Nilivyokasirishwa nikaenda tazara nikang'ata reli nikarudi nyumbani

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,042
Reaction score
3,095
wakuu kutoka kwenye stori yangu kunakitu unaweza kujifunza kwangu ukachukua na kukitumia siku fulani:

Siku moja nilikasirika sana.
Sio ile hasira ya kawaida. Ilikuwa ile hasira ambayo unahisi kama kichwa kinataka kupasuka na mtu akikuuliza swali dogo tu unaweza kujibu vibaya au umpige.

Nilikaa dakika chache nikagundua kitu kimoja: nikibaki pale nitaharibu mambo.

Basi nikaondoka.

Sikumwambia mtu naenda wapi, sikuchukua ushauri wa mtu yeyote. Nilitembea moja kwa moja mpaka nikafika TAZARA. Pale kwenye reli nikasimama nikaiangalia reli kwa sekunde kadhaa.

kisha nikang’ata reli kwa hasira zote...

Baada ya hapo nikanyanyuka, nikajipangusa vumbi, nikageuka nikarudi nyumbani.

Njiani nikagundua hasira yote imeisha.

Watu wengi wakikasirika wanagombana, wanatukana au wanaharibu mahusiano. Mimi siku hiyo niliamua kwenda kung’ata reli kisha nikarudi.

Somo ni rahisi tu:
Ukikasirika sana, usifanye maamuzi makubwa. Tafuta kitu cha kwaida kitakachokutoa kwenye ile hali ya hasira

Sio lazima kung’ata reli… unaweza ukaenda dukani ukanunua mandazi ya miatano ( hapa atakufungia kwenye gazeti au mfuko ). unatupa mandazi kisha unatafuna gazeti. mbinu za kawaida kama hizi mimi huzitumia na zina saidia sana ku deal na vitu vidogovidogo
 
Huwa naondoka kwa mda eneo la tukio mpaka nikipoa narudi.
Sema kwa wanandoa hii njia ni ngumu, maana mnagombana saa 7 usiku na ukute mpo nje ya mji huko hamna pa kwenda.
Na ndio maana wengi wanaishia Kupigana.
 
Back
Top Bottom