi.

HITIMISHO
Kifaa hiki kipo kwenye hatua zake za awali za utekelezaji na matumizi lakini kikiboreshwa zaidi kinaweza kwenda mbali zaidi kimatumizi ya umeme ya vifaa vingi vinavyochangiwa na wapangaji na pia hata vile ambavyo havihusishi umeme moja kwa moja kama vile malipo ya bili za maji.

Ubunifu zaidi unahitajika katika sayansi na teknolojia na ubunifu huu uweze kuthaminiwa na mfumo na kupewa kipaumbele ili kuleta mabadiliko yenye tija na kwa vizazi vya baadae. Makala hii imetumika kama mfano lakini katika jamii kuna wabunifu wengi, waliosoma na ambao hawajasoma ambao wakitambuliwa, kuendelezwa na kupewa kipaumbele na Serikali pamoja na mifumo iliopo watakua na mchango mkubwa sana katika sayansi na teknolojia ya nchi yetu.​
 
Attachments

  • 1659466110043.png
    1659466110043.png
    101.1 KB · Views: 98
Upvote 495
Asante Bw. WAZO,
Makala hii haijalenga kuhusu ubunifu wa Mita ndogo kama ulivyosema, bali inahusu kifaa ambacho moja kwa moja kinatoa zamu ya nguvu ya umeme kutoka kwenye Mita kuu au Mita ndogo (kiitwacho Kichagua umeme au APS) kwenye nyumba au apatimenti zenye wapangaji wengi.

Kuhusu idea ya Mita ndogo, hio sio Kenya tu, bali hata Tanzania inatumika miaka kibao na hata hapa ninapoishi pia ipo, nimeifunga na ninaitumia.

Naomba upitie vizuri Makala hii bila shaka utaelewa vizuri.​
Je, hiyo mita ndogo unayo tumia wewe hapa Tanzania ina uwezo wa kila mwenye apartment kuongeza umeme wake ktk mita yake pekee? Na umeme uki kata una kata kwa mhusika mmoja pekee?

Hii ndio mita ndogo nayo ongelea mm hapa. Ina uwezo huo. Kwa TANZANIA TANESCO hawaja anza kuzitoa. Na sidhani kama Tz, hiyo kitu ipo. Ingekuwa ime sambaa mitaani. Ila Tz tuna zile mita ndogo nyeusi kama meter reader tu. Idea mbovu sana. Ila nayo ongelea Nyumba ina kuwa na mita kubwa 1 na sub mita hata 18 kulingana na vyumba au apartments, ambazo kila mmoja ana ongeza yeye peke yake na umeme una kata kwa mmoja tu. Huenda unifafanulie hiyo ya Tz, unayo tumia kama ina function kama hizo nilizo eleza. Size yake na urefu ni sawa na Calculator. Samahani lakini mkuu.
 
Asante.
Kuhusu utendaji kazi wa Mita ndogo niliyokueleza ( na ninayoitumia), nimeieleza vyema kwenye Makala kama njia zilizopo za utatuzi wa tatizo hivyo nakuomba upitie vizuri Makala mwanzo hadi mwisho na utapata picha halisi ya kifaa ninachokielezea mimi pia utaweza kutofautisha na kifaa au mfumo unaousema kuwa upo, halafu tuendelee na mjadala naamini polepole tutaelewana Bw. Wazo.
 
Kubuni na Kutengeneza Kifaa Kinachotatua Changamoto ya Malipo ya Bili za Umeme Kwenye Wapangaji Wengi.
Imeandikwa na: K. Masanja

View attachment 2312386

UTANGULIZI
Sayansi na teknolojia katika Dunia ni dhana muhimu sana katika kuleta maendeleo. Licha ya kwamba katika nchi zinazoendelea kuna vikwazo mbalimbali kama kukosa mwendelezo na usimamizi, lakini kupitia taasisi mbalimbali za elimu na wataalamu hapa nchini Tanzania, watu wanaendelea kupata mwamko na kutumia ubunifu katika swala zima la sayansi na teknolojia. Makala hii inaeleza ni jinsi gani nimeweza kutumia elimu na ubunifu kutengeneza kifaa kinachotatua changamoto ya malipo ya vifaa vya umeme vinavyotumiwa na wapangajia zaidi ya mmoja mfano; Fensi za umeme, Taa za nje za ulinzi, Pampu za maji na Geti za umeme.​

TAARIFA YA TATIZO
Kwa mfumo uliopo, vifaa tajwa hapo juu, vinakua vimeunganishwa kwenye mita ya mpangaji mmojawapo, swala ambalo hupelekea mpangaji huyo kudai mchango wa malipo ya umeme wa matumizi wa vifaa hivyo. Kwa sababu mbalimbalii, baina ya wapangaji wamekua wakikimbia, kuchelewesha na kupuuza mchango wa malipo hayo, kitu ambacho kimepelekea upotevu wa muda kukusanya na kudai mchango, migogoro, kutelekezwa, kuhairishwa na kuachwa kwa huduma nzuri zinazopatikana au kutolewa na vifaa hivyo vya umeme.​

NJIA ZILIZOPO ZA UTATUZI WA MALIPO
Mpaka sasa kuna njia tofauti tofauti zimekua zikitolewa ili kujaribu kutatua tatizo la mgawanyo wa ulipaji bili za umeme kwenye apatimenti na nyumba za kupanga. Njia hizi zinatumia mita kama ilivyoelezwa hapa chini.​
  1. Mita shirikishi
    Hii ni njia inayotumiwa kwenye nyumba nyingi za kupanga ambayo wapangaji wote wanakua wameungwa kwenye mita moja. Hivyo ni wajibu wa mpangaji au mwenye nyumba anaeaminiwa kufanya mgawanyo na wapangaji wote kushiriki katika malipo.​
  2. Mita ndogo
    Hii ni njia bora kuliko ile ya kwanza inayotumia mita ndogo ndogo zinazoweza kupima na kuonesha matumizi ya umeme ya mpangaji mmoja mmoja na malipo kupewa yule anaemiliki mita kuu. Kielelezo namba 1, kinaonesha jinsi mita ndogo inavyotumika.​
View attachment 2312384
Kielelezo namba 1: Mfumo wa matumizi ya mita ndogo za umeme.

CHANGAMOTO YA NJIA ZILIZOPO
Matumizi ya mita shirikishi na mita ndogo maranyingi huhusisha ukokotozi wa kutumia mikono au kichwa ambao unaathiriwa na makosa ya kibinadamu na kupelekea malipo ya bili yasiyo na uwiano hivyo kufanya njia hizi zisifikie lengo la kutatua changamoto iliopo.​

KIFAA KAMA SULUHISHO LA MALIPO YA UMEME
Baada ya kuona kuwa, njia zilizopo bado hazijakidhi mahitaji ya kutatua tatizo la malipo kwa wapangaji nikaamua kubuni na kutengeneza kifaa ambacho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha malipo ya bili ya umeme. Kielelezo namba 2, kinaonesha picha ya kifaa hicho ambacho kinaitwa Kichagua umeme (APS).​

View attachment 2312393
Kielelezo namba 2: Kichagua umeme (APS)

TEKNOLOJIA YA KIFAA NA KILIVYO TENGENEZWA
Kichagua umeme (APS) ni kifaa ambacho moja kwa moja kitachagua nguvu ya umeme kutoka kwenye mita kuu za wapangaji, moja baada ya nyingine kwa muda fulani, ili kuhakikishwa kuwa kila mpangaji anachangia takribani kiasi sawa cha umeme kwenye vifaa wanavyochangia kimatumizi richa ya kua kila mmoja ana LUKU mita yake. Kila mpangaji atanunua umeme wake kama kawaida, wakati ule kifaa kitafanya kazi ya kuchagua umeme kutoka kila mpangaji kwa muda sawa na kupeleka kwenye mfumo wanaochangia matumizi. Kifaa hichi kimetengenezwa na sehemu kuu tatu ambazo zinashirikiana katika utendaji kazi;

Sehemu ya kwanza: Sensa, ambayo imeundwa na rezista zinazotegemea mwanga na diodi zinazotoa mwanga, hivyo kama kuna umeme, diodi zitawaka na rezistensi kwenye rezista itapungua na kuruhusu kiwango kidogo cha volti kwenda sehemu ya pili.

Sehemu ya pili: Kichwa cha kifaa, ambacho kimeundwa na kidhibiti kidogo (maikrokontrola) aina ya Arduino uno kinachopokea taarifa kutoka kwenye Sensa na kutoa maamuzi ya kuswichi yanayofanywa na sehemu ya tatu. Kinatumia lugha ya compyuta na maamuzi yanayotolewa yanategemeana na lugha iliyoandikwa.

Sehemu ya tatu: Swichi, ambayo imeundwa na rilei zinazofunga na kufungua kutokana na taarifa kutoka kwenye Sehemu ya pili. Idadi ya rilei inategemeana na idadi ya LUKU mita au wapangaji waliopo kwenye apatimenti moja. Kielelezo namba 3, kinaonesha muonekano wa kimuunganiko wa ndani na sehemu kuu za kifaa.​

View attachment 2312396
Kielelezo namba 3: Muonekano wa ndani wa kimuunganiko wa kifaa.

MFUMO WA UTENDAJI KAZI WA KICHAGUA UMEME KWENYE NYUMBA
Katika mfumo wa utendaji kazi wa kichagua umeme-APS, ni muhimu kuzingatia kuwa, kifaa kitahakikisha, kila mpangaji atatumia muda wa masaa 24 tu kwa kila mzunguko kupeleka umeme kwenye vifaa wanavyochangia. Hivyo kwa wapangaji watatu, watatumia masaa 72 (siku 3) kukamilisha mzunguko mmoja, yaani katika hali ya kawaida ambayo kila mpangaji atakua na umeme, mzunguko utakua; Mpangaji- A, Mpangaji-B, Mpangaji- C, kwa mzunguko wa kwanza, na mzunguko utaendelea kujirudia. Muda ambao umeme wa mpangaji husika utakua unatumika, utaoneshwa na kiashiria cha taa ndogo kama inavyooneshwa kwwenye Kielelezo namba 4, ambacho (a) ni muda wa Mpangaji- A, (b) ni muda wa Mpangaji- B, na (c) ni muda wa Mpangaji- C.​

View attachment 2312399
Kielelezo namba 4: Kichagua umeme kwa muda wa Mpangaji- A, Mpangaji- B, na Mpangaji- C.

Kunakipindi ambacho mpangaji husika anakua hana umeme, kipindi hiki kifaa kitachagua mpangaji anaefuata na kipindi tu umeme ukirudi kwa mpangaji ambae hakua na umeme, kifaa kitamrudia na kukamilisha muda ambao alikua amebakiza na mzunguko utaendelea kama kawaida. Kielelezo namba 4, kimetumia taa moja ya umeme lakini kichagua umeme kinaweza kutumiwa kwenye vifaa vingi kama vile; Taa za nje, Geti la umeme, na Pampu ya maji vinavyochangiwa na wapangaji kama inavyooneshwa na Kielelezo namba 5, hapo chini.
View attachment 2312405
Kielelezo namba 5: Muonekano wa kichagua umeme-APS, kwenye huduma mbalimbali za umeme kwenye nyumba ya wapangaji wengi.

HITIMISHO
Kifaa hiki kipo kwenye hatua zake za awali za utekelezaji na matumizi lakini kikiboreshwa zaidi kinaweza kwenda mbali zaidi kimatumizi ya umeme ya vifaa vingi vinavyochangiwa na wapangaji na pia hata vile ambavyo havihusishi umeme moja kwa moja kama vile malipo ya bili za maji.
Ubunifu zaidi unahitajika katika sayansi na teknolojia na ubunifu huu uweze kuthaminiwa na mfumo na kupewa kipaumbele ili kuleta mabadiliko yenye tija na kwa vizazi vya baadae. Makala hii imetumika kama mfano lakini katika jamii kuna wabunifu wengi, waliosoma na ambao hawajasoma ambao wakitambuliwa, kuendelezwa na kupewa kipaumbele na Serikali pamoja na mifumo iliopo watakua na mchango mkubwa sana katika sayansi na teknolojia ya nchi yetu.​

Safi sana Mkuu
 
Habari yako ndugu Kmasanja20

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo

Ahsante!!
Tuko pamoja Deogratias
 
Sema umetafssiri tu kwa Kiswahili. Idea siyo yako. Ume kopi na ku paste tu. Hiyo njia ipo Kenya ina tumika miaka kibao (ya mita ndogo). Mm binafsi niliwahi mshirikisha Meneja wa TANESCO Mkoa flani mwaka 2020 wazo hilo. Yeye aka foward kwa wakuu wake Dar. Wakuu wake waka pinga kuwa its Costful to them. Japo ni uongo. Hizo sub meter ata nunua mwenye nyumba mwenyewe na wapangaji wake na siyo TANESCO. TANESCO ina agiza tu na kuwa uzia wateja kama ilivyo hizo za kwenye nguzo.

Inshort, nilichoka na Tz baada kujibiwa hivyo! Ni kajua haya mashirika ya Umma yana ongozwa na watu wenye IQ ndogo kiasi gani. Lakini nili mwakikishia huyo boss, kwa muelekeo wa sasa wa nyumba na Apartments, TANESCO mpende au msipende hiyo technology lazima mta adopt hata kwa lazima tu.
Nili toa huu ushauri bure. Na nili mtumia na Sample za mita (picha). Hata uki google online zipo.
hiki kifaa unachosema wewe kuwa kipo Kenya na uliwashirikisha Tanesco kinaitwaje? ukiweza weka picha hapa jukwaan, je kinaweza kutumika kwa Tanzania kama mtu akiagizia kutokea huko Kenya?
 
Hiko kifaa kipo hapa Tz, niliwahi kuuliza bei kkoo wakati fulani walikuwa wanauza arround 170,000/=Tsh.
 
Bw.Kiduila.
Pia usisahau kupiga kura na kutoa maoni kuhusu kifaa kama ilivyoelezwa kwenye Makala yangu.
Asante.
 
Hongera sana kwa ubunifu mzuri serikali inabidi ilinde haki miliki zenu na panapohitajika support itolewe ili kuwapa motisha wabunifu kama nyinyi. Tanzania tuna watu wenye akili tatizo vipaji vyao havilindwi. Big up and keep it up.

By the way kidude cha kuvote sijakiona mpaka sasa hivi. Nimejaribu sana kukitafuta lakini kwenye simu yangu hakijitokezi.
 
Back
Top Bottom