wakuu kutoka kwenye stori yangu kunakitu unaweza kujifunza kwangu ukachukua na kukitumia siku fulani:
Siku moja nilikasirika sana.
Sio ile hasira ya kawaida. Ilikuwa ile hasira ambayo unahisi kama kichwa kinataka kupasuka na mtu akikuuliza swali dogo tu unaweza kujibu vibaya au umpige.
Nilikaa dakika chache nikagundua kitu kimoja: nikibaki pale nitaharibu mambo.
Basi nikaondoka.
Sikumwambia mtu naenda wapi, sikuchukua ushauri wa mtu yeyote. Nilitembea moja kwa moja mpaka nikafika TAZARA. Pale kwenye reli nikasimama nikaiangalia reli kwa sekunde kadhaa.
kisha nikangβata reli kwa hasira zote...
Baada ya hapo nikanyanyuka, nikajipangusa vumbi, nikageuka nikarudi nyumbani.
Njiani nikagundua hasira yote imeisha.
Watu wengi wakikasirika wanagombana, wanatukana au wanaharibu mahusiano. Mimi siku hiyo niliamua kwenda kungβata reli kisha nikarudi.
Somo ni rahisi tu:
Ukikasirika sana, usifanye maamuzi makubwa. Tafuta kitu cha kwaida kitakachokutoa kwenye ile hali ya hasira
Sio lazima kungβata reliβ¦ unaweza ukaenda dukani ukanunua mandazi ya miatano ( hapa atakufungia kwenye gazeti au mfuko ). unatupa mandazi kisha unatafuna gazeti. mbinu za kawaida kama hizi mimi huzitumia na zina saidia sana ku deal na vitu vidogovidogo