Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Nakumbuka 2021 kuna mshkaji wangu aliniomba nimsainie line ya simu kwa NIDA yangu kwa sababu alikuwa hana kitambulisho cha Taifa. Basi mimi si nina muamini nikamsajilia kwa wale wakala wanaozungukaga mitaani, kipindi hicho niko Arusha yeye akaenda kufanya mishe zake Morogoro
Baada ya miezi kadhaa, nikapigiwa simu na polisi. Wananiambia nahitajika kuripoti kituo cha polisi. Nilipofika nikaanza kuhojiwa kwa kuhusu kesi ya uhalifu wa kimtandao na utapeli wa pesa kupitia simu.
Nimebaki tu natoa macho maana sielewi wanaongea nini. Baadae nikamuelezea afande kuwa mimi nilimsajilia mtu flani na hiyo namba mimi siitumii. Wakapiga ile namba kwenye simu yangu haipokelewi, na hakuna njia ya kuthibitisha kuwa nilimsajilia laini hiyo kwa uaminifu.
Ikabidi niingie gharama za kulipa watu waliodai kutapeliwa ilikuwa kama milioni 1 na laki 3 hivi ikanitoka. Nimetoka hapo nimeenda nyumbani kwa mhusika familia yake inasema hata wao hawampati.
Wakuu wewe ulikutana na kisa gani kwa kumsajilia mtu line ya simu?